Home Latest News Klabu za England ngoma nzito Uefa

Klabu za England ngoma nzito Uefa

1334
0
SHARE

MICHUANO ya klabu Bingwa Barani Ulaya inaendelea wiki ijayo, huku kukiwa na mtihani mgumu kwa klabu za England kujiweka katika mazingira mazuri ya kufuzu hatua ya 16 bora. Hali hiyo inatokana na ukweli kuwa katika mechi za kwanza hatua ya makundi hazikufanya vema, hivyo kutakiwa kujipanga katikati ya michuano hii ili kurejesha heshima zao ndani ya Uefa.

Hali hiyo inatokana na ukweli kuwa ukiiacha Chelsea pekee, nyingine zote zilizosalia ziliambulia vipigo, hivyo kutakiwa kushinda mechi zijazo ili kurejesha matumaini ambayo tayari yameshawatia shaka mashabiki wao, japokuwa bado ina michezo mitano. Katika mechi za kwanza hatua ya makundi, Chelsea iliiadhibu Makab Tel Aviv kwa mabao 4-0. Arsenal ambayo inaonekana kuwa na matokeo mabaya katika Ligi Kuu ya England msimu huu, katika mechi ijayo ya Uefa itakutana na Olimpiakos na kutakiwa kushinda mchezo huo ili kujiweka katika nafasi nzuri kutoka Kundi F kuelekea hatua itakayofuata.

Meneja wa Arsenal, Arsene Wenger, amekuwa na kipindi kigumu hivi karibuni kwa kupoteza michezo muhimu katika ligi tofauti inazoshiriki, ikiwemo ya Uefa kwa kuchapwa mechi ya kwanza dhidi ya Dynamo Zagreb ya Croatia kwa mabao 2-1 na Ligi Kuu ya England, kwani hivi karibuni ilichapwa na Chelsea.

Dinamo Zagreb waliochukua ubingwa wa Croatia 2014/2015 sasa watasafiri mpaka Alianz Arena kucheza na mabingwa hao wa Ujerumani 2014/2015, Bayern Munich. Klabu ya Bayern Munich kutokea Ujerumani wanaongoza kundi F kwa jumla ya pointi tatu na watakuwa na upinzani mkali watakapovaana na Dinamo Zagreb walio katika nafasi ya pili kwa pointi 3, kwa tofauti ya mabao ya kufunga na kufungwa.

Bayern wapo katika nafasi nzuri pia katika msimamo wa Ligi Kuu nchini Ujerumani ‘Bundesliga’ wakiwa katika nafasi ya pili kwa jumla ya pointi tano kwa kushinda michezo yake yote mitano. Kocha Jose Mourinho atakuwa na kibarua kizito Chelsea itakapovaana na Porto, timu aliyoifundisha msimu wa 2002- 2004 katika Ligi Kuu ya nchini Ureno. Chelsea wana nafasi ya kushinda mchezo huo kutokana na kiwango kizuri wanachokionesha hivi sasa kwa kushinda michezo mitatu ya mwisho kati ya mitano waliyocheza.

Porto wapo katika nafasi ya pili kwa pointi moja waliyoipata kwenye mchezo dhidi ya Dynamo Kyiv kwenye mchezo wa awali wa kundi G. Klabu ya Manchester City itakabiliana na Borusia Monchengladbach katika mchezo wa kundi D, huku wakiwa na kumbukumbu ya kichapo kutoka kwa Juventus kwenye mchezo wa kwanza.

Man City wameshinda jumla ya michezo 3 katika michezo mitano ya mwisho waliyocheza na kupoteza michezo miwili katika michuano yote waliyoshiriki. Kibibi kizee cha Turin, klabu ya Juventus ya nchini Italia watacheza mchezo wao wa pili kutoka kundi D dhidi ya Sevila, wanaoongoza kundi hilo kwa tofauti ya mabao. Sevila ya nchini Hispania waliwachapa Monchengladbach 3-0 katika mchezo wao wa kwanza na Juventus wakiwachapa City mabao 2-1.

Manchester United watacheza dhidi ya Wolfsburg ya Ujerumani walio katika nafasi ya pili ya kundi lao, mara baada ya kuwachapa CSKA Moskva. Man United, wanaofundishwa na Louis Van Gaal walipoteza mchezo wao wa kwanza kwa kufungwa bao 2-1 na PSV na watatakiwa kujihakikishia ushindi ili kuweza kusonga mbele. Van Gaal amekuwa na kikosi kizuri hivi karibuni, huku kinda mpya, Anthon Martial akifufua zaidi matumaini ya timu hiyo kwa kupachika mabao 3 katika mechi zake 2 za kwanza. Katika kundi A klabu ya Real Madrid ya nchini Hispania itasafiri mpaka Sweden kwa ajili ya kukipiga na Malmo.

Madrid wanaonekana kuwa katika kiwango kizuri hivi sasa mara baada ya kushinda kwa jumla ya mabao 11 kwenye mechi zake tatu zote za mwisho kwenye michuano tofauti.

Madrid walishinda mabao 4-0 dhidi ya Shaktar Donetsk kwenye mchezo wake wa kwanza, huku wakimtumia vizuri winga Christian Ronaldo katika safu ya ushambuliaji. Shaktar Donetsk walimaliza katika nafasi ya pili kwenye msimamo wa Ligi Kuu ya Ukraine msimu wa 2014/15 na wapo katika nafasi ya pili msimu huu kwa kushinda mechi 6 kati ya 8 za ligi hiyo.

PSG walio katika nafasi ya pili nyuma ya Madrid kwenye kundi A nchini Hispania katika michuano ya Uefa watacheza dhidi ya Shaktar kwenye mchezo wao wa pili hatua hiyo ya makundi. Klabu hiyo ipo katika nafasi ya kwanza katika Ligi Kuu nchini Ufaransa na inaonekana kuwa vizuri kutokana na kuwa na safu nzuri ya ushambuliaji inayoongozwa na Edinson Cavan pamoja na Ezequiel Lavezi.

Barcelona, wenye pointi 1, watawaalika klabu ya Ujerumani, Bayer Leverkusen, katika dimba la Nou Camp katika mchezo wa kundi E, huku wakiwa na wakati mgumu mbele ya timu hiyo inayoongoza kundi hilo mara baada ya kuwachapa Bate Borisov kwenye mchezo wa awali.