Home Habari Korosho kufyeka vigogo zaidi

Korosho kufyeka vigogo zaidi

3238
0
SHARE

NA MWANDISHI WETU

UMAKINI na ufuatiliaji wa hali ya juu wa oparesheni ya kupakia, kusafirisha na kuwalipa wakulima fedha za korosho unatajwa kuwa kaa la moto kwa baadhi ya vigogo serikalini pamoja na wafanyabishara wa zao hilo. RAI linachambua. Hadi kufikia sasa zao hilo limesha ‘fyekelea mbali’ vigogo saba wa serikali, wanasiasa na tayari wafanyabiashara na wananchi zaidi ya 20 wakitiwa mbaroni na Jeshi la polisi na wengine kuburuzwa mahakamani.
Taarifa ambazo RAI imezipata kutoka, Lindi, Mtwara na Ruvuma zimebainisha kuwa baadhi wafanyabishara, viongozi wa kuchaguliwa, kuteuliwa na hata wa kuajiriwa, walikuwa wakilitumia zao hilo kufaidika hasa nyakati za msimu kama ilivyo sasa.Hata hivyo, pamoja na Rais Dk. John Magufuli kulivalia njuga zoezi hilo, bado wapo baadhi ya watu kwa makusudi wanataka kuendeleza utaratibu usiofaa wa kuwalangua wakulima na kujipatia kipato isivyo halali.RAI limeelezwa kuwa tayari mfumo wa kufanya mambo kwa mazoea umeshawagharimu na utaendelea kuwagharimu baadhi ya viongozi kama ilivyomtokea kwa diwani wa Kata ya Nalasi Magharibi (CUF), Alfa Kabango ambaye anadaiwa kushiriki kwenye ulanguzi wa korosho.Kabango na watu wengine saba wanadaiwa kulangua korosho kutoka kwa wakulima kwa bei Sh. 1,500 na wengine wakibadilisha korosho na nyama ya ng’ombe.Tayari baadhi ya viongozi wa mikoa na wilaya akiwamo Mkuu wa wilaya ya Tunduru, Juma Homera wamesema oparesheni ya kushughulika na walanguzi ni endelevu na hasa ikizingatiwa kuwa nia ya Rais Magufuli ni kutaka kuona mkulima anafaidika na zao hilo hatua inayowaweka pabaya viongozi na wafanyabiashara waovu.Hivi karibuni Rais Magufuli alitangaza hadharani nia ya kutaka wakulima wafaidike na jasho lao na kuweka wazi kuwa serikali yake itazinunua korosho zote nchini kwa bei ya Sh. 3,300 na kuliagiza Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) kusimamia zoezi hilo.Kiasi kikubwa cha korosho kinakadiriwa kulimwa kwenye mikoa ya Mtwara, Lindi na Ruvuma ambako hadi sasa korosho inayodaiwa kuwa ghalani ni tani 90,232 huku uzalishaji kwa mwaka huu ukikadiriwa kutozidi tani 220,000.
VIGOGO WALIONG’OLEWA NA KOROSHOWakati zoezi hilo likiendelea tayari wapo vigogo wa juu serikalini waliong’olewa kwa sababu mbalimbali zinazohusiana moja kwa moja na zao la korosho.
MKURUGENZI CBTSakata la korosho lilianza taratibu Aprili mwaka huu baada ya aliyekuwa Waziri wa wizara ya kilimo, Dk. Charles Tizeba kusitisha mkataba wa kazi wa aliyekuwa Mkurugenzi wa Bodi ya Korosho Tanzania, Hassan Jarufo.
Dk. Tizeba alitangaza uamuzi huo Aprili 21, na kubainisha kuwa sababu za kuagiza kusimamishwa kazi kwa mkurugenzi huyo, ni kutoridhishwa na upatikanaji wa viuwatilifu kwa wakati katika kustawisha zao hilo.“Hizi hatua tunazochukua ni kuhakikisha kuwa wadau wakubwa wa korosho ambao ni wakulima wanaendelea kunufaika na zao lao, hivyo wakulima wasiwe na wasiwasi kwani pamoja na kuondolewa Mkurugenzi huyo shughuli za serikali zitaendelea kama kawaida na maslahi yao yatasimamiwa ipasavyo” alisema.KAIMU MKURUGENZI CBTAidha, Wizara ya kilimo ilimtangaza Profesa Wakuru Magigi kukaimu nafasi ya Mkurugenzi wa Bodi hiyo ambaye alidumu hadi Oktoba mwaka huu.
Mkurugenzi huyo alitumbuliwa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa huku Rais Magufuli akiunga mkono hatua hizo na kuagiza Profesa Magigi kurudishwa wizarani.DK. TIZEBA, MWIJAGENovemba 10 mwaka huu, moto wa korosho ulihamia kwa mawaziri, ambapo Rais Magufuli aliwatimua mawaziri wawili katika baraza lake.
Mawaziri hao ni aliyekuwa Waziri wa Kilimo, Dk. Charles Tizeba na aliyekuwa Waziri wa Viwanda na Biashara Charles Mwijage.Rais Magufuli alieleza hadharani sababu za kutengua uteuzi wa wawili hao kwa kudai kuwa ni kuendelea kuzorota kwa sekta ya kilimo na viwanda.Alisema licha ya kuwa sekta za kilimo na viwanda ni nyeti na muhimu kwa maendeleo ya Watanzania, lakini zaidi ya asilimia 60 ya Watanzania ambao ni wakulima muda mrefu wamekuwa vibarua wa watu wenye uwezo katika mazao yote.
Baadhi ya sababu hizo ni jinsi mawaziri hao walivyoshindwa kushughulikia suala la bei ya Korosho, Kahawa, Pareto na ufufuaji wa kiwanda cha Chai Mponde kilichopo Tanga na kile cha Buko kilichopo   mkoani Lindi.Akizungumzia suala la korosho alisema:  “Sikuona statement (taarifa) yoyote ya Waziri wa Viwanda au Kilimo hata kuwakemea sekta binafsi.”DK. ANNA ABDALLAHAidha, panga hilo pia lilimkumba aliyekuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Korosho, Dk. Anna Abdallah baada ya Rais Magufuli kuivunja bodi hiyo Novemba 10 mwaka huu.
WAKURUGENZI WATUMBULIWAWakati sakata hilo la korosho likiwa halijapoa, Waziri mpya wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Joseph Kakunda naye alifanya maamuzi magumu kwa kuwatumbua Wakurugenzi wawili kwa madai ya uzembe ambao umesababisha kuzorota kwa viwanda vya korosho.Wakurugenzi hao ni Isaac Legonda aliyekuwa Mkurugenzi wa maendeleo ya viwanda na Augustino Mbulumi ambaye alikuwa Mkurugenzi wa Usimamizi wa Maghala.Kakunda alitangaza uamuzi huo Novemba 13 mwaka huu baada ya kutembelea viwanda vya mikoa ya Lindi na Mtwara na kukuta hali mbaya ikiwa ni pamoja na viwanda vingi kugeuzwa maghala.
20 MBARONITangu sakata hilo la korosho lianze pia kumeshuhudiwa na vibweka mbalimbali ambavyo kwa namna moja au nyingine pia vimesababisha zaidi ya wa 20 wanaojihusisha kununua korosho kwa utaratibu usio rasmi kwa wakulima, maarufu kama ‘kangomba’ kukamatwa mkoani Ruvuma.
Mkuu wa Wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma, Juma Homera, alisema watu 14 tayari wamefikishwa mahakamani. “Wananchi walitutumia sms (ujumbe mfupi wa simu) na tulitumia pia vyanzo vyetu vingine vilivyoko vijijini kubaini kangomba,” alisema Homera.
Hatua hizo zinadaiwa kuwa mwendelezo wa korosho kuwa kaa la moto kwa viongozi wa serikali, wafanyabiashara na hata wananchi wasiokuwa waaminifu.
Baadhi ya wasomi waliielezea hatua mbalimbali zilizochukuliwa na serikali ikiwamo ile ya sasa ya kununua korosho yote ya msimu huu kwa bei ya Sh. 3,300, kama hatua nzuri, lakini inayohitaji kuzingatia misingi ya uchumi.Mhadhiri wa Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam(UDSM), Dk. Benson Bana mbali na kuusifu na kufananisha na njia alizopita muasisi wa Taifa la China, Mao Zedong, lakini alisema bado hajaelewa mageuzi anayoyafanya Rais Dk. Magufuli yanasimama katika msingi wa falsafa ipi ya kiuchumi.“Kama ilivyokuwa kwa Mao Zedong nasi tunaweza kusema tunayaona mabadiliko makubwa ambayo hatujui kama yanaongozwa na itikadi fulani au fikra sahihi za Rais,” alisema Dk. BanaAlisema, daima nchi zote panapotokea suala la mvutano wa bei kama ilivyokuwa katika sakata la korosho, Serikali huingilia kati kwa sababu sekta binafsi inayoongozwa na wachache haiwezi kuachiwa iendeshe uchumi.Kwa upande wake mchambuzi wa masuala ya siasa, Dk Azaveli Lwaitama alisema uamuzi wa Rais Dk. Magufuli wa kuingilia