Home Makala KUMBE YALIKUWA MABADILIKO YA CHAMA!

KUMBE YALIKUWA MABADILIKO YA CHAMA!

1340
0
SHARE

NA MARKUS MPANGALA


TANGU mwanzoni, wakati na baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka jana kuna masimulizi mengi ninayoambiwa kuhusiana na suala la mabadiliko. Tena masimulizi hayo yamekuwa mengi na mengine yamekuwa hewa, pamoja na atoke huyu aingie yule basi; ndiy o mabadiliko! Looh!

Dhana ya mabadiliko ilikuwa imepata upenyo. Ikadakwa na kila mwanasiasa. Ikasimuliwa kwa walevi, wakavu, wagonjwa, walemavu, vipofu, viziwa na kila aina ya binadamu. Tuliambiwa mambo mengi kuhisiana na suala la mabadiliko.

Uzuri wa dhana ya mabadiliko haikumilikiwa na upande wowote wa siasa. ukisikilzia hotuba za wagombea wa udiwani, ubunge hadi urais kwa upane wa UKAWA habari ilikuwa ileile ya mabadiliko. Kwa upane wa chama tawala hali ilikuwa ileile kw awagombea wake walianza kuimba mabadiliko.

Dhana ya mabadiliko ilishika kasi mno. Kila mmoja akawa anaimba kadiri aonavyo na kuelewa. Yalikuwa mabadiliko yaliyowateka wanasiasa, wananchi na wengineo. Tuliambiwa ni mwaka mabadiliko.

Tuliambiwa juu ya mabadiliko ya elimu. Tualiambiwa utoaji wa elimu bure kutoka chekechea hadi vyuo vikuu. Hayo yalisisitizwa na wagombea wa UKAWA.

Pia tuliambiwa elimu bure kutoka shule ya msingi hadi sekondari kwa upande wa Chama cha Mapinduzi (CCM). Ingawa wimbo wa elimu bure ulidakwa kutokana na sera ya elimu, kwahiyo masikioni mwangu haukuwa mpya na wala haukustahili kuwa sehemu ya ilani ya vyama vya siasa, kwa maana hawakuwa na ubunifu wowote.

Tulieleza kuhabarishana na kusisitiziana juu ya mabadiliko. Mwishowe mgombea wa CCM, John Magufuli alishinda uchaguzi mkuu kwa asilimia 58.  Matokeo hayo hayakuwa mazuri kwa UKAWA, huku baadhi ya wafuasi wakionyesha kukata tamaa na wengine kutamka bayana kuchikizwa nayo. Ninatambua kuwa lilikuwa suala la kawaida na halipaswi kutumika kama kejeli, bali kuwapa moyo kushindana wakati mwingine.

Baadhi yeti ni miongoni mwa waliokubali dhana ya mabadiliko.  Tulikubali dhana hiyo miaka 7 iliyopiga kabla ya ngonjera za uchaguzi wa mwaka jana. Tulikuwa na sababu za msingi na tuliamini tutabadilika endapo tutazitendea haki ripoti za Mkaguzi na Mdhibiti wa Hesabu za Serikali.

Tulikerwa namna ripoti za CAG zilivyogeuzwa kuwa kittikio cha wimbo wa matumizi mabaya ya mali za umma. Tulikerwa tukiamini inawezekana kuondokana nalo na kujenga jamii inayothamini na kuheshimu mali za umma.

Tunaamini hilo lilijenga taswira kuhitaji kiongo thabiti na mwenye uamuzi imara. Kiongozi mwenye kiburi na kutenda kinyume cha matarajio kwamba ataenenda kwa kauli tamu tamu kama za huduma kwa wateja. Tulihitaji rais mwenye ukali ikibidi kupindukia.

Tuliamini nchi yetu ilihitaji kiongozi mwenye kudhibiti mambo ya hovyo yalikuwa yameota mizizi. Tuliamini tunaweza kumpata hata ndani ya CCM kwakuwa bado tunaamini wapo makada wao wenye uwezo wa kubadilika na kuleta mabadiliko.

Tuliamini pia wapo makada wa UKAWA wenye uwezo wa kubadilisha mambo katika nchi yetu. Tuliamini wanaweza kwakuwa punje ya uwezo wao ilionekana. Bahati mbaya likafanyika kosa la karne. Ulikuwa mwisho wa matamanio ya mabadiliko.

Hata hivyo kuibuka kwa John Magufuli kulikuwa na matumaini mapya. Kulikuwa na mtazamo mpya. Kuliibua fikra mpya na kwamba sasa tunakwenda kujenga misingi ya kijamii na wajibu. Tunakwenda kujenga sekta binafsi yenye misingi na uimara. Tunakwenda kujenga nidhamu na kiburi cha kitaifa kama vile ambavyo Mwenyekiti Mao Tse Tung alivyofanya kule China.

Katika mazingira hayo ndipo tuliamini na tutaendelea kuamini hata ifikapo mwaka 2020 John Pombe Magufuli anafaa, anastahili na ndiye lilikuwa chaguo bora zaidi kati ya wagombea wote walioomba ridhaa kwetu wananchi. Hatuamini kusema hivyo ni kubeza uwezo wa washindani wake, lakini kanuni za mchuano zinafahamika kuwa lazima apatikane mshindi na washindwaji. Hakuna namna nyingine.

Pamoja na kuamini kuwa Magufuli anastahili haina maana kwamba hana dosari. Hata hivyo tunaamini katika dosari hizo yapo mambo yanarekebishika, na yatafanikiwa.

Kitu ambacho hatukuelewa wakati wa mbiu za mabadiliko ni nini falsafa yake ya wakati huo wa uchaguzi. Tulifahamu juu ya falsafa ya mabadiliko ni pamoja na kusimamia misingi ya uadilifu pamoja na kubadilika hatua kwa hatua.

Tuliamiani kubadilika huko ni pamoja na kuzibadili akili na mitazamo yetu. Tuliamini hivyo kwakuwa hakuna mabadiliko yoyote yanayofanikishwa katika jamii yoyote na nchi yake pasipo kubadili fikra zake.

Madhumuni yetu yalikuwa kuhakikisha serikali inachukua hatua juu ya orodha ya wauzaji wa dawa za kulevya badala ya kujivunia kumiliki orodha na kuwafahamu pekee. Tuliamini kuwa falsafa ya mabadiliko ni pamoja na kujiandaa kuhimili mitikisiko yake. Tuliamini hiyo ndiyo njia pekee ya kukabiliana na mawimbi ya mabadiliko. Tukajianda kwa hilo, ndiyo maana manung’uniko yanayoendelea sasa, wengine hatutikisiki.

Kwenye dhana hiyo ya mabadiliko tunadhani watu wengi wametekwa kwenye haya mambo ya kutafuta visingizio. Tuliona na tulijua uhalisia wa Tanzania wakati wa kampeni. Tulisikia watu wakiimba kwa mikogo na madoido mabadiliko! Mabadiliko! hata asi tukafurahi.

Kama nilivyosema awali kuwa, baadhi yetu tulifahamu makusudio ya mabadiliko na tulifahamu falsafa yake. Lakini ukiwauliza baadhi ya waimbaji mabadiliko anayoyataka wala hayafahamu. Hapo tulijua kumbe watu hawaelewi kinachoendelea. Lazima tuambizane kuwa mbaaidliko tuliyoimba hayakuwa na maana kwamba ajitokeze mtu wa kumfanyia kazi mwananchi nyumbani kwake. Lazma watu wafikiri zaidi.

Tunaamini kuwa Magufuli anawabana watu kwenye kona zao itabidi wafikirie zaidi au wafe njaa. Haiwezekani watu walioimba mabadiliko hawajui kubadilika kifikra. Hawajui mabadiliko ni hatua na vitendo. Sijui walitaka mabadiliko ya kuketi kwenye sofa na kuletewa mlo.

Ulalamishi ni mwingi na wanatumia muda mwingi kulalamika. Lakini hawatumii muda huo huo kufikiri mambo chanya. Eti oohh! uchumi unayumba….. swali ni kuwa: wewe inakuadhiri vipi? Wakati wanasema uchumi unapanda huwa unakuathiri? Ni maneno ya kisiasa tu.

Ili tukubali mabadiliko lazima tukiri inahitajika juhudi kubwa kupunguza pengo la walionacho na wasionacho.. Watu walijilimbikizia mihela huku wengine wakiwa maskini wa kutupwa. Kwahiyo njia nzuri ya kubadili hayo ni kutumia akili.

Tunasahau kuwa tunachoona sasa ni matokeo ya ulaji rushwa uliopindukia. Na ili kuondokana na hali hiyo ni lazima kukabiliana nayoi kwa sura kavu, chungu na uso wa mbuzi. Ni lazima kutikisa kuta za walaji rushwa ambao walitengeneza himaya ya uchumi usiokuwa na mizizi.

Hili ni funzo la kuonyesha  namna rushwa inavyoathiri jamii na taifa. Tunapoamua kukagua vyeti maana yake tunaondoa uozo uliokumbatiwa kana kwamba ndiyo msingi wake. Ona watu waliokuwa hawana vyeti lakini walikuwapo kazini.

Muumini wa mabadiliko hawezi kuchukua uhakiki wa watumishi wa umma. Hawezi kuchukia uhakiki wav yeti vya watumishi. Hawezi kuchukia mapambano dhidi ya rushwa. Hawezi kuchukia urekebishwaji wan chi. Hawezi kuimba mabadiliko kisha akachukia hatua za kubadilika.

Kumbe wapo wanaochukia mabadiliko hayo kwakuwa chama chao hakikushinda. Wanachukia kwakuwa matamanio yao yalikuwa kubadili chama cha kuongoza nchi wala hawakuwa na mpango wa mabadiliko kwa kutazama nani anafaa kubadilisha mambo.

Baadhi yetu tunaipenda sana Tanzania na hatutaki kusikia tena zile blah blah blah nyingi za nchi masikini ili tupate kisingizio cha kuridhika. Ni lazima tuyapende mabadiliko na hatua zake pamoja na maitikisko yake. Katika hilo tusitaniane tafadhali.