Home Habari Kuna mengi yanayotishia uhai wa binadamu

Kuna mengi yanayotishia uhai wa binadamu

1377
0
SHARE

NA MARKUS MPANGALA

BINADAMU anakabiliwa na changamoto nyingi katika mazingira; afya yake, matokeo ya uchumi na viwanda, hali ya hewa na madhara ya umasikini.  Wiki iliyopita tulieleza hatari ya utamaduni unaozoeleka wa matumizi ya silaha za kemikali na baolojia na kuhatarisha maisha ya binadamu. 

Leo tunakuletea masuala ambayo yanahatarisha uhai wa mwanadamu. Tunatambua hakuna binadamu atakayeishi miaka zaidi ya 200 hapa duniani, lakini wanawajibika kulinda mazingira ya sasa kwa manufaa ya kizazi kingine.  

1. Vita ya Nyukilia

Silaha za nyukilia zimekuwa zikitumiwa kama nyenzo ya kutafuta upatanisho baina ya mataifa ya Korea Kaskazini  dhidi ya Korea Kusini na Marekani kwa upande mwingine. 

Silaha hizo zimewahi kutumiwa katika shambulio la Hiroshima na Nagasaki wakati w avita vya kwanza vya dunia, lakini sasa silaha za nyukilia zinaelekea kuwafikia hata makundi ya kigaidi. Litakuwa jambo baya zaidi kama wanadamu watadhani kuwa vita dhidi ya silaha za nyukilia haiwezekani.

Kwa mujibu wa mwandishi H.G Wells, kupitia kitabu chake cha ‘The Time Machine’ anasema ulibaki muda mfupi kabla ya mgogoro wa Cuba na Marekani kutumbukia kwenye vita vya nyukilia. 

Utafiti unaonesha kuwa nchi moja kati ya tatu, zina uwezekano wa kumiliki silaha za nyukilia. Uwezekano huo kwa sasa umefikia asilimia. 

Nchi mbali mbali zimekuwa kwenye hekaheka za kumiliki mitambo ya makombora ya nyukilia, uhusiano mbaya kati ya Marekani na Urusi, ni ushahidi tosha juu ya vita vya silaha vya nyukilia zilivyo mbaya. 

Matumizi ya silaha za nyukilia baina ya mataifa makubwa yanaweza kuua maelfu kati ya mamilioni ya watu moja kwa moja na kwa muda mfupi au kutokea miaka michache ijayo.

Mathalani bomu la Cobalt, linatajwa kuwa moja ya silaha hatari ambayo inaweza kumuua kila mmoja. Lakini ipo kwenye majaribio na utengenezaji wake ni ghali zaidi. 

Athari za matumizi ya silaha za nyukilia zinaweza kutokea kwenye sekta ya kilimo ambako itasababisha mabilioni ya watu kukosa chakula. Na kusababisha magonjwa.

2. Majanga ya asili. 

Majanga ya asili yamechukua uhai wa watu wengi kuliko vita. Hata hivyo majanga ya asili sio kitisho kinachoishi; kwa sababu kuna watu wamezuia virusi kuathiri maisha yao. Kusambaa kwa magonjwa ambayo hayazuiliki, ni miongoni mwa majanga yanayomkabili mwanadamu. 

Ushahidi wa hili ni kuenea ugonjwa wa kaswende, umekuwa sugu na tishio kwa wananchi wa Bara la Ulaya. Magonjwa yanayotokana na virusi vya panya vimekuwa hatari kwa maisha ya mwanadamu. 

Majanga mengine ni kama vile vimbunga ambavyo wananchi wa Msumbiji waliathiriwa kimbunga Idai. Siku chache baadaye nchi hiyo ikashuhudia takribani wanancnhi 380,000 wakiwa hatarini kutokana na kukabiliwa na kimbunga kingine Keneth.

Nchini Zimbabwe wananchi nao wamekuwa wakikabiliana na kimbunga Keneth. Mataifa ya Malaysia,Cambodia,Pakistan, Marekani,Thailand,

Mikoa ya Tanzania ya Pwani,Lindi, na Mtwara ilitikiswa na tishio la kimbunga Keneth. Baadhi ya mataifa yamekumbwa na vimbuka vya Fani, Idai, Phailin, Hudhud, Nilofar, Haiyan, Vardah, Viyaru, Aila, Nargis,Irma, Gonu,Gaja,Mekunu na vingine vingi. 

Majanga hayo yamekuwa yakiungana na matetemeko ya ardhi pamoja na mlipuko wa volcano yamekuwa tishio katika maisha ya mwanadamu hapa duniani.

3. Ubunifu

Uwezo wa kiakili ni jambo lenye nguvu kubwa duniani. Ni kigezo kimojawpao cha kutatua matatizo mbalimbali na kuratibu mipango, hiyo ni kwanini viumbe wengine hawakupewa zaidi ya binadamu. 

Ili binadamu aendelee kuishi anategemea zaidi uamuzi wake, wa nini cha kufanya na kipi si cha kufanya. Kuwa mwenye akili ni faida halisi kwa mtu na taasisi yoyote ile, kwahiyo kupiga hatua za kuboresha na kupata maendeleo binafsi na taasisi inahitajika kuwa na akili ya pamoja. 

Matunda ya akili ya pamoja ndiyo yamefanikisha kutengeneza program za akili za bandia. Tatizo ni kwamba akili inawezesha kukamilisha mipango, lakini ikiwa  imepangiliwa vibaya inaweza kuleta matatizo makubwa kwa jamii na mtu binafsi. Kwahiyo inahijitika mifumo ya akili ambayo inaweza kuzingatia maadili. 

Athari ya akili bandia (Artificial Intelligent) inadhoofisha ubinadamu,hisia,falsafa,uhusiano,kujiamini na kushusha uwezo wa binadamu kiakili.

4. Mazao ya teknolojia

Unaitwa uzalishaji wa kisasa au kilimo cha kisasa. Yote ni sahihi. Kila mmoja anaweza kusema ni jambo zuri kwa maendeleo ya binadamu. Uchaguzi unaonesha kuwa licha ya mafanikio na mazuri yaliyomo kwenye mazao ya teknolojia lakini kilimo chake hakiendelezi ardhi. 

Tatizo linakuja pale mazao yanayozalishwa kwa teknolojia yanaongeza nguvu na uwezekano wa kushindwa kujilinda dhidi ya asili. Uzalishaji wa asili ni mzuri kwa maendeleo ya ardhi yenyewe pamoja na kilimo. 

Mazao ya kisasa yanaonekana kuwa rahisi,hayana gharama, lakini mfumo wa uzalishaji wake ni kama silaha ya maangamizi. Kwa sababu katika ulimwengu ambao mataifa yanashindana kutengeneza silaha na kushambulia kabla ya adui hajafanya hivyo, kutegemea mazao ya kisasa ni kutoa nafasi ya maangamizi kwa wanadamu. 

Silaha inaweza kuwa ndogo sana, mfano kutumia sumu kusambaza kuweka kwenye vituo vya uzalishaji wa mazao ya kisasa ikiwemo zile za kuua mfumo wa fahamu ni rahisi kuwaangamiza watu wengi. 

Ni rahisi sumu kuangukia kwenye mikono yamtu yeyote, mfano mzalishaji wa mazazo ya kisasa kisha akatumika kuangamiza watu anaowataka.