Home Makala KWA HALI HII UNGA HAUTASHUKA BEI….

KWA HALI HII UNGA HAUTASHUKA BEI….

1236
0
SHARE

Watu kila mahali wanalia kuwa unga umepanda bei mno. Tatizo hili halipo kwenye nchi yetu tu. Huko Kenya Bunge la nchi hiyo limeita kikao cha dharura mwanzoni mwa wiki hii kwa ajili ya kujadili ni namna gani ya kushusha bei ya bidhaa hii muhimu.

Cha kushangaza asilimia 20 tu ardhi ya Tanzania ndio ambayo inatumika kwa kilimo nchini. Eneo kubwa lenye rutuba zaidi ya asilimia 46 ya eneo lote la Afrika mashariki lipo Tanzania yaani eneo hilo linalimika karibu ainza tano za nafaka na kustawi vizuri.

Katika Ukanda huu Tanzania ndio yenye political stability kuliko nchi zote. Kwa maana hiyo hakuna sababu yoyote ile inayozuia watu wasishiriki katika shughuli za kiuchumi kikiwemo kilimo.

Tanzania ina hekta milioni 44 za ardhi ya kilimo, na 5% tu ndiyo inayolimwa. Asilimia zaidi ya 50 ya wakazi wa jumuiya ya Afrika mashariki inategemea chakula toka Tanzania.

Tuna mvua za kutosha kwa mwaka mzima, tumezungukwa na maji kila pembe ya nchi hii.  Kwa mujibu wa sensa ya mwaka 2012 vijana ni asilimia 35 ya watanzania wote. Asilima 44 watoto na asilimia 21 ni wazee ambao hawana uwezo wa kushiriki kwenye kilimo.

Lakini kwa Tanzania hii asilimia 35 ya vijana ipo busy instagram, facebook na kuendesha bodaboda huku hii asilimia 21 ya wazee wakiendelea kujikita kwenye kilimo cha mazoea.

Vijana hawa asilimia 90 hawajui nini maana ya kilimo na hawajaandaliwa kwa ajili ya kutumia fursa hii. Haishangazi mhitimu wa SUA degree ya kilimo kwenda kukabana koo na aliyehitimu darsa la saba kwenye kijiwe cha bodaboda huku wakigombea abiria.

Serikali iwaonyeshe kundi hili la vijana fursa hii. Badala ya Serikali kuzuia kuuza mahindi na sukari Kenya iwezeshe watu kuzalisha bidhaa hizi kwa wingi ili tupate faida ya fursa hii.

Mimi si msomi wa Uchumi ila naona kuna kitu tunakosea hapa kuzuia uuzaji wa bidhaa hizi nje badala ya kuweka mkazo kwenye uzalishaji.

Thadei Ole Mushi