Home Michezo Kimataifa Kwa mechi hizi, Chelsea watamkumbuka Sarri

Kwa mechi hizi, Chelsea watamkumbuka Sarri

1349
0
SHARE

HASSAN DAUDI NA MITANDAO

HATIMAYE picha limeisha Maurizio Sarri hatakuwa katika benchi la ufundi la Chelsea msimu ujao. Juventus wamemrejesha nyumbani, Italia, kwa mkataba wa miaka mitatu.

Hata hivyo, baada ya msimu wake mmoja pale Chelsea, kocha huyo anaondoka akiwa ameipa mataji mawili (Kombe la Ligi na Ligi ya Europa) na ameiacha ikiwa ndani ya ‘top four’, kwamba itacheza Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao.

Hata hivyo, hiyo si tu itakayowafanya mashabiki wa Chelsea wamkumbuke kocha huyo. Hebu cheki mechi hizi zitakazobaki kwenye kumbukumbu zao hata baada ya kutimka kwa mkufunzi huyo.

Chelsea v Tottenham

Ni mechi ambayo Chelsea walishuka dimbani wakiwa na maumivu ya kupoteza mchezo wa fainali ya Carabao Cup dhidi ya Manchester City, siku ambayo Sarri alitibuana na kipa wake, Kepa Arrizabalaga.

Hata hivyo, wakati wengi wakiamini Chelsea wangefungwa, Sarri aliiongoza kupata pointi tatu kwa ushindi wa mabao 2-0 katika mtanange huo uliokuwa wa Ligi Kuu England (EPL).

Dynamo Kiev V Chelsea

Huo ulikuwa ni mtanange wa hatua ya 16 bora ya Ligi ya Europa, ambapo Chelsea walishinda mabao 5-0, tena wakiwa ugenini.

Licha ya Chelsea kushinda mabao 3-0 wakiwa nyumbani, kule Misri walicheza soka la kiwango cha juu zaidi, shukranji pekee kwa ‘hat-trick’ ya Olivier Giroud na Callum Hudson-Odoi na Marcus Alonso, ambao nao kila mmoja alizitikisa nyavu.

Liverpool v Chelsea

Ilikuwa ni vita ya raundi ya tatu ya Kombe la Carabao na Chelesea walishinda mabao 2-1. Mechi hiyo iliyochezwa Anfield mwishoni mwa mwaka jana, ilikuwa ya kwanza kwa Liverpool kupoteza mechi.

Katika dakika ya 58, Daniel Sturridge aliitanguliza Chelsea walichomo kupitia kwa beki wake wa pembeni, Emerson, kabla ya Hazard kumaliza picha.

Chelsea v Man City

Kuelekea mchezo huo wa Ligi Kuu, ambao Chelsea walizimaliza dakika 90 wakiwa na ushindi wa mabao 2-0, Sari hakuwa akipewa nafasi ya kuondoka na pointi tatu.

Kiwango kizuri cha Chelsea siku hiyo kilionekana kuanzia katika eneo la ulinzi na kisha kuimaliza Man City kwa mtindo wa mashambulizi ya kushitukiza.

Siku hiyo, ni N’Golo Kante na David Luiz ndiyo waliofunga na kumfanya Pep Guardiola aondoke uwanjani akiwa ameinamisha kichwa chake kwa huzuni.

Chelsea v Arsenal

Ni mtanange wa fainali ya Ligi ya Europa, ambayo tofauti na ilivyokuwa ikichukuliwa, ilikuwa nyepesi kwa Chelsea na si Arsenal iliyokuwa ikipewa nafasi.

Imani ya wengi kuwa Blues wangefungwa mapema tu ilitokana na tukio la video iliyomuonesha kocha Sarri akiwa na hasira mazoezini.

Lakini pia, isisahaulike kwamba Gunners walikuwa wakitambia rekodi ya Unai Emery katika michuano hiyo kwani tayari alishatwaa mara tatu ubingwa akiwa na Sevilla.

Hata hivyo, hali ilikuwa tofauti katika Uwanja wa Wanda Metropolitano, mbele ya mashabiki 67,829 waliovijaza viti vya dimba hilo linalotumiwa na Atletico Madrid.

Ni kwa sababu hadi mwisho wa mchezo huo uliotarajiwa kuwa wa kukata na shoka, Arsenal walikuwa hoi kwa mabao mawili ya Eden Hazard na moja moja kutoka kwa Pedro na Olivier Giroud.

Matokeo hayo si tu yalikuwa mabaya kwa Arsenal kwa kuwa walilikosa taji kwa kichapo kizito namna hiyo, bali pia walipishana na tiketi ya kucheza Ligi ya Mabingwa Ulaya, michuano ‘pacha’ na ile ya Ligi ya Europa.