Home Latest News KWANINI DUNIA IMEPOTOSHWA KUHUSU KILICHOTOKEA LIBYA?

KWANINI DUNIA IMEPOTOSHWA KUHUSU KILICHOTOKEA LIBYA?

1914
0
SHARE

NA MPOKI BUYAH

MWANASHERIA Ayesha Muammar Gaddaf  ambaye amewahi  kufanya kazi na Sadam Hussein, kwa sasa anaishi kama malaika huko katika Taifa la kifalme Oman.

Ayesha na familia yake wamepewa hifadhi kwa sharti la kutojihusisha na musuala ya kisiasa au harakati za aina yoyote ile.

Mwanajeshi huyu na mtoto pendwa wa Muammar Gaddaf, alizaliwa mwaka 1976 akiwa mtoto wa tano wa Gaddafi, baada ya majeshi ya dunia kulizunguka Jiji la Tripol na kupoteza matumani ya kuishi katika Taifa walilozaliwa, hivyo Agosti 30, mwaka 2011 walivuka mpaka wakiwa na mama yao mzazi Safia Muammar Gaddafi, Hannibal Muammar Gaddafi na dada mtu Ayesha akiwa na ujauzito wa miezi tisa na kumwacha baba yao, Gaddafi na kaka yao Saif al Islam wakipambana na yale ambayo vyombo vya Magharibi kama CNN na BBC  waliyaita majeshi ya dunia.

Kuwashinda Nato na wale walioitwa waasi lilikuwa jambo la ndoto ndio maana Ayesha nã Mama yake Safia walivuka mpaka kuelekea Algeria, kipindi  hicho Ayesha ambaye alikuwa mjamzito na machungu ya kumpoteza mume wake, watoto wake wawili, kaka zake wanne.

Serikali ya Algeria ilithibitisha kwamba, familia ya Gaddafi ilikuwa imewasili nchini humo. Ayesha alipofika Algeria siku moja baadaye alijifungua mtoto wa kike, familia hiyo ilivuka mpaka wakiwa na magari ya kifahari pamoja na ulinzi wa kutosha. Ulikuwa ni msafara uliokuwa na magari zaidi ya 15, familia hiyo ya Gaddafi ni moja kati ya familia tajiri kulingana na Taasisi ya World Human Records.

Wakati wala unga, majambazi wezi wakubwa wa malighafi za Afrika  watoto  wa mtaani, Al qaeda na Nato pamoja na makundi ya kigaidi ambayo yalitengenezwa na Marekani na  mataifa ya Kiarabu yalipovamia Libya, pasipokuwa na sababu zozote zile zaidi ya kuyasaka mafuta ya Libya.

Ni vyema ukaujua ukweli juu ya kile kilichotokea Libya, waandishi wengi na wachambuzi wengi wamekuwa wakishindwa kuongea ukweli wa kile kilichotokea Libya, Áfrika na dunia  imedanganywa juu ya kile kilichotokea Libya na Iraq.

Ni dhahiri kuwa historiaa ya Áfrika inapaswa kuandikwa na Waafrika wenyewe ila cha kushangaza tumekuwa watumwa wa Wazungu watuambie juu ya Afrika bila kujua agenda yao ni nini juu ya yetu.

Ayesha Gaddafi mtoto mpendwa  na aliyekuwa  mshauri mkubwa wa Serikali ya Tripol aliwahi pia kusimamia kesi ya Saddam Hussein, akiwa anaandamwa na Marekani na washirika wake, Ayesha kuanzia July 24, 2009 aliwahi kuteuliwa na UN kama balozi wa HIV/AIDS.

Pia amewahi kuteuliwa na Jumuiya ya Umoja wa bara la Ulaya kama balozi wa kutetea haki za wanawake Libya na dunia kwa ujumla wake. Ayesha alikuwepo katika jopo la wanasheria waliokuwa wakijaribu kumnasua Sadam Hussein kutoka kwenye mtego wa panya uliotegwa na Marekani na washirika wake. Ayesha Gaddafi pia akiwa katika ubora wake amewahi kufanya kazi na Umoja wa Kimataifa (UN) kama balozi wa Goodwill  kwa muda wa miaka mitatu mpaka pale alipovuliwa ubalozi huo baada kukutwa na hatia ya kushiriki katika vuguvugu la mabadiliko kwa kuhamasisha mauaji ya raia wasio na hatia mwaka 2011.

Wazungu wana msemo unaosema ‘hakuna adui wa kudumu na hakuna rafiki wa kudumu bali wana masilahi ya kudumu’, Ayesha alikuwa rafiki yao mkubwa lakini walikuja wakawaua watoto wake, baba yake na kaka zake wengi na kumuwekea vikwazo vya kiuchumi. Hapa ndipo unapokuja kugundua kwamba maisha hayana mwenyewe na hakuna anayepanga kesho maana mwenye mamlaka ya kuamua kesho ni Mungu pekee yake.

Ayesha Gaddafi ambaye anatafutwa na umoja wa kimataifa kwa kuhusika na mauaji yaliyotokea Libya, lakini zote hizo ni figusifigusi za Marekani na washirika wake katika kupotosha ukweli kwamba Gaddafi na familia yake walikuwa ni mashetani na wakandamizaji na waminyaji wa uhuru wa kujieleza kwa wananchi wake wakati UN RECORDS za mwaka 2009 hadi 2011, wananchi wa Libya walikuwa wanaishi kwa furaha kuliko Uingereza, Ufaransa, Marekani na Urusi, shutuma na vimbwanga vimetengenezwa na mashirika ya kimagharibi na mataifa machache ya Kiarabu ambayo yanatumika kama kibaraka wa Marekani katika kuivuruga amani ya dunia uko Mashariki ya Kati.

Baada ya Alu-Qaida, NATO  na Magembe ya wahuni au wauza madawa kutoka pamoja na baadhi ya wanajeshi kutoka Ufaransa na mashambulizi ya anga ambayo yalifanywa na wakina Clinton na ndugu yake Obama mwanzoni kabisa mwa March 2011, yalipelekea mvurugiko mkubwa na kusambaratika kwa Taifa hilo lenye utajiri mkubwa wa mafuta, baada ya miezi 5 ya vita watu wengi walikufa na miundombinu kuchafuliwa vibaya mno, ilipofika Agosti 2011, familia ya Muammar Gaddafi kuanzia mke wa colonel Mammary Gaddafi kwa Jina la Sofia (Safia), mtoto wake mkubwa wa kike, Aisha Gaddafi na watoto wake wawili walikuwa tayari mpakani mwa Algeria wakisubiri ruhusa ya kuingia katika nchi hiyo walikaa mpakani kwa mda wa masaa 12 ndipo waliporuhusiwa kuingia Algeria na kupata hifadhi kwa mda. Familia hiyo ilikuwa imeongozana na magari ya kifahari yasiyopungua 10 na baadhi ya mizigo mingine huku wakimwacha Muammar Gaddafi akiendelea na mapambano dhidi ya matapeli wa kimagharibi.

Utofauti mkubwa kati ya Wazungu na Waafrika, ni kwamba Wazungu wao wanasoma ili kupata na kuongeza maarifa  yapate kuwasaidia maishani mwao, lakini Waafrika wenye akili chachu na mgando wanasoma ili kupata vyeti na kazi nzuri na ndio maana miaka 50 imepita tangu Wazungu waondoke hakuna kilichobadilika Afrika zaidi ya miti pekee ndio imebadilika, lakini nyani na ngedere ni wale wale. Waafrika mafanikio makubwa wanayoyataka kuwa na mke mzuri na gari zuri wakidhani hayo ndio mafanikio, kuwa na mshikaji mzuri mpiga chuma ndio mafanikio unayoyataka, sasa kwa upumbavuu huu unaofikiria kwanini BBC, CNN, FORK NEWZ, ALJEZEERA, NBC  wasikupangie cha kufanya, kwa ujumla wake maisha ni mchakato mrefu sana, Wazungu wanatushangaa sana kutokana na akili zetu finyu, hapa naenda mbali na kukumbuka usemi wa Patric Otione Lumumba, kwamba mafanikio ni mchakato wa kufeli kutoka hatua moja kwenda hatua nyingine, katika maisha usipofeli basi hujafanikiwa bado, lakini pia tambua kwamba katika maisha yako si lazima uyafikie malengo yako na malengo mengine hutayapata au kuyafikia na ukifosi sana utaumia.

Sisi Waafrika tukishapata uhakika wa kula na kushiba pamoja na kuvaa vizuri bila kusahau kuwa na mke mzuri, basi tunaona tumemaliza kila kitu. Kwanini Wazungu wasituchagulie mfumo wa maisha tunayotakiwa kuishi, ndio maana Trump Fred rais wa 45 wa Marekani aliwahi kusema Waafrika wanawaza ngono tu na si vinginevyo. Trump aliendelea kwa kusema Afrika ndio watu wavivu duniani na wanaongoza kwa wizi, ni maneno machungu na hakuna mtu aliyekanusha maana ni ukweli mtupu, tumeyapa kipaumbele mambo ya kijinga na hapo ndipo CNN na BBC  wanatuaminisha kwamba GADDAFI alikuwa dikteta na tunakubali, kwa kuwa sisi ni vilaza wa kudadavua mambo tumeaminishwa kwamba Robert Gabriel Mugabe ni dikteta na tumekubali pia. Ukienda mbali zaidi walituaminisha kwamba Saddam Hussein alikuwa anamiliki silaha angamizi na wakamnyonga Decemba 31 kwa kuwa wao ni wakubwa wanatupangia nini chá kutuambia.

Utapata wapi muda wa kufanya uchunguzi na kuutambua ukweli, ni kweli Gaddaf alikuwa mtu mbaya. Viongozi wa Afrika waliambiwa wasimuunge mkono Gaddafi wala kumsaidia maana ni mtu hatari, kama Gaddafi ni mtu hatari mbona alikuwa anachangia mfuko wa Umoja wa Afrika (AU) kwa asilimia 50 peke yake, Gaddafi alikuwa hatari, mtu ambaye wananchi wake walikuwa wanaishi vizuri kuliko wananchi wa Uingereza na Urusi pamoja na Marekani, mtu ambaye alishindwa kumjengea nyumba baba yake mpaka alipohakikisha watu wa Libya wana makazi salama kwa asilimia 80.

Baba yake Gaddafi anakufa katika nyumba ya nyasi japokuwa Gaddafi alimwahidi baba yake atamjengea nyumba, lakini ngoja awajengee Walibya. Tunapotoshwa na Wazungu, ndio tunaambiwa taarifa za uongo juu ya Afrika na tunakubali, tumeambiwa Jonas Savimbi alikuwa kibaraka tumekubali, tunaambiwa Gaddafi alikuwa dikteta tumekubali, tumeambiwa Osama alikuwa gaidi tumekubali, tumeambiwa Nkuruma alikuwa na uroho wa madaraka tumekubali, huu ujinga tunatakiwa tufike mahali tuupinge na kukataa. Tuliambiwa Sadaam Hussein alikuwa anatengeneza silaha angamizi tukakubali.

Tuliambiwa Muamar Gaddafi aliwamiminia risasi waandamanaji, hivi Tanga lini waandamanaji wanabeba silaha.Hivi tangu waandamanaji wanavamia na kuuawa vituo vya polisi , vyombo vya kimataifa ambavyo tunaviamini na kuvisikiliza majumbani mwetu kama CNN, BBC ambao ndio maagenti wakubwa wa mataifa ya magharibi, hawa ndio wanaharibu na kuaribuu amani ya Afrika, hawa walidai kwamba waandamanaji walipigwa risasi wakati wale walikuwa kikundi cha wala madawa ya kulevya, majambazi, Al Qaida ambao wengi  walitoka nje ya Libya.

Huu upotoshaji ulikuwa mkubwa kiwango cha digrii, Gaddaf ameijenga nchi kwa umakini mkubwa kwa mda wa miaka 42 na kuwapa kila kitu lakini Gaddaf huyo huyo awamiminie risasi watu wake. Hawa walijiita waandamanaji walikuwa wamebeba silaha nzito na kuvamia kambi za kijeshi na kuua hakuna waandamanaji wa kipuuzi namna hiyo duniani kote.

Kikundi hicho cha wahalifu walitolewa mali, walitoka Mauritânia, Iraq na Saudia ambayo umoja wa mataifa ya kimagharibi walisema ni Walibya wakati hawakuwa Walibya. Waandamanaji gani wanaandamana na silaha za kivita mkononi, waandamanaji gani wanavamiaa ghala la silaha uko Tripoli na Benghazi. Tulivyoambiwa hivyo tuliamini kwanza wale walikuwa ni waandamaji wakati walikuwa vibaka na marambaia waliochukuliwa Mauritânia, Mali, Saudi na Iraq wengi walikuwa wamenunuliwa na kupewa pesa  nyingi kwenda kumuondoaa Gaddafi kwa kupewa msaada na mashetani Nato, Gaddafi alikuwa ni kiongozi ambaye aliwaelewa vizuri Wazungu. Wazungu hawajawahi kumpenda mtu mweusi na kosa kubwa ambalo alilifanya Obama, Clinton na Nicolas Sacozy  ni kumua Gaddafi na dunia ingekuwa ina usawa, basi wangetakiwa wapandishwe kizimbani kwa mauaji ya Muammar Gaddafi.

Mwaka 1951 Taifa liliitwa Libya linalopatikana Kaskazini mwa Bara la Afrika, lilikuwa ni moja kati ya Taifa masikini duniani. Lilikuwa taifa masikini kuliko hata Sudan Kusini ya sasa, kikwazo kikubwa cha umasikini wao kilikuwa ni ukame.

Ikumbukwe kwamba asilimia 64 ya Taifa hilo limezungukwa na Jangwa la Sahel, lakini baada ya kuingia Muammar Gaddafi kwa kufanya mapinduzi pasipo kumwaga damu mwaka 1969, mambo yalibadilika sana. Wazungu hawapendi kuona Afrika tunayafikia malengo yetu. Wazungu hawajawahi kutupenda kabisa, wanafurahi wanaposikia tunauwana kisa madaraka. Wazungu walifurahia kilichoendelea Libya, walifurahia kilichoendelea Tunísia na Misri,

Waafrika wametugawa na kitu kinaitwa demokrasia, walituambiaa tuunde vyamaa vingi. Leo tumeunda ila ukifika uchaguzi lazima tuchapane risasi, kwanini ukifika uchaguzi unakuwa uwanja wa vita, tunashindwa kushindana kwa hoja tunashindana kwa kuchapana risasi.

0762155025, mpokibuya@gmail.com