Home Habari LUGOLA AONGOZA KWA MAAGIZO

LUGOLA AONGOZA KWA MAAGIZO

4447
0
SHARE

NA JOHANES RESPICHIUS


WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola amekuwa waziri namba moja kutoa kauli na maagizo mengi ndani ya kipindi kifupi tangu ateuliwe kushika wadhifa huo.

Lugola aliteuliwa Julai mosi mwaka huu na kuapishwa Julai 2, mwaka huu, Ikulu jijini Dar es Salaam akichukua nafasi ya Mwigulu Nchemba ambaye uteuzi wake ulitenguliwa na Rais Dk. John Magufuli kwa sababu mbalimbali.

Katika kipindi cha siku 21 hadi kufikia mwanzoni mwa wiki hii, Lugola ameshatoa maagizo zidi ya 13 huku jeshi la polisi likiongoza kwa kupokea maagizo mengi kutoka kwa waziri huyo.

Mara tu baada ya kuapishwa,  Julai 3 alifanya ziara mkoani Mbeya kwa lengo la  kufanya uchunguzi wa sababu za kukithiri kwa ajali za barabarani kwenye mkoa huo

AGIZO 1

Katika ziara hiyo Lugola aliagiza kuvunjwa kwa Balaza la Taifa la Usalama Barabarani pamoja na kamati zake zote nchi nzima.

Alisema kuwa aliamua kufanya hivyo kutokana na kushindwa kupambana na ajali.

AGIZO 2

Pia alimwagiza Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Simoni Sirro kufungia leseni za madereva ambao wameonywa zaidi ya mara tatu na kuwachukulia hatua za kinidhamu maofisa na askari wazembe wa mikoa 10 ya kipolisi inayoongoza kwa ajali za barabarani.

AGIZO 3

Julai 6, mwaka huu, Waziri huyo wakati akizungumza na vyombo vya habari pamoja na wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalana na idara zilizo chini ya wizara hiyo alimwagiza Katibu Mkuu wa Wizara hiyo kuwashusha vyeo, Mkuu wa Usalama Barabarani Mbeya, Mrakibu wa Polisi,  na Mkuu wa Kikosi cha Zimamoto na Uokoaji mkoani Kagera, Mrakibu Mwandamizi wa Polisi, George Mrutu ambaye alikuwa tayari ameshaenguliwa katika nafasi hiyo.

AGIZO 4

Katika mkutano huo pia aliwaagiza wakuu wa vyombo vya usalama chini ya wizara yake, kubeba Ilani ya Chama cha Mapinduzi (CCM) kwa kile alichodai kuwa wanafanyakazi ya chama kilichopo madarakani, hivyo ni lazima waitumie katika kuweka mipango kazi.

AGIZO 5

Julai 12 waziri huyo alitembelea Idara ya Uhamiaji na kuzungumza na watendaji wakuu wa idara hiyo huku akiagiza na kuwataka askari wa uhamiaji waliopo mipakani kujitafakari kwa maelezo kuwa utendaji wao hauridhishi.

AGIZO 6

Lugola alipofanya ziara ya kikazi katika makao makuu ya kikosi cha kutuliza ghasia Upanga Julai 19 mwaka huu, alimpa siku 14 IGP Sirro kumueleza mikakati ya kuwawezesha Watanzania kufanya kazi kwa saa 24.

Aidha, alimtaka IGP Sirro amwambie kama jeshi la polisi limeshindwa kupambana na majambazi hadi kufikia hatua ya shughuli nyingi kufungwa inapofika jioni kwa kuhofia kuvamiwa.

AGIZO 7

Katika ziara hiyo hiyo ya Ukonga, Lugola alimtaka IGP Sirro amweleze ni kwa nini mabasi hayatembei usiku. Je ni kwa sababu Jeshi la Polisi limenyoosha mikono kwa majambazi, alisema  majambazi hawawezi kuamua ni maeneo gani raia waende na yapi wasiende.

AGIZO 8

Aidha, Lugola baada ya kubaini kuwa mbwa maalum wa kikosi cha bandari hayupo mahala pake pa kazi alitoa agizo kwa IGP Sirro akimtaka  afuatilia alipo mbwa huyo na kumpa ripoti katika muda ambao ulikuwa hauzidi saa 10.

AGIZO 9

Julai 21, mwaka huu waziri huyo alipokutana na wanahabari aliagiza kulazwa mahabusu kwa dereva yeyote atakayesababisha ajali na kama ikibainika ajali hiyo ilisababishwa na ubovu wa gari basi hata mmiliki alale ndani kabla ya kupandishwa kizimbani.

Alisema ikitokea dereva yoyote akafikishwa Mahakamani kabla  ya kulazwa mahabusu, basi  huyo aliyefanya hivyo atashughulika nae.

AGIZOP 10

Lugola pia alimwagiza Mkurugenzi Mkuu wa Mamala ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA),  Dk. Andrew Massawe, afike Ofisini kwake, jijini Dodoma Julai 25, mwaka huu akiwa na watu waliopewa tenda ya kuleta mtambo wa kutengeneza vitambulisho vya Taifa na wamweleze kwa nini mtambo huo haujaletwa au waende na pesa walizopewa.

AGIZO 11

Waziri huyo wa Mambo ya Ndani mwishoni mwa wiki iliyopita aliliibua upya sakata la Lugumi kwa kumwagiza IGP Sirro kumtafuta mmiliki wa Kampuni ya Lugumi, Said Lugumi na kumfikisha ofisini kwake Julai 31 saa 2 asubuhi mwaka huu.

AGIZO 12

Lugola aliagiza jeshi la Magereza kuhakikisha wafungwa wanajilisha na kulisha mahabusu, na kwamba hataki kuona wafungwa nchini wanaishi kama ndege wa angani.

Alisema wafungwa hawalimi ila wanakula bure, badala yake wanatakiwa wafanye kazi na kujitafutia chakula wao wenyewe badala ya kusubiri kupewa chakula na Serikali.

Aliyesema hayo Julai 16 wakati akihojiwa katika kipindi cha Tuambie kilichorushwa na kituo cha televisheni cha TBC1 Jumatatu usiku, na kubainisha kuwa amewaagiza wasaidizi wake kupitia sheria vizuri na kumpelekea mpango mzuri wa utekelezaji wa agizo la Rais, la kuwatumia wafungwa kufanya kazi za kilimo na ufugaji na kujitafutia chakula wao wenyewe.

“Hata kama ni meno, lazima walimie meno, watatumia meno yao kulima mahindi, kulima maharage ili wajilishe, na nimemwambia Inspekta Jenerali wa Magereza, katika hili sitaki kisingizio cha aina yoyote”.

Lugola amesema kuwa amemueleza Inspekta Jenerali wa Magereza kutumia Shirika la Uzalishaji Mali, Benki ya Kilimo na TIB kuchukua mikopo katika kutekeleza agizo hilo la Rais.

Waziri Lugola amesema utoaji wa chakula bure gerezani umesababisha baadhi ya wafungwa kuona gerezani kama ndiyo sehemu ya kupumzika na kula bure bila kufanya kazi, na kusababisha baadhi yao kila wanapobakiza mwezi mmoja kumaliza vifungo au wakimaliza vifungo na kuachiwa huru, wamekuwa wakifanya makosa mengine kwa makusudi ili warudi tena gerezani.

“Wanajitafutia makosa na kuendelea kukaa bure na kula chakula bure bila kufanya kazi,”alisema.

AGOZO 13

Julai 23, mwaka huu, Waziri huyo aliagiza kuwekwa Mahabusu kwa Askari Polisi aliyekuwa katika kituo cha polisi cha utalii na Diplomasia baada ya kushindwa kuelezea vitabu muhimu vinavyotakiwa kuwa kwenye chumba cha mashitaka.

AGIZO 14

Lugola aliagiza kukamilika haraka kwa mchakato wa askari 10 wanaotakiwa kusoma lugha za kimataifa na masuala ya kidiplomasia ili wakafanye kazi kwenye kituo hicho

MAAGIZO/KAULI

Amemuagiza IGP apeleke mkakati wa uchumi wa viwanda, anashughulikia kubambikia kesi, amejiridhisha watanzania wasio na kesi wapo mahabusu ya vituo vya polisi

Ameagiza kuwekwa ndani kwa polisi waliomshikilia mama aliyekwenda kituoni kusema, mumewe anayedaiwa pesa sh. 5,000 hayupo.

Lugola aliagiza mama huyo aachiwe na polisi waliomweka ndani waingizwe wao.

Alipata kusema Polisi wasiposhughulikia majambazi watapata tabu sana, anaweka mkakati ili mabasi yaendeshwe na madereva wawili na wote  wapimwe kilevi kila wanapopita.

Amemwagiza IGP ampelekee majina na sifa za wakaguzi wa magari, ametaka mtu yeyote akipokea mgeni aende akatoe taarifa serikalini.

Ameweka wazi kuwa mtru akihusisha uhalifu na vyombo vya serikali atapata cha mtema kuni,

Alisema hajaridhishwa na mmoja wa wakuu wa Zima Moto huko Kagera, ambaye alihojiwa huku anazunguka tu na kiti

Ametaka kuonana na watu wa Baraza la Kiswahili (BAKITA) juu ya msemo “ajali haina kinga” kwani kinga ipo.