Home Latest News MA DC VIJANA FANYENI ZAIDI …

MA DC VIJANA FANYENI ZAIDI …

5957
0
SHARE

Na ABRAHAM GWANDU –ARUSHA                    |                     

HAKUNA jambo la ajabu sana ambalo limefanywa na Rais Dk John Magufuli katika kuwateua vijana kushika madaraka na kuongoza au kutumikia nafasi mbalimbali kama sehemu ya kumsaidia kazi ya kuwatumikia wananchi.

Ameshafanya hivyo katika teuzi nyingi alizofanya tangu alipoapishwa kuwa Rais mara baada ya kuchaguliwa katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2015. Hii inaonyesha imani kubwa aliyo nayo kwa vijana wa taifa hili.

Mara hii katika uteuzi wake , Rais amewateua tena vijana machachari kushika nafasi kadha zikiwemo za ukuu wa Wilaya , Mkoa, Makatibu tawala Mikoa na Wilaya na hata makatibu na manaibu makatibu Wakuu wa Wizara na taasisi nyinginezo.

Mara hii kati ya walioteuliwa na Rais , ukanda huu wa Kaskazini yamechomoza majina mawili ya vijana machachari ambao ni mwanahabari Jerry Muro na mwanasiasa kwa kuzaliwa kama mwenyewe anavyojiita ,Lengai ole Sabaya .

Nianze na ole Sabaya ambaye ni Mkuu mpya wa Wilaya ya Hai Mkoani Kilimanjaro , huyu historia yake ya kisiasa ,kikazi na kiharakati  ni ndefu kidogo. Kabla ya kuteuliwa alikuwa Diwani wa Kata ya Sambasha Jimbo la Arumeru Magharibi MKoa wa Arusha.

Pia aliwahi kuwa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) Mkoa wa Arusha na alijaribu kugombea nafasi hiyo kwa ngazi ya taifa lakini hakupenya kwenye chujio la vikao vya maamuzi kwa hivyo safari yake ikaishia njiani ,hakufanikiwa.

Sabaya Diwani Kata ya Sambasha na yule Sabaya Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Arusha wanajulikana vizuri hususani kwa wakazi wa Jiji la Arusha , Halmashauri Mbili za Meru na Mkoa mzima kwa ujumla wake. Alitambulika kwa aina ya maisha yake .

Mara chache hukutana na vijana wenzake katika yale maeneo fulani wakajadili masuala mbalimbali ya nchi ikiwemo siasa, uchumi, michezo nakadhalika huku akisindikiza mazungumzo kwa fundo la mvinyo maarufu wa ‘dompo’ .Huyu ndiye Sabaya mcheshi na mchangamfu.

Wengi wanasubiri kumshuhudia Sabaya Mkuu wa Wilaya ya Hai, na Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama ambaye majukumu yote ambayo angelifanya Rais ,yeye sasa atayafanya kwa ngazi hiyo ya Wilaya.

Sio kazi ya kubagua wananchi kwa misingi ya itikadi za kisiasa, dini wala ukabila. Sio kazi ya kwenda kufyeka shamba la Mbowe ,ni kazi ya kutumikia watanzania wanaoishi Wilaya ya Hai. Alikuwa akitumikia wananchi katika eneo dogo Kata ya Sambasha sasa amepanda cheo, Rais amemuongezea jukumu.

Alikuwa Mwenyekiti wa kikundi cha vijana wa CCM, sasa ni Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya ,eneo ambalo wanaishi watu wenye vyama na wasio navyo. Ni kweli yeye ni mwanachama wa CCM lakini jukumu alilopewa kwa mujibu wa katiba linakataa kuwabagua wananchi kwa misingi ya itikadi yake.

Wilaya ya Hai kwa upande wa magharibi inapakana na wilaya ya Arumeru, wananchi wanaoishi katika eneo hili wanafanana kwa kila kitu. Mila na desturi zao hazitofautiani sana .Wachaga wa Machame na Wameru ni wale wale .

Huku Arumeru Rais Magufuli kamteua Mwanahabari Jerry Muro kuwa DC . Kma sio busara na hikma ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo tungemshuhudia Muro msemaji wa klabu ya mpira wa miguu ya Dar Young African.

Ilikuwa baada ya kuapishwa kwake , katika hotuba yake ya kushukuru , ndipo  Muro alipoanza kwa makeke, akitaka kumaliza mara moja changamoto na migogoro isiyokwisha inayowakabili wananchi wa Arumeru . Ni kweli Arumeru inasifika kwa migogoro ya ardhi kwa miaka dahari tangu enzi za mkoloni kabla ya uhuru wa Tanganyika.

Kwenye mpira wakati akiwa msemaji wa Yanga ilikuwa rahisi kwake kuwaaminisha wapenzi wa timu hiyo kuwa kuifunga Simba ni kama kuchinja kuku unayemfuga mwenyewe haina haja kumlenga na manati , hata kama baada ya mchezo matokeo yakawa kinyume.

Kutokana na makeke hayo ndipo wanaojua (RC Gambo) wakamwambia kijana nenda pole pole. Uongozi unatofautiana kutoka eneo moja hadi jingine. Ni tofauti na kushika kalamu au kamera ili kunasa tukio la kihabari kama ambavyo alikuwa akifanya.

Imani huzaa imani, kama ambavyo Rais alivyowamini ninyi , kazi yenu vijana mlioaminiwa rudisheni imani kwake kupitia utumishi uliotukuka. Wananchi katika maeneo yenu hususani vijijini wana matatizo makubwa yanayohitaji ubunifu kuyatatua.

Wengi wenu ni vijana mliosoma vizuri, elimu yenu haitakuwa na maana iwapo haitasaidia kupunguza matatizo ya mnaowaongoza. Kazi ya DC sio kutisha watu kwa kuwasweka mahabusu saa 24 kwa kutumia ile sheria ya mkoloni inayoitwa amri ya DC.

Kazi yenu kuonyesha njia , kubuni mikakati, kusimamia utawala bora kwa kuzingatia sheria nzuri sio mbovu. Wakulima bado hawajaona tija katika kilimo, wafugaji wanaendelea kufuga kwa mazoeya. Wafanyabiashara wanaendelea kunyanyaswa katika nchi yao kama wako utumwani vile. Hakuna masihi wa kuja kuwakomboa , ni ninyi.

Mkiyatekeleza hayo , wala hamtotumia nguvu kubwa ya vyombo vya dola kumaliza vyama vya upinzani katika maeneo yenu, vitajifia vyenyewe kwa kukosa sera , ajenda ya kuwaambia wananchi maadamu ninyi kwa niaba ya serikali mnatekeleza wajibu wenu wa kuwaletea maendeleo.Na ABRAHAM GWANDU –ARUSHA.

Mkiyatekeleza hayo , wala hamtotumia nguvu kubwa ya vyombo vya dola kumaliza vyama vya upinzani katika maeneo yenu, vitajifia vyenyewe kwa kukosa sera , ajenda ya kuwaambia wananchi maadamu ninyi kwa niaba ya serikali mnatekeleza wajibu wenu wa kuwaletea maendeleo.