Home Uchambuzi Afrika Maadhimisho ya mapinduzi Algeria chachu ya ukombozi Sahara Magharibi

Maadhimisho ya mapinduzi Algeria chachu ya ukombozi Sahara Magharibi

2969
0
SHARE

Baadhi ya wanaharakati wa Sahara Magharibi

NA NOEL SHAO

Algeria wanaadhimisha mwezi wa Baraka, ikiwa ni sherehe ya miaka 64 ya mapinduzi ‘’Glorius revolution’’. Mwezi huu huitwa mwezi wa Baraka kwa sababu Novemba mosi, 1654, ni siku Algeria ilipo fanya mapinduzi na kuhitimisha miaka mingi ya mteso ya ukoloni  kutoka kwa Ufaransa, mapinduzi  yaliongozwa na chama  cha ‘National Liberation Front (FLN)”

Kwa hakika, wanamapinduzi wa Algeria walifanikiwa licha ya  changamoto nyingi walizo kumbana nazo, bila shaka walifanikiwa katika kuitengeneza historia ya Algeria ya leo. Sherehe za mapinduzi ya Algeria hurudisha kumbukumbu ya miaka 64 nyuma ya wapiganaji walio jitoa kuingia msituni kwa ajili ya ukombozi wa taifa lao.

Maadhimisho ya Novemba ni matokeo ya historia ndefu ya taifa la Algeria na wazalendo waliojitoa kuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha mapinduzi ya Algeria yanafanikiwa. Kama ilivyo desturi ya mataifa mengine, Algeria inawaenzi na kuwakumbuka wanapigania uhuru wake kama Emir Abdelkader, El-Mokrani, na Ibn Badis na wengineo, wanaobaki kama alama ya ujasiri kwa juhudi zao za kuongoza mapinduzi hayo.

Mapinduzi na ushindi wa Algeria ulichagizwa pia na kuwahamasisha watu si kupingana na wakoloni tu bali na maadui wengine wa ndani na nje. Hivyo hamasa ya Novemba mosi kwao ni jambo la kudumishwa na kuenziwa kwa gharama kubwa kwa kuwa yaligharimu vifo vya watu wengi, mateso na uharibifu mwingi.

Mapinduzi ya Algeria hayakulenga kujipatia uhuru wa bendera tu bali kuijenga jamii iliyo na usawa na uwajibikaji kwa manufaa ya taifa lao.

Aidha, hata baada ya mapinduzi, Algeria iliendelea kuunga mkono juhudi mbalimbali za nchi jingi katika kujikomboa na madhila kadhaa hususani ya ukoloni. Wao wanaamini katika kujitawala, haki na uhuru ndio maana wanaunga mkono juhudi za ukombozi ndani na nje ya Afrika.

Kwa kuzingatia misingi ya kujitawala Algeria wanaamini jumuiya ya kimataifa haiwezi kukaa kimya wakati taifa la Sahara Magharibi na Palestina wanahitaji haki, amani na uhuru wao.

Kilinachoisukuma Algeria ni kile kile kilicho isukuma Tanzania kuwa kitovu cha mapambano Afrika. Mara baada ya uhuru 1961, Tanzania iliendeleza vuguvugu la ukombozi katika nchi mbalimbali barani Afrika na nje ya Afrika.

Waasisi wa mapambano ya Afrika wakiongozwa na, Mwalimu Julius Nyerere, Kwame Nkruamah, Nelson Mandela, Samora Machel, Edward Mondalane,  Jomo Kenyeta na wengineo, waliamini Afrika huru ni ile Afrika ambayo nchi zote za Afrika ziko huru.

Walianzisha kauli ya, Afrika moja, Afrika huru, ili kuchagiza mapambano endelevu ili hata kama nchi fulani imesha pata huru wake badala ya kujikita katika kutazama mambo yake ya ndani, wajielekeze kwenye uhuru wa nchi nyingine pia.

Afrika kabla ya ujio wa wakoloni lilikuwa ni bara moja kiasili, lililokuwa na utamaduni wake, hivyo dhana hii ilizidi kuchagiza mapambano dhidi ya ukoloni.

Baada ya mapambano hayo ya miaka kadhaa, limebaki taifa moja ambalo halijapata uhuru wake Afrika, taifa la Sahara Magharibi ambalo watu wake wapo kwenye mateso ya ukoloni kutoka kwa Moroko kuanzia mwaka 1975.  Bahati mbaya mfumo wetu wa elimu umeshindwa litambua taifa hili la mwisho ambalo halija pata uhuru wake hivyo kupelekea historia kutoandikwa na kutunzwa vizuri.

Wakazi wengi wa Sahara magharibi walio kimbia mateso ya ukoloni wamehifadhiwa katika makambi mbalimbli nchini Algeria.

Ni jukumu la viongozi wa Afrika kuasisi na kuendeleza mapambano dhidi ya ukoloni ili kuhakikisha wanasaharawi wana jitawala. Licha ya juhudi nyingi zilizo fanyika za ndani na za kimataifa, umoja na mshikamano ndio utaikomboa Sahara kutoka kwenye mikono dhalimu ya Moroko.

Tukishindwa kufanya hili, tutakuwa tumesaliti juhudi za waasisi wetu ambalo walipenda kuona tunashikamana kwa umoja, kwa pamoja na kudumisha udugu wetu katika kutetea wanyonge popote walipo.

Ni wajibu wa viongozi wenye nia ya dhati ya kukemea uovu, wanamapinduzi, na waharakati wote ni wakati wa kupaza sauti kuona mataifa hayo ambayo hayako huru yanajipatia uhuru wake, tukishindwa kufanya hivyo kama kizazi cha leo, waasisi wetu hawata tusamehe kadhalika vizazi vijavyo vitashindwa kutusamehe.