Home Habari MAALIM SEIF: MAENDELEO SI BABARABA PEKEE

MAALIM SEIF: MAENDELEO SI BABARABA PEKEE

4517
0
SHARE

NA MWANDISHI WETU

KATIBU Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Maalim Seif Sharif Hamad, amesema ili wananchi wanufaike na maendeleo ya Taifa lililo huru, lazima maendeleo hayo yamguse mwananchi mmoja mmoja.

Pia alisema licha ya malengo ya mapinduzi ya Zanzibar yaliyoongozwa na Sheikh Abeid Amani Karume kulenga kuwaletea maendeleo wananchi wa Zanzibar, hadi sasa maendeleo hayo hayajawafikia wananchi kama ilivyokusudiwa.

Maalim Seif alitoa kauli hiyo juzi katika moja ya mikutano yake kwenye ziara anazoendelea kuzifanya kisiwani Unguja.

“Mzee Karume alisema wazi wazi kwamba tunapindua tunataka tujitawale wenyewe, kwa hiyo mkoloni akaondoshwa, haya niambieni wananchi wenzangu leo Zanzibar tuna maendeleo ya kujivunia? Zanzibar imebadilika kwa kiasi gani?

“Huwezi kusema mimi nimejenga barabara mtu anakula barabara?… maendeleo ni yale yanayomgusa mtu moja kwa  moja, maisha yake yabadilike yawe mazuri siyo yawe mabaya zaidi. Sasa hapa tunashuhudia kwamba kila mwaka mambo yanakuwa mabaya zaidi kuliko miaka iliyopita.

“Zanzibar Unguja na Pemba ilikuwa ni aibu kwa mtu kukaa barabarani akaomba, kweli au uongo? Leo njoo Unguja au siku ya Ijumaa nenda Misiktini uone kina mama wamekaa miskitini mikono hivi,” alisema Maalim Seif.