Home KIMATAIFA Maiti yazini na mfanyakazi wa Mochwari

Maiti yazini na mfanyakazi wa Mochwari

3694
0
SHARE

HASSAN DAUDI NA MITANDAO

DUNIA haiishi mambo, kila uchwao yanaibuka mambo mapya na mazito yanayofurahisha na wakati mwingine kuhudhunisha.

Yapo mataifa hayaishi mambo kutokana na ukubwa wake ama kwa sababu ya kukua kwa teknolojia yake.

Ukuaji wake huo husababisha wananchi wake kufanya vituko vingi kupitiliza. Hufanya hivyo kwa nia ya kutaka kuona matokeo ya hicho wanachokifanya.

Mataifa yaliyoendelea hasa Marekani huongoza kwa vibweka na vimbwanga hivyo vinavyoishangaza dunia.

Moja ya vimbwanga hivyo ni hiki kilichofanywa mwaka 2012 na mwanamama Felicity Marmaduke raia wa Marekani.

Mwanamama huyo anayefanya kazi kwenye chumba cha kuhifadhia maiti maarufu kama mochwari alijikuta akiingia matatani baada ya kupata uja uzito kwa kujamiiana na mtu aliyekufa kwa maana ya maiti. 

Mtandao wa habari wa dead serious news umesema tukio hilo linadhaniwa kutokea katika chumba cha kuhifadhia maiti cha Mourning Glory, nje ya Lexington, Missouri. 

Polisi wa mjini humo wamemshtaki Felicity Marmaduke kwa kosa la kunajisi na kuchezea maiti. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na polisi, kiungo cha kiume cha mwili wa mtu aliyekufa kilihamasika wakati mwili ukioshwa. Taarifa zinasema, kwa kuwa mwanamama huyo alikuwa peke yake, aliamua kujamiiana na mwili huo.

Kwa mshangao hata wa mwanamama huyo, maiti huyo alitoa mbegu za kiume. Wiki chache baadaye Marmaduke alijikuta ni mja mzito. Baada ya kumwambia daktari wake mfululizo wa matukio, daktari huyo aliwataarifu polisi. 

Marmaduke alikamatwa na polisi akiwa nyumabni kwake, si mbali sana na mochuari anayofanyia kazi. Katika tukio la kushangaza zaidi, mwanamama huyo amesema anapanga kudai urithi kutoka kwa familia ya mtu huyo aliyekufa.

Kwa kuwa raia wa Marekani wametawaliwa na vituko, kidume John Wojtowicz  ambaye amekaa kimahamahaba, aliamua kwenda kuiba benki ili alimpie mpenzi wake afanyiwe upasuaji wa kubadili jinsi yake.

Kushindwa kwa jaribio hilo la wizi kulisababisha filamu ya The Dog Day Afternoon kutengenezwa na makala nyingine kibao zikafuatia,na filamu ya hivi karibuni ,The Dog, si ya kimahaba ,lakini yenye kugusa hisia za watu na haina ufiche na yenye kuelezea hali halisi ya mwenyeji wa jiji la New York .

Katika hali ya kawaida hakuna mtu ambaye anaweza kuthubutu kwenda kuiba ama kupora benki ili kufanikisha upasuaji wa kurekebisha maumbile ya mwandani wake ,na ndio sababu iliyolazimu filamu hiyo kutengenezwa anaeleza Wojtowicz ,kwamba katika filamu hiyo The Dog – inamuelezea mwanamume mmoja aliyeamua kujitumbukiza katika kesi mbaya ya wizi katika benki ,tukio ambalo Marekani haijawahi kushuhudia.

Mnamo tarehe ishirini na mbili mwezi August mwaka 1972, John Wojtowicz na wenziwe wawili , Salvatore Naturale na Bobby Westenberg walielekea katika tawi la benki mjini Brooklyn baada ya kushindwa katika jaribio la wizi pia na kutimuliwa kwenye benki nyingine ya Manhattan, wakiwa wamebeba bunduki aina ya shotguns lakini hawakufanikiwa, walishindwa vibaya.

Westenberg hakufanikiwa kupora kiasi kikubwa cha pesa akaamua kutoka, mfanyakazi mmoja wa benki akagundua nusu ya pesa haimo katika kasha la kuhifadhia pesa,mwingine akapiga kengele ya hatari .

Mara eneo lote likazingirwa,wafanyakazi nane wa benki wakageuka kuwa mateka katika kujaribu kujinusuru Polisi nao wakaanza kujadiliana nao ili wawaachilie wafanyakazi hao nao wajisalimishe.

Nje ya jengo watu wapatao mia mbili walikusanyika kushuhudia tukio hilo lililokuwa kama filamu hivi ,tukio lililo husisha FBI , kitengo cha dharura,walenga shabaha mahiri wakiwa juu ya mapaa ya majengo, na wapiga picha za televisheni nao hawakukosa.

Wojtowicz aliicheza nafasi yake kwa umahiri mkubwa, akiwa na madai kadhaa kwa mateka moja wapo likiwa ni chakula kwa mateka ,na akamlipa mleta pizza kiasi kikubwa cha pesa . Akapata mpango, akawarushia mashuhuda wa seke seke hilo ,kwa hilo yeyote angempenda tu.

Saa mbili za majadiliano yao,Wojtowicz akaongeza kiasi cha madai yake kwamba anataka mkewe aliyeko hospitali ya kata ya King’s aletwe eneo la tukio. Jina lake ni Ernest Aron. Ni shoga. Nami ni shoga . Hivyo mimi na mke wangu wote ni mashoga