Home Makala Kimataifa Marekani itaendelea kuwa mteja wa Urusi

Marekani itaendelea kuwa mteja wa Urusi

2587
0
SHARE

Jengo la Bunge la MarekaniNa Yona Maro

MWAKA 2014, Bunge la Marekani lilipitisha sheria ya kuacha kutegemea injini za Urusi kwa ajili ya safari za anga za juu kuanzia mwaka 2019 kutokana na mgogoro wa Ukraine.

Hata hivyo, Desemba 2015, katazo hilo lilifutwa Aprili mwaka huu, jeshi la Marekani lililiambia Bunge kwamba katazo hilo litasababisha hasara ya dola za Marekani bilioni 1. Naomba nijadili kidogo ni kwanini Marekani haiwezi kuacha kutegemea injini za kiresi kwa sasa na hata miaka mengine 5.

Kabla ya kuendelea ni vizuri tukajua kwamba vyombo vya Marekani na baadhi ya ndege kubwa za kijeshi za Marekani na mataifa mengi hutumia injini za Urusi kwa ajili ya roketi na safari nyingine za anga za juu, injini hizi ndiyo bora na nafuu kidunia kwa sasa na hakuna mbadala .

Injini zinazoongelewa hapa ni aina ya RD-180, mpaka sasa Marekani haina mbadala wake wala hakuna nchi duniani inayobuni na kuzalisha kwa kiwango kinachotakiwa kama urusi. ubunifu wa kitu hiki unatakiwa miaka mingi ya utafiti, kubuni, kutengeneza, kufanya majaribio hatimaye kuanza kufanya kazi kitu ambacho Marekani haiwezi kwa sasa .

Labda inayoweza kutumika inaitwa Delta, hii ni ndogolakini , gharama za kuiendesha ni kubwa na itahitaji mipango mingi .

Pili kama Marekani ikiamua kuachana na RD-180, gharama za kusafirisha setelaiti katika anga za juu zitaongezeka maradufu kitu ambacho kinaweza kuleta mgogoro kati ya serikali na walipa kodi. Hivi sasa injini ya RD-180 inatumika kurusha roketi aina ya Atlas ambayo ndiyo moyo wa safari za anga za juu kwa Marekani. Mbadala wa kurusha setelaiti kubwa huko angani ni Delta ambayo gharama yake ni mara 5 zaidi ya ile ya RD-180 kwa mruko mmoja ili iweze kuendana na viwango vya Jeshi la Marekani.

Roketi aina ya SpaceX ambazo zimekua zinasifiwa kwa siku za karibuni huko Marekani hazijafikia viwango vinavyotakiwa na Jeshi la Marekani kwa ajili ya matumizi wanayoyataka wao. ina maana asilimia 40 ya roketi zitakazorushwa na Marekani kwa kutumia DELTA zitatumia mabilioni ya dola na gharama kubwa.

Kuachana na roketi za kirusi aina ya RD-180 ni kama kujikata ngwala kwa sababu kama DELTA zikileta shida ina maana Marekani haitakua na mbadala tena, safari za anga za juu zitasimama, utafiti unaweza kusimama na shuguli za kijeshi na kijasusi zinazofanywa na Marekani zinaweza kwenda mrama, hata biashara za mawasiliano, hali ya hewa, matangazo ya Tv na redio, intaneti na mengine mengi.

Mwisho ni kujua kwamba kama Marekani ikiachana na roketi za kirusi mapema zaidi kabla ya kujiandaa itaweza kuingia hasara nyingi za kiuchumi na kijamii, pia itaweza kuvujisha siri za kijeshi na mengine wanayofanya katika anga za juu si kwa Urusi tu hata kwa mataifa mengine .

Ingawa Marekani inahitaji kuachana na injini za kirusi kwa maslahi ya muda mrefu lakini kuachana nazo ni vigumu kwani inahitaji maandalizi na mambo mengine mengi ya muda mrefu ili kuzuia taifa kuingia katika migogoro maana hasara yake ni kuanzia dola bilioni 1.

Kwa ufupi, Marekani inahitaji kutumia roketi za Urusi kuweka setelaiti zake anga za juu kwa miaka mengine 5 au 10 kabla ya yenyewe kuwa na uwezo wa kujenga zake lakini hata ikifika huko huwezi kufahamu Urusi, India, China au jumuiya ya Ulaya na mataifa mengine yatakuwa katika hatua gani katika teknolojia hizo za anga za juu. wanaweza kuwa mbali zaidi na isiwe chochote wala lolote .

Sijui umejifunza nini kupitia makala haya, kama umejifunza jambo lolote unaweza kuchangia mawazo yako ili Watanzania wenzetu nao waelimike.

0786 806028