Home Burudani Marioo : Sihitaji mahusiano kwa sasa

Marioo : Sihitaji mahusiano kwa sasa

2597
0
SHARE

Na Jeremnia Ernest

MiongonI  mwa chipukizi wa muziki  wa  Bongo Fleva wanaofanya vizuri kwa sasa ni Omar Mwanga maarufu Mario.

Mario kwa sasa anapasua anga la muziki huo hapa nchini kupitia singo yake ya Chibonge ambayo imewakamata watu wengi.

Historia yake kimuziki     

Mario alizaliwa mwaka 1995 jijini Dar es Salaam. Anasema, akiwa bado mtoto mdogo, wazazi wake walimpeleka kuishi kwa bibi yake, Rufiji mkoani Pwani.

Anasema safari yake rasmi kimuziki ilianza rasmi, baada ya kushindwa kuendelea na elimu ya sekondari kutokana na changamoto za kifamilia.

Anasema baada ya kumaliza elimu ya msingi na kushindwa kuendelea na elimu ya sekondari alilazimika kufanya kazi ya katika mgahawa(Mama ntilie).

Asema akiwa anafanya kama ya mama ntilile ndipo alipoamua pia kujihusisha na na muziki.

Mario limetoka wapi?

Anasema jina Mario limetokana na ongezeko la herufi mbele na nyumba katika jina lake halisi ya Omar.

Anasema jina hilo alipewa na wazazi wake, lakini anakana kuwa lina  uhusiano na vijana wanaojihusisha na wanawake wenye vipato vikubwa (wanaolelewa)ili kupata unafuhu wa maisha.
Mario anasema baada ya  mapambano ya muda mrefu katika muziki alipata bahati ya kujiunga na kituo cha kuendeleza vipaji vya muziki kinachofahamika Tanzania House of Takent (THT), ambacho kilikuwa kinamilikiwa na aliyekua Mkurugenzi wa Uzalishaji na Vipindi wa Clouds Media, Ruge Mutahaba.

Anasema huko alikutana na wasanii ambao tayati walitoka kimuziki na kufanya nao, ikiwemo kuwatungia nyimbo.

Anawataka wasanii aliowahi kufanya nao kazi kuwa ni mwanadada Gigy Money kupitia  singo ya  ‘Nampa Papa’,  Nandaya  katika wimbo wa ‘Wasikudanganye’, Ditto ‘ Nabembea’ na Christian Bella ‘ Yapambe’.

Mwaka jana Mario aliingia mkataba na produza Hanscana  kwa ajili ya kurekodi na  kufanya video za nyimbo zake.

Hata hivyo anasema mkataba huo hautamzuia kufanya kazi na THT.

Anasema ngoma ya Chibonge imempa heshima ambayo hakuwahi kufikiria kama ataipata katika tasnia ya muziki.

“Kikubwa ambacho najivunia katika ngoma ya Chibonge ni heshima niliyoipata,  wengi wamegundua uwezo wangu katika kuimba kupitia nyimbo hii,”ana sema  Mario ambaye hivi karibuni aliachia  singo nyingine inayokwenda kwa jina la ‘Inatosha’.

Anasema licha ya kwamba amewai kutunga nyimbo kadhaa za wasainii maarufu  lakini kwa upande wake hajawahi kutungiwa.

“Sisemi kama haiwezekani, kama atatokea mtunzi ambaye atakuawa na uwezo kunizidi  nitakua tayari kuutumia wimbo wake,”anasema.  

Mario awali alikuwa akifanya kazi ya kutunga nyimbo  zinazoimbwa na wasanii wengine  bure lakini kwa sasa itabidi inabidi achangie gaharama.

“Kwa sasa siwezi kufanya kazi kwa ajili ya kujulikana, niliowapatia wanatosha, mtu anayehitaji wimbo ajipange kifedha ama tuandikishiane mapato yatakayo patika katika huo wimbo tugawane,” anasema Mario.

Anasema anapenda kuwatungia wasanii wa kike kwasabasabu  hana upinzani nao katika  suala zima la sauti kufanana.

“Huwa napenda kuwatungia nyimbo wanawake kwakua hatuwezi kufanana sauti, ni tofauti na wanaume,”anasema.

Hivi karibuni  msanini huyo aliposti katika mtandano picha ya gari aina ya BMW, kitendo kilichowafanya mashabiki wengi wa muziki kujiuliza amepata wapi fedha za kununulia  usafiri huo wa gharama.

“Mimi nimeanza kufanya sanaa chini kwa chini kwa muda mrefu hivyo watu wasistushwe na mafaniko wanayoyaona, yametokana na muziki na  hakuna kingine,”anasema.

Mario aliwahi kuhusishwa kuwa na mahusiana na mwanadada Amber  Lulu ambaye pia ni msanii wa muziki wa Bongo Fleva, lakini ,mwenyewe anakana.

“Sijawahi kuwa na uhusiano na Amber  Lulu, mimi namchukulia kama dada yangu, na si yeye tu, hakuna msanini niliyewahi kutoka naye,”anasema.

Anasema ukaribu wake na  Amber Lulu ulitokana na shuguli zao za muziki lakini si kitu kingine.

Mario anasema kwa sasa hana msanii mpenzi na hafikirii kuwa naye kwakua bado anasafari ndefu katika muziki hivyo  asingependa kuchanganya  vitu viwili.

“Nimejiwekea malengo katika muziki ambayo nimeanza kuyatimiza hivyo sitaingia katika ulimwengu wa mapenzi mpaka sanaa itakaponilipa,” anasema Mario.

Mmoja wa wasanii wa kiume ambao amewahi kufanya nao kazi na kutafuta jinsi ya kutoka ni Hanstone , lakini kwa sasa ukaribu wao umepungua, hili analizungumzia kwa kusema;

“Hanstone  ni mdogo weangu ambaye tulikuwa pamoja ila kwa sasa kila mmoja anafanya mishe zake kwa sababu tumeshapata umaarufu,” anasema Hastone.

Anawashukuru mashabiki wake kwa kusema ndio waliomfikisha hapo alipo kutokana na kumuunga mkono katika kazi zake za muziki.