Home Latest News Masikini, matajiri wote wanaisoma

Masikini, matajiri wote wanaisoma

1110
0
SHARE

“Hatunywi sumu hatujinyongi, CCM mbele kwa mbele, tumeipenda wenyewe, chaguo letu wenyewe, CCM mbele kwa mbele……”

“CCM ni ile oh ni ile ile”, acha waisome namba eeh waisome namba CCM mbele kwa mbele “, Tumejipanga mwaka huu mtaisoma”….. wavimbe wapasuke watajijua wenyewe”,

Hayo ni mashairi yanayopatikana katika wimbo unaojulikana kama ‘CCM mbele kwa mbele’ ambao ulifanikiwa kupata umaarufu kwa kupitia upande wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wakati wa uchaguzi Mkuu uliopita.

Wimbo huo ambao naamini kwa waimbaji walilenga kuonyesha kwamba wenye kustahili kuisoma namba ni wapinzani lakini hali imekuwa tofauti na fikra walizokuwa wakifikiri.

Hata wakati Rais John Magufuli anaingia madarakani na kuanza kutimiza dhana yake ya kutumbua majipu iliyotafsiriwa na wenye kufikiri mambo kwa mapana yake kuwa na lengo la kupanga safu yake.

Ukweli ambao Magufuli, mashabiki na wapenzi wa chama chake hawakuwa tayari kuukubali zaidi ya kusema ililenga kuwaondoa matajiri waliosema walikuwa wakiishi ‘kimalaika’ ili nao waje kuishi kama ‘shetani’

Wakati akisema hayo watu wa kada ya chini waliamini kwamba inaweza kuwa msaada kwao ili waishi maisha mazuri kama waliyokuwa wakiishi matajiri hao.

Kama wimbo huo unavyosema watu wa hali ya chini wakaamini ‘matajiri hao wataisoma namba peke yao’ lakini cha kuchekesha pamoja na kuwabana hali imekuwa mbaya kwa hao matajiri na masikini.

Pamoja na kupewa matumaini makubwa ya kusaidia watu wa hali ya chini kama ambavyo Ilani ya chama chake kwa kuwa ndiye aliyeteuliwa kuisimamia.

Dk. Magufuli tayari ameshaonyesha si rahisi kuwawezesha vijana kupata ajira.

Kwa mara ya kwanza wakati akiwaapisha wakuu wa mikoa, Dk. Magufuli alijinasibu kutokuwa kiongozi wa kuzalisha ajira mpya kwa vijana.

Katika hotuba yake ya Ikulu kwa wakuu wa mikoa aliwataka kuwakamata vijana wasiotaka kufanyakazi jambo ambalo lilitaka kufanyiwa kazi na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda lakini lilishindikana kutokana na kukosa haki hiyo kisheria.

Katika hotuba hiyo hakuonyesha namna ya uzalishaji wa ajira na badala yake Rais Magufuli aliwataka wakuu wa mikoa wasimamie watu wafanyekazi ambazo hazipo huku akiwatuhumu wale wanaoshinda wakicheza Pool table kutwa nzima kuanzia asubuhi kukamatwa.

Uamuzi ambao Rais Magufuli ametafakari na kuona njia pekee ya kuwabana vijana wasiofanyakazi ni kuwakamata kwa nguvu na kuwapeleka kwenye mapori ili wakalime, akiamini kwamba hiyo inaweza kuwa dawa kwao.

Hadi leo Dk. Magufuli hajawaeleza hawa masikini aliowaahidi kwamba hatowaangusha ni kwa kiasi gani amewazalishia ajira mpya.

Magufuli na viongozi wake wameishia kuwataka vijana waende wakalime, hapa swali kla kujiuliza ni je, amekamilisha ahadi alizokuwa akizitoa za kuboresha sekta ya kilimo?

Nakumbuka wakati akifungua Bunge la 11, mwaka jana aliahidi kuendeleza sekta za mifugo na uvuvi na kilimo.

Kwa sekta ya kilimo aliahidi kuiangalia katika mtazamo wa kibiashara na viwanda kwa lengo la kuwa na viwanda vya kisasa vya kuongeza thamani mazao yatokanayo na kilimo.

Pamoja na Dk. Magufuli kila wakati kusema kwamba anajua matatizo makubwa yanayowakabili wakulima, wafugaji na wavuvi.

Swali ni kwamba kama anatambua uduni huo ambao aliuelezea sasa kwa nini, hajaanza na kutatua tatizo hilo hadi leo?.

Kweli Dk. Magufuli atakuwa amesahau zile njia alizowaahidi Watanzania kwamba atawashawishi watu wa sekta ya kilimo kwa kuboresha sekta hiyo ili vijana wengi zaidi wavutiwe na kujiunga nazo.

Tatizo wakati Magufuli alipokuwa akiwatumbua hao waliokuwa wakiitwa wanatafuna nchi ili waishi maisha ya kishetani wengi waliamini kwamba huenda sasa wale waliokuwa wakiishi kishetani hapo nyumbani ingekuwa wakati wao wa kuishi kimalaika.

Tofauti na ilivyokuwa ikiaminika hivi sasa hali imekuwa ngumu si kwa matajiri hao waliokuwa wakifaidika bali kwa wote wakiwamo masikini waliokuwa wakishangilia wakidhani wao watapata nafuu.

Maumivu ya maisha yanayoshuhudiwa sasa yamekuwa yakikumba wote pasipo kubagua watu kwa kada zao za dini, kabila vyama hata kama ulikuwa ulali kuhakikisha CCM inashinda.

Sitaki kuamini hivi sasa kama Mkuu wa nchi amesahau kusimamia utoaji wa pembejeo, kutoa zana za kisasa za kilimo, ufugaji na uvuvi kwa ajili ya kuboresha sekta hizo na kuwaacha watu hawa waisome namba kiasi hiki.

Sitaki kuamiani kwamba Rais atakuwa amewaacha wakulima hawa waisome namba kutokana na kuacha kuwaletea wataalamu wa ugani, kuacha kuwawezesha kupata masoko ya uhakika ya mazao yao, kuwapatia mikopo kwa kupitia Benki ya Kilimo ili kumilisha lengo la wapiga kura wake.

Hakuna asiyeisoma namba hasa watu wa chini wakiwemo wakulima ambao hutumia huduma za fedha za kampuni za simu, pamoja na kuwaahidi kuwaondolea kero mbalimbali za kodi.

SHABAN MATUTU, +255 717 368 668