Home Makala Miaka minne ya JPM makamishna watano TRA

Miaka minne ya JPM makamishna watano TRA

1900
0
SHARE

*JPM aamua kusimmama na hoja za wanyonge

Na ASHA BANI

NI safari ya milima na mabonde, ambapo tangu alipteuliwa kuongoza nchi Novemba 5, 2015, Rais Dk. John Magufuli hadi sasa ameshateua makamishna wanne kuiongoza Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).

Hadi kufikia Juni Juni 8, 2019,  alipotangaza kumteua Edwin Mhede kushika wadhifa huo akichukua nafasi ya Charles Kichere aliyemteua kuwa katibu tawala wa Mkoa wa Njombe.

Taarifa iliyotolewa na kurugenzi ya nawasiliano Ikulu ilieleza nafasi ya Mhede aliyekuwa naibu katibu mkuu wa viwanda na biashara itajazwa baadaye.

Mabadiliko ya TRA

Hadi sasa kutokana na uteuzi huo inafanya idadi ya makamishna wakuu waliohudumu chini ya Rais John Magufuli kufika watano ikimjumuisha Rished Bade aliyemkuta wakati anaapishwa.

Bade aliteuliwa kushika wadhifa huo Mei 2014 na Rais Mstaafu Jakaya Kikwete ambaye alihudumu mpaka mwishoni nwa mwaka 2015 alipotenguliwa.

Baada ya kumuondoa Bade, Rais Magufuli alijaza nafasi hiyo kwa kumteua Dk. Philip Mpango ambaye baada ya kuridhishwa na utendaji wake alimpandisha cheo, kwanza alimteua kuwa mbunge na kisha akampa Uwaziri wa Fedha na Mipango.

Kuondoka kwa Mpango kulimpa nafasi Alphayo Kidata kuwa kamishna mkuu wa TRA akitoka kuwa katibu mkuu wa ardhi, nyumba na makazi.

Baada ya muda mfupi wa kuwa kamishna mkuu, Kidata alirudishwa kwenye wadhifa wake wa awali ila akapelekwa Ikulu.

Baada ya Kidata kuwa katibu Mkuu Ikulu mwaka 2017, Rais Magufuli alimteua Charles Kichere kuwa Kamishna wa kodi, nafasi aliyodumu hadi Juni 7 alipopelekwa Njombe kuchukua nafasi iliyoachwa na Erick Shitindi aliyestaafu.

Sasa Dk. Edwin Mhede  amechukua mikoba ya kuiongoza TRA akitarajiwa kukidhi matarajio ya Serikali ya Tanzania na wafanyabiashara pia.

Kwa upande wa Serikali, Rais Magufuli anataka idadi ya walipakodi iongezeke kutoka milioni 2.27 waliopo sasa huku wafanyabiashara wakitaka kuondolewa kwa kero wanazokabiliana nazo pindi wanapohudumiwa na maofisa wa mamlaka hiyo mfano makadirio makubwa ya kodi.

Hoja kubwa nne ambazo wafanyabiashara walimweleza Rais John Magufuli juzi juu ya Mamlaka ya Mapato nchini (TRA), zimechangia kwa kiasi kikubwa kungolewa kwa aliyekuwa Kamishna Mkuu wa mamlaka hiyo, Charles Kichere na kuifanya taasisi hiyo kuwa kaa la moto kwa vigogo.

Katika kikao kilichofanyika Ikulu wiki iliyopita, Waziri Mkuu Kasim Majali, alitoa mfano wa mfanyabiashara mmoja ambaye aliombwa rushwa na maofisa wa TRA na alivyokataa kuwapa walifungia mzigo wake kwenye bohari kwa miaka mitatu mpaka pale yeye alipoungilia ndipo mzigo huo ukatolewa Aprili mwaka huu.

Mfanyabiashara wa mafuta kutoka Mwanza, Agustino Makoye alisema ukusanyaji wa tozo ya ushuru wa huduma mkoani humo ni wa vitisho.

Makoye alisema wahusika wamekuwa wakitumia silaha jambo alilodai linakatisha tamaa ya kufanya biashara.

“Wanakuja polisi wakiwa na bunduki na wanakuwa watu wengi wakati ni ushuru tu ambao unakusanywa na Jiji na halmashauri. Kwanza ukiwaona tu wakiwa na bunduki wanakufanya ukose raha ya kufanya biashara,” alisema Makoye.

“Tumekuwa na wasiwasi na ukusanyaji huo kwa sababu mfumo si mzuri na tumekuwa tukipewa madai makubwa kuliko mtaji.

 “Wanakuja wanakuambia tangu mwaka 2015 hadi 2017 unadaiwa Sh milioni 200 na wewe una mtaji wa Sh  milioni 20,000 kwa hiyo Rais  nikuambie ukweli, wananchi hawa  wanachonganishwa na watumishi wasio waaminifu.

“Utakapoambiwa Sh milioni 200 utaambiwa ndani ya siku saba uzilete, utakapozunguka mlango wa nyuma utaambiwa leta Sh milioni 20 na ile ya kwanza haipo,”alisema Makoye.

Naye mfanyabiashara wa mafuta kutoka Singida, alilalamika kuwa biashara zake zimekuwa haziendi kwa sababu ya kodi nyingi hadi amefunga kiwanda chake cha mafuta cha mkoani Arusha.

“Hawa wakusanyaji wa kodi sifa yao kubwa imekuwa ni kufunga viwanda na hawatushauri tunafanyaje ili tusonge mbele.

“Mfano nalipa kodi 41, kila mmoja anataka apewe ushuru. Watu wengi hapa wameongelea service levy sasa haya yote nilipie wapi. Hii ni changamoto kubwa ukiuliza manispaa wanakwambia lipa kila mahali,” anasema.

Walivyong’oka

Bade ndio wa kwanza kuanza kungolewa na Rais Magufuli TRA Novemba 27 mwaka, 2015 kufuatia kasoro za kiutendaji zilizobainika katika mamlaka hiyo.

Rais alichukua uamuzi huo baada ya ziara ya kushtukiza ya Waziri Mkuu Majaliwa katika Bandarini jijini Dar es Salaam.

Katika ziara hiyo alibaini kuingizwa nchini kwa makontena zaidi ya 300 ambayo hayakulipiwa ushuru na hivyo kusababisha upotevu wa Sh bilioni 80.

Bade aliteuliwa na Rais wa awamu ya nne, Jakaya Kikwete kushika nafasi hiyo Tangu Mei 6, 2014 akichukua nafasi ya Harry Kiliya aliyestaafu Desemba 14, 2013.

KILIO CHA WAFANYABIASHARA

Mfanyabiashara wa mafuta kutoka Singida, alisema amelazimika kufunga kiwanda chake Mkoani Arusha kwa sababu ya kodi nyingi.

“Hawa wakusanyaji wa kodi sifa yao kubwa imekuwa ni kufunga viwanda na hawatushauri tunafanyaje ili tusonge mbele.

“Mfano nalipa kodi 41, kila mmoja anataka apewe ushuru. Watu wengi hapa wameongelea ‘service levy’ sasa haya yote nilipie wapi. Hii ni changamoto kubwa ukiuliza manispaa wanakwambia lipa kila mahali.

“Ushuru wa mashudu tunachajiwa kutoka wizarani sijui wana nguvu gani na huko barabarani wanachaji tena na gari inakamatwa na ikilala ni fedha nyingi tena unachajiwa,” alisema

BUTI ZA JESHI 5,000

Ofisa Usalama wa Kiwanda cha bora, Sylivery Buyaga anasema licha ya kutengeneza buti nzuri za jeshi kwa miaka mitatu sasa lakini jeshi la Tanzania bado linaagiza viatu nje.

Anasema wamekuwa wakijitahidi kuzalisha viatu hivyo kwa ubora wa hali ya juu kwa kutumia mashine nzuri na wameajiri zaidi ya watu 400 lakini mwitikio wa kuungwa mkono na jeshi nchini ni hafifu.

“Nasema haya kwa masikitiko makubwa, hadi sasa tuna pea 5,000 zilizo stoo lakini sasa tumejaribu kujitanua kwenda nje ya nchi kutafuta masoko lakini wanataka waone kwanza kama Tanzania ambako ndiyo nyumbani tumefanya nini hakuna kilichofanyika.

“Nchi ya Rwanda na Uganda waliomba kiwanda hicho kipelekwe nchini kwao na majeshi yatakuwa yananunua kila mwaka lakini kutokana na uzalendo suala hilo lilishindikana.

“Uganda tulipewa na eneo, viongozi wangu.. na barua nyingi nimeandika lakini hakuna aliyejibu barua hizo,” alilalamika.

Anasema kuhusu ubora wa ngozi, kutokana na mahitaji ya ngozi kutoka sehemu mbalimbali lakini wamekuwa wakiuziwa isiyokuwa na kiwango cha juu huku ile ya daraja la kwanza ikiuzwa katika nchi ya Kenya.

“Pia sekta hii ya ngozi ina matatizo makubwa sana kuanzia uchinjaji, ukusanyaji wa ngozi hadi kwa wale wanao process shida kubwa ninayoiona hapa ni sekta hii kuwa chini ya Wizara ya Viwanda na biashara wakati wataalamu wa ngozi waliosomea wako wizara ya mifugo, mimi nilikuwa naona sekta hii ingerudi kule kwa wataalamu waliosomea,”anasema.

RCO MORO KITANZINI

Kwa upande wake, mfanyabiashara kutoka Morogoro anasema wafanyakazi wa kiwanda cha tumbaku wamewekwa ndani bila kufunguliwa mashtaka.

Kutokana na hilo, Rais Magufuli alimsimamisha  Waziri wa Uwekezaji, Angella Kairuki kujibu hoja hiyo ambapo alisema  tayari aliwasiliana na  Wizara ya Mambo Ndani ya Nchi kwa ajili ya kuchukua hatua.

Majibu hayo yalionekana kutomridhisha Rais Magufuli ambaye kabla hajamsimamisha Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, anasema yeye mwenyewe alimsikia Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola akizungumzia suala hilo lakini hakuona hatua iliyochukuliwa.

Akijibu hoja hiyo, Katibu Mkuu wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Jacob Kingu,  alisema suala hilo wanalishughulikia na Rais Magufuli alipohoji aliyewaachia watu hao ni akina nani alisema ni Mkuu wa Upepelezi Mkoa wa Morogoro (RCO) na kutaka hapo hapo asimamishwe kazi.