Home Afrika Mashariki MIGOGORO SIASA ZA KENYA NI WA KI-HISTORIA

MIGOGORO SIASA ZA KENYA NI WA KI-HISTORIA

1354
0
SHARE

 

Uchaguzi kenya

NAIROBI, KENYA

Inaelezwa kwamba uchaguzi mkuu wa Kenya uliofanyika juzi ni miongoni mwa chaguzi ghali zaidi Barani Afrika.

Gharama za uchaguzi huo zinatarajiwa kufikia Dola za Kimarekani bilioni moja na hivyo kuufanya kuwa uchaguzi ghali zaidi katika kile kinachoitwa uwiano wa gharama kwa kila mpiga kura – (cost-per-voter basis).

Matumizi ya fedha kwa upande wa serikali na taasisi binafsi zote ziko juu kuliko wakati wowote katika historia za chaguzi katika nchi hiyo.

Wakati wananchi wa Kenya wakisubiri matokeo rasmi ya mwisho kuhusu uchaguzi huo wachambuzi wa mambo wanasema hali ya hofu kubwa iliyosambaa nchini kuelekea uchaguzi huo ilitokana na si kingine bali historia ya ghasia za uchaguzi hasa ule wa 2007 ambao ulisababisha vifo vya zaidi ya wananchi 1,200.

Baadhi ya wadadisi wa mambo wanasema maumivu haya wakati wa chaguzi hayatokani na suala la ukabila, husuan baina ya Waluo na Wakikuyu, suala ambalo limekuwa likitangazwa sana ili kuaminisha ulimwengu, bali ni mapambano kati nguvu ya demokrasia na wezi wa kura ili kujipatia ushindi isivyo halali.

Wadadisi hao wanaenda mbali zaidi na kusema ni mapambano kati ya walicho nacho na wasicho nacho. Ni mapambano ya wasicho nacho kujaribu kuwaondoa wakandamizaji wao. Wanasema Kenya ni nchi ambayo ghasia za 2007 zilikuwa zinatabiriwa kutokea, na zilitokea kwa haraka zaidi bila ya matarajio.

 

Hata hivyo nchi za Magharibi zimekuwa zinataja kwamba ikilinganishwa na jirani zake Tanzania, Uganda, Somalia na Ethiopia, Kenya kwa miaka mingi ilikuwa ni nchi tulivu na iliyopiga maendeleo makubwa kiuchumi.

 

Walikuwa wanaongeza kwa kusema muonekano wa Kenya katika uso wa dunia ulikuwa unatamaniwa na nchi nyingi Barani Afrika, kwani ni nchi pekee katika Ulimwengu wa Tatu (Third World) ambayo ni mwenyeji wa taasisi na mashirika kadha ya Umoja wa Mataifa, na pia kuwa kitovu cha mashirika ya kimataifa ya misaada ya kibandamu yanayohudumia nchi za ukanda huo.

 

Hivyo kutokana na mtazamo wa nchi za Magharibi katika sifa hizi, kuibuka ghafla kwa ghasia baada ya uchaguzi wa 2007 uliwastua sana.

 

Na ndiyo imekuwa sababu kubwa ya kuwapo hofu safari hii, ikiongezewa na malalamiko kutoka vyama vya upinzani kuhusu uchaguzi uliopita wa 2013 ambao walidai kulikuwapo wizi wa kura.

 

Hadi siku mbili kabla ya uchaguzi, kura nyingi za maoni zilimuonyesha mgombea urais wa chama cha Jubilee, rais aliye madarakani Uhuru Kenyatta akiongoza kwa asilimia nyembamba dhidi ya mpinzani wake Raila Odinga wa kutoka vyama vya muungano wa NASA.

Kuna watu wamekuwa na hofu nyingine kwamba pamoja na sheria na kanuni za uchaguzi zilizorekebishwa sana – nyingi kwa msukumo kutoka upinzani, bado hii haina garantii ya kutoibuka kwa ghasia wakati na baada ya uchaguzi.

Pengine hii ina mizizi ya ki-historia ambayo inakwenda nyuma zaidi ya miaka 50. Jomo Kenyatta na Oginga Odinga walikuwa na maswahiba wakuu katika siasa ambao baadaye, katika miaka ya 60 walijenga uadui mkubwa. Sasa hivi watoto wao wanaliendeleza bifu lile.