Home Habari Migogoro ya ardhi Mbarali na mwarobaini wake

Migogoro ya ardhi Mbarali na mwarobaini wake

239
0
SHARE

Na PENDO FUNDISHA-MBEYA.

BONDE la Mto Ruhaa Mkuu ni moja ya mabonde manne yanayounda bonde la mto Rufiji mengine ni bonde la mto Kilombelo, bonde la Luhevi na bonde la Rufiji chini.

Bonde hili linaukubwa wa kilomita za mraba 85554 sawa na asilimia 47 la eneo lote la bonde la rufiji likiwa na  mipaka ya hifadhi ya Ruhaa iliyopanuliwa kujumlisha hifadhi ya Usangu na ardhi dhoefu ya Ihefu kupitia tangazo la serikali namba 28 la March14, 2018.

Inaelezwa kuwa tangazo hili liliathiri Vijiji 33 vilivyopo kwenye hifadhi hiyo ambavyo vipo ndani ya Wilaya ya Mbarali, eneo lililokuwa kwenye hifadhi tangu enzi za mababu na kipindi hicho lilikuwa na ukubwa wa hekta 10,000 baada ya tangazo hilo la serikali la GN 28 zimefika zaidi ya hekta 20,000.

Utokana na tangazo hilo la serikali kutolewa mwaka 2018 kumekuwa na sintofahamu kwa wananchi wa Wilaya ya Mbarali hali iliyoibua kuibuka kwa migogoro na mivutano juu ya utekelezaji wa tangazo hilo ambao asilimia kubwa ulilenga kuwaondoa wananchi 40,000 ambao walikuwa wakiishi ndani ya vijiji hivyo.

Kutokana na uwepo huo wa mivutano wa migogoro kwa muda mrefu hatimaye Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanznaia, Dkt. John Pombe Magufuli amewza kuonyesha nia ya kumaliza tatizo hilo kwa njia ya amani na haki sawa kwa kila pande mbili ikiwemo wananchi wa Mbarali na serikali inayowaongoza.

Akiwa  Mkoani Mbeya kwa ziara ya kikazi ya siku tisa, Rais akizungumza na wananchi wa Mbarali alisema katika mchakato mzima wa utangazaji wa tangazo hilo, kuna mambo ambayo serikali iliyakosea na yapo mambo ambayo wananchi nao wameyakiuka hivyo muda wa ziada ulihitajika ili kutatua tatizo hilo na haki kupatikana kwa kila pande.

“Nasema kwa uwazi kabisa bila ya kuficha, tangazo hili lilipo tangzazwa, upande wa serikali yapo tuliyokosea yapo pia yaliyokuwa yamekosewa na wenyeji wa Mbarali,”alisema.

Rais, alitumia nafasi hiyo kuyaweka bayana baadhi ya mambo ambayo serikali imetajwa kuyakosea ni kwamba kabla ya serikali kutoa tangazo hilo la kuviondoa vijiji kwenye hifadhi hiyo ilipaswa kufahamu vijiji hivyo 33 ambavyo vilikuwa na watu 40,000 watu wake wataenda kuishi wapi.

Anasema, lakini pia, serikali ilipaswa kujiuliza kama inazihitaji hekta hizo 20,000 na kwa matumizi yapi kwani tangu awali wananchi walikuwa wakitumia hekta 10 na bado yapo maeneo ambayo yalikuwa hayatumiki.

Anasema, Wilaya ya Mbarali inafahamu kwamba Ruhaa Mkuu unaundwa na mito mikuu isiyopungua tisa ambayo ni Mbarali, Ruhaa, Kimani, kizigo, Lukosi, Ruhaa Mdogo, Ndembela na Chimala na kwamba inafahamika kwamba bonde la mto Ruhaa linachangamoto zake.

Anazitaja changamoto hizo kwamba ni  matumizi ya maji yasiyoendelevu kwenye kilimo cha umwagiliaji ikiwemo uchepushaji wa maji bila ya kibali.

“Mtu anachepusha maji wakati anafahamu maji ya mto huo ndio yanasaidia Mtera na Kidatu kupata umeme lakini maji haya ndio yatatumika kwenye mradi mkubwa wa umeme wa Rufiji lakini changamoto nyingine ni kilimo katika ulimaji wa miteremko, uchomaji moto olela nyingine ni uingizaji wa mifugo na uchimbaji holela  wa madini,”alisema.

Alisema, wazee wa miaka ya nyuma ni mashahidi wa zuri wa mto huo ambapo kipindi hicho walikuwa wanatumia na kuona maji yakitiririka bila ya kukatika katika na siku ya kikatika ujue kwa mwezi mara moja lakini hivi sasa maji yanaweza kukatia na kudumu zaidi ya miezi mitatu hata sita.

Lakini kwa sasa nyinyi wenyewe mnaona na kushuhudia viboko na samaki wanakufa kutokana na kukosa maji  hivyo kama taifa wameweka malengo yakufufua Kanda ya Kusini kuwa Kanda ya vVivutio vya Utalii.

Hofu inayotawala nchi ni kwamba mkakati huu wa kutangaza vivutio utafanikiwaje kama mito inakauka, viboko wanakufa kwani watalii hawezi fika kuangalia mizoga, kwa hiyo wanambarali mtambue kuwa serikali inaangalia mambo mengi katika kutatua migogoro hii.

Alisema, anajaribu kuangalia changamoto hizo lakini serikali ya awamu ya tano inasisitiza kilimo na suala la hapa kazi tu na bonde  la Mbarali ndilo linalolisha watanzania kupitia zao la mpunga na kwamba wapo baadhi ya watu wametengeneza ajira kupitia viwanda vingi vidogo vidogo vilivyoanzishwa.

“Ukiwa na changamoto hizi  ni lazima serikali iketi na kuona nini cha kufanya, wote tunahitaji haya wakulima wanahitajika sana na ninawapongeza kwa kulima, inawezekana msingekuwepo basi hata mchele tungekuwa tunaagiza nje lakini biashara ya kilimo nayo ni biashara kama biashara nyingine,”alisema.

Anasema, kutokana na changamoto hizo ambazo kwa asilimia kubwa ni mtambuka kwani nyingi zinategemeana ndio sababu serikali iliunda tume ya mawaziri 8 ikiongozwa na  Waziri wa Ardhi, Nyumba na Makazi, Willium Lukuvi, Waziri wa TAMISEMI, Suleiman Jafo na wengine.

“Mawaziri hao walikutana na kujadili mambo mengi, walitafiti na kujiridhisha juu ya changamoto hizo na ripoti imekamilika na itawasilishwa kwenye baraza na kutolewa maamuzi, nataka niwaeleze ndugu wanambarali kwamba serikali hii mliyoiweka madarakani kamwe haiwezi ikawaonea,”alisema.

Aidha, alisistiza kuwa serikali inazifahamu changamoto zinazowakabili wananchi kwani vipo vijiji vilivyokuwepo ndani ya hifadhi kabla ya hilo tangazo, vipo vijiji vinaofisi na shule hivyo haiwezekani vikabomolewa tu kwa madai kwamba hiyo ni hifadhi.

Lakini Rais, anatoa tahadhari kwa wananchi ambao walikubali kuondoka kwenye hifadhi hiyo na kulipwa fidia ya fedha kikiwemo kijiji cha Machimbo, lakini vipo vijiji mfano kijiji cha machimbo ambao walilipwa milioni 800 na katika zoezi hilo zilibaki milioni 31 kwamba  kwa mujibu wa makubaliano walipaswa kuondoka lakini hawajaondoka.

“ Hawa ambao walichukua fedha ya serikali lakini hawakuondoka dawa na jibu lao litakuja tofauti na wale ambao hawakuchukua,  nina waeleza ukweli huwezi kuvipata vyote kwani fedha ya serikali haipotei bure.

“Lakini lazima tukubali ukweli, kilimo tunakihitaji  lakini mazao ya kilimo tutayalima kwenye mawe?. Lazima twende kwenye maji na mbolea hivyo hii ni changamoto.

Aidha, Rais Magufuli alisema, changamoto nyingine ni mradi wa umwagiliaji wa moja ya skimu ambayo serikali ilitumia kiasi cha shilingi Milioni 23 na baadae mradi huo kugaiwa wananchi ambapo kila mwananchi alikabidhiwa kipande cha ardhi cha ukubwa wa ekari moja moja lakini wahusika waliviuza vipande hivyo kwa wafanyabiashara.

Anasema skimu moja iligharimu milioni 23 baadae wananchi waligaiwa ardhi hiyo kwa kila mmoja kupata ekari moja moja lakini waliuza vipande hivyo kwa watu wenye fedha na sasa nao wameingia kwenye orodha ya wanaolalamika kudai maeneo yao ya ardhi.

“Serikali baada ya kumaliza mradi huu wa skimu iligawanya ardhi kwa kuwapa ardhi wananchi ambao nao walizitoa kwa wafanyabiashara leo nao wanadai, sasa wewe serikali ilikupa bure..nyinyi mkauza…leo mnalalamika lakini nalo hili litatolewa ufafanuzi,”alisema.

Hata hivyo, anasema asilimia kubwa ya migogoro hii inatawaliwa na matumizi ya maji, wafugaji wanadai mifugo yao ipate maji, wakulima wanataka mazao yao yapate maji huku maji hay ohayo yanatakiwa kutumiwa na watanzania wote na huo ndio ukweli.

“Ukweli ni kwamba watu wameufuata mto huu, tena wameenda kwenye kona wakachimba zaidi ya kilomita kadhaa na kupeleka kwenye mashamba yao, kwa hiyo maji badala ya kutelemka na wao kuchukua machache yote yanaenda kwenye mashamba yao na kupotelea huko wengine hawapati maji, inafika mahala hata Mtera inakauka na ikikauka  umeme hautoki.

“Miaka ya nyuma tuliingia kwenye mzozo wa umeme kwa sababu mtera na kidatu zilikuwa zikikauka lakini watu wamejiunganishia na wengine wanapampu tu..jambo la ajabu ni kwamba hapa Mbarali nasikia kunamashine za kuvuta maji zaidi ya 200 na watu wakimaliza shughuli zao za kuiba maji hawakumbuki hata kufunga…wanaacha maji yanatiririka ovyo na wanajisahau kwamba maji yale ni rasilimali za watanzania wote na hii nayo ni chanagmoto,”alisema.

Hivyo kupitia changamoto hizo Rais,amewataka wanambarali kuwa wavumillivu kwani serikali ipo mwishoni kupata mbadala utakao saidia kupunguza au kuondoa kabisa kero na changamoto hizo alkini amewaonya kuachana kuendekeza majungu, fitina na visasi visivyo kuwa na tija bali wafanye kazi.