Home Habari MREMA: SASA NIMEPONA

MREMA: SASA NIMEPONA

1775
0
SHARE

NA MWANDISHI WETU


MWENYEKITI wa Chama cha Tanzania Labor Party (TLP), Agustine Mrema amesema sasa afya yake imeimarika hatua inayomfanya aamini kuwa amepona.

Mara kadhaa Mrema alizushiwa kufariki dunia, jambo ambalo amesema anaamini limewarudia waliomzushia uongo huo.

Pamoja na kuzungumzia afya yake, Mrema alisema anawashangaa waliokuwa wakimdhihaki kuwa yeye ni CCM, ambao wao ndio wamekuwa wa kwanza kuhamia huko.

Mrema ambaye pia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Parole, alitoa kauli hiyo mkoani Kilimanjaro katika ibada ya kumshukuru Mungu kwa kumponya maradhi ya saratani yaliyokuwa yakimkabili.

Akitoa shukurani hizo kwenye Kanisa Katoliki la Bikira Maria Malkia wa rozari, parokia ya Uomboni alisema anaamini Yesu amemponya kwa sababu wakati wote hakuwahi kwenda kwa mganga kuomba msaada.

“Ningekuwa nimeenda kupiga bao au nimeenda kwa mganga ningekuwa nababaika kuwa aliyeniponya ni Yesu au mganga.  Kwa kuwa sikwenda kwa mganga yoyote basi aliyeniponya ni Yesu, kwanini nisimtolee ushahidi?.

“Nasema Yesu ameniponya kwa sababu kulikuwa na kampeni ya kutaka niende kwa mizimu, nikaambiwa nikitaka mambo yangu yaninyookee basi niombe mizimu ya wazazi wangu wa zamani  na ndugu, kwa hiyo ile  mizimu sikuiomba, sikuabudu,  sikuiheshimu na nimepona… nani kama Yesu. Ningetambikia nisingethubutu kuja kusimama hapa madhabahuni,” alisema.

Aidha, Mrema aliwataka Watanzania kumuunga mkono Rais John Magufuli kwa juhudi anazofanya za kuimarisha uchumi na  kuhudumia wanyonge,

Alisema tangu  Rais Magufuli aingie madarakani amefanya kazi kubwa ya kuwasaidia wenye uhitaji ikiwamo kumpeleka India kwa matibabu.

“Namshukuru Rais Magufuli, kwa sababu Mungu anatenda miujiuza kupitia kwa watu, huwezi kumuona Yesu akitembea barabarani umuombe lifti kwa sababu  Yesu haendeshi  gari, lakini Mungu kwa kupitia watu, mimi nilikuwa mtu wa kufa maneno mengi yalisemwa sana mwaka 2015.

Inaendelea…………… Jipatie nakala ya gazeti la RAI