Home Makala Kimataifa MUBUTU SESESEKO ALIVYOCHANGIA DRC KUWA DAMPO LA WALANGUZI (3)

MUBUTU SESESEKO ALIVYOCHANGIA DRC KUWA DAMPO LA WALANGUZI (3)

1077
0
SHARE

NA MBWANA ALLYAMTU

SEHEMU ya pili tuliangazia chimbuko la nchi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), ambapo pamoja na mambo mbalimbali tulidadavua kuhusu mvutano wa kongo baada ya uhuru 1960. Hata hivyo, mfululizo wa makala hizi umelenga kuchambua namna Rais wa pili wa nchi hiyo, Mobutu Seseseko, alivyochangia mauaji ya Waziri Mkuu wa kwanza wa nchi hiyo, Patrice Lumumba. Pia jinsi alivyoigeuza Kongo kuwa jalala la mabepari. Endelea…

Jaribio la pili la kuipundua Serikali

Waziri Mkuu Moise Tshombe ambaye ndiye aliyekuwa kiongozi wa Congolese National Convention (CNC), alishinda uchaguzi kwa kura nyingi katika uchaguzi wa Machi 1965, lakini Kasa-Vubu alimtunuku kiongozi wa upinzani Evariste Kimba kuwa waziri mkuu. Hata hivyo Bunge lilipinga uteuzi huo. Kufikia hapo Serikali ilikuwa inayumba na Mobutu alichukua nafasi hiyo kwa kufanya mapinduzi ya kijeshi Novemba 25, 1965. Hii ni mara tu ya kufikisha umri wa miaka 35.

Chini ya utawala wa dharura, Mobutu alifikiri atapata nguvu kamili ya uongozi ndani ya miaka mitano. Hotuba yake ya kwanza baada ya kuchukua madaraka, Mobutu aliuambia umati wa watu mjini Leopoldville katika uwanja wa mkuu kuwa tangu wanasiasa waharibu nchi basi kwa miaka mitano hatutakuwa na chama cha siasa wala shughuli za kisiasa. Nguvu za bunge zilibaki kuwa ni mhuri tu kabla ya kufutwa kabisa lakini baadaye zilirudishwa.

Idadi ya majimbo ilipunguzwa na ushawishi wa majimbo ulidhoofishwa. Hii ilileta utawala wa amri kutoka kwa rais. Kwa kifupi Serikali ya Mobutu ilikuwa madhubuti na pia siasa haikutakiwa kabisa. Neno siasa lilikuwa ni sawa na uhaini na mwanasiasa alimaanishwa ni mtu mpenda rushwa, tapeli na mhaini.

Hata hivyo, mnamo mwaka 1966 kulianza msukumo wa vikundi vya vijana vya kujitolea vilianza mikakati ya kumuondoa Mobutu ambaye alijiita ‘Shujaa wa Pili wa Nchi’ baada ya Lumumba. Kwa nguvu zote alijipa cheo cha mtu aliyefuata nyayo za Lumumba na moja ya mambo aliyoazimia ni kuwa na Serikali halali ndani ya Congo. Mwaka 1967 kilizaliwa Chama cha Popular Movement of the Revolution (MPR) ambacho mpaka 1990 kilikua chama pekee cha kisiasa kilichoruhusiwa. Kwa lugha nyingine kilikuwa chama kilichoruhusiwa kisheria kuendesha shughuli za kisiasa nchi nzima katika imani moja.

Serikali ilikuwa ni njia ya kueneza chama. Kila raia alikuwa mwanachama wa MPR tangia kuzaliwa. Sera kubwa ya chama iliyojulikana kama N’Sele, ilikuwa na lengo la kuleta mapinduzi, uongozi wa vitendo ndani ya chama, hali hii ilionekana kama ni mchanyiko wa siasa za ujamaa na ubepari.

Msemo mashuhuri wa MPR ulikuwa: “Hatuko mlengo wa kulia wala wa kushoto” na wenyewe waliongeza: “Hatuko hata katikati” miaka ya baadaye. Chama cha MPR kilifanya uchaguzi kila baada ya miaka saba na mshindi kuwa raisi wa Jamhuri. Kila mwaka Mobutu alikuwa anapendekezwa kama mgombea pekee na jina lilipitishwa na uongozi mkuu wa chama ambao walikuwa na orodha ya wagombea nafasi za uongozi ndani ya chama. Bunge lilirudi kila baada ya miaka mitano kama chombo cha kutunga sheria na kilimpa rais wa chama nguvu zote za kuendesha Serikali.

Mwaka huo huo vyama vyote vya kutetea haki za wafanyakazi viliunganishwa na kuwa chama kimoja National Union of Zairian Workers, chama hiki kiliendeshwa moja kwa moja kwa amri kutoka serikalini. Kwa matakwa ya Mobutu mwenyewe chama hiki kilikuwa chombo cha kuhakikisha agenda za Serikali zinatekelezwa makazini iwe kwa sheria, nguvu au kwa ubishi.

Vyama vingine vya kutetea haki za wafanyakazi havikuruhusiwa mpaka 1991. Akikabiliwa na upinzani mwanzoni mwa utawala, Mobutu aliweza kuwanyamazisha, aliweza kuwafanya wapinzani wake wengi wamkubali kwa kutumia mbinu mbalimbali na mbinu hizo zikishindwa, nguvu ilitumika.

Mwaka 1966 mawaziri wanne waliwekwa ndani kwa kilichoaminika kuwa jaribio la kupindua Serikali. Walishtakiwa katika mahakama ya jeshi na walinyongwa hadharani, watu 50,000 wakishuhudia. Jeshi la Katanga liliteketezwa na mipango mingine iliyopangwa na jeshi la wazungu mwaka 1967 haikufanikiwa.

Mwaka 1970 karibia kila aliyekuwa tishio katika utawala wake alimalizwana sheria za chama na Serikali zilifikishwa karibu katika kila kona ya nchi. Mwaka huu unaweza kuelezewa kuwa mwaka uliofikisha kileleni utawala wa Mobutu wa kisheria na nguvu.

Mfalme Baudouin wa Ubelgiji alifanya ziara ya kiserikali iliyokuwa na mafanikio makubwa na mwaka huo huo uchaguzi wa bunge na rais ulifanyika. Chama cha MPR pekee ndio kilishiriki uchaguzi ingawa kwa kisheria ilitakiwa vyama viwili vya kisiasa vishiriki uchaguzi.

Kulingana na matokeo ya uchaguzi huo kwa mashaka, MPR ilipata ushindi wa asilimia 98.33 ya wapiga kura wote. Katika uchaguzi wa raisi, Mobutu alikuwa mgombea pekee, wapiga kura walipewa karatasi mbili wachague kati ya kijani kukubali au nyekundu kukataa. Mobutu alishinda kwa kuta 10.131.699 mpaka 157. Jinsi Mobutu alivyozidi kupata nguvu ndiyo alivyoimarisha jeshi kwa nia moja kubwa ya kumlinda yeye. Kulikuwa na Kikosi Maalum cha Raisi, Jeshi la Usalama, Jeshi Maalumu la Upelelezi na Vitendo.

+255679555526, +255765026057.