Home Latest News MUNDE TAMBWE UKOMBOZI WA VIJANA TABORA

MUNDE TAMBWE UKOMBOZI WA VIJANA TABORA

4243
0
SHARE
Mbunge wa Viti maalumu, Tabora, Munde Tambwe akikabidhi Mabati kwa Kamati ya Shule ya Msingi Kanyenye.

NA HASTIN LIUMBA, TABORA


MBUNGE wa viti maalumu mkoa wa Tabora Munde Tambwe ni kielelezo tosha cha utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Yapo mambo mengi ambayo mbunge huyo amefanikiwa kuyatekeleza kwa vitendo, ikiwa ni pamoja na kupigana na adui umasikini.

Mbunge huyo amefanikiwa kuunganisha kundi la vijana na kinamama na kuwapatia mafunzo mbalimbali ya wajasiliamali na upatikanaji wa mikopo na kutoa misaada kwa wenye uhitaji maalumu.

Katika mahojiano maalum na gazeti hili, Tambwe anaeleza mambo kadhaa ambayo amefanikiwa kuyatekeleza.

Tambwe anaeleza kuwa katika kipindi cha miaka miwili yapo mambo kadhaa ambayo amefanya kwa makundi mbalimbali hadi sasa.

Tambwe anasema kwa jitihada zake amewezesha wajasiliamali 8,700 kutoka katika kata 29 zilizoko jimbo la Tabora mjini kupatiwa mafunzo ya kujikwamua kiuchumi kwa gharama ya sh milioni 23.

Alisema amedhamiria kuwakomboa wajasiliamali wadogo mkoani na ataendelea kutoa mafunzo hayo kwa akina mama na vijana.

Lengo la kufanya hivyo ni  kuunga mkono juhudi za serikali ya Rais John Magufuli kusadia wanyonge nchini na yeye nia yake ni kuifanya Tabora kuwa ya viwanda.

Alisema baada ya semina na mafunzo yaliyotolewa kwenye Kata 29 za manispaa Tabora,sasa amejikita kwenye kutoa mitaji.

Julai mwaka huu ametoa kiasi cha sh 500,000 kwa kikundi cha kinamama wajasiliamali wa Kata ya Itetemia.

Alisema katika kata zote 29 mwaka 2017 ametoa sh milioni 14,500,000 ikiwa kila kata watapata mgao kama mtaji sh 500,000 ili mafunzo waliyopata wakaanze kuzalisha na hiyo ni njia sahihi kwa wajasiliamali hao kuelekea Tanzania ya viwanda.

Alisema licha kuanza kutoa mitaji hiyo bado kama mbunge wa viti maalumu ataendelea kuzunguka mkoa mzima ili kuendelea na mafunzo hayo hasa kwa kinamama ambao kimsingi ndiyo wazalishaji wakubwa nchini.

Aidha licha hayo aliongeza amejipanga na kuanza kufanyia kazi jinsi yakuwaunganisha wajasiliamali hao kutambuliwa na baraza za Uwekezaji nchini ili wawezeshwe katika misaada mbalimbali.

Alisema amefanikiwa katika kuwasaidia wajasiliamali hao lakini kwa mwaka 2010 vipo vikundi ambavyo alivianzisha na kuvipatia mikopo lakini vipo vilivyofanya vyema na vingine vilikufa kutokana na kutofata taratibu za vikundi.

Alisema mafunzo waliyopata wajasiliamali hao ni utengenezaji Sabuni za maji na ngumu,utengenezaji mishumaa,utengezaji batiki,utengenezaji Shampoo,utengenezaji Mafuta ya kula na usindikaji mazao mbalimbali.

Aidha aliongeza mafunzo mengine waliyopata ni namna ya utunzaji vitabu vya kumbukumbu za fedha,namna ya ukopati fedha kwenye taasisi za kifedha na jinsi ya kuweka na kukopa.

Tambwe alisema amepanga kuzunguka katika wilaya zote mkoani hapa ili kuendesha mafunzo hayo licha kuwa hana mfuko wa jimbo na kwamba hana itikadi za vyama licha ya yeye kuwa mwanaCCM.

Tambwe anaeleza kuwa alipambana na kuhakikisha mkopo wa fedha kiasi cha sh milioniu 150 zinapatikana kwa wajasiliamali wadogo mkoani Tabora ambao kimsingi walionyesha nia ya kutaka kuondokana na ufukara na umasikini walionao.

Hatua hii ilifikia mahali wakati nafatilia kupata mkopo huo kwa vikundi ambavyo nilikuwa nimeviwezesha katika semina za kuwawezesha zikiwemo zile zilizoendeshwa na baraza la taifa la uwezeshaji wananchi kiuchumi zinafanikiwa.

Katika wajasiliamali wadogo waliowezeshwa walikuwa ni zaidi 8000 hivyo niligeuka kama mtumishi wa benki ya Posta na hatimaye Mungu mwema walengwa hawa walifanikiwa kupatiwa mkopo wa sh milioni 150 na nawashukuru benki ya Posta (TPB Bank PLC) na imani mkopo huo toka wamepatiwa wameendelea kuzalisha.

Duniani kote anatambua kazi ya kina mama na vijana katika kitu kinachoitwa uwezeshaji hivyo pamoja na kwamba haikuwa kazi rahisi lakini siku zote kupanga ni kuchagua kundi hili ni kubwa nina imani wanazalisha.

Natumaini katika kuwapigania wajasiliamali hawa wadogo wakiwemo wanaume na wanawake ni matarajio na malengo yangu ni kuiondoa Tabora na umasikini ili jamii ipate maisha mema na mazuri mkoani kwetu.

Tambwe anasema na kufafanua yeye kwa kutambua ibara ya 57 ya kifungu kidogo cha (d) cha ilani ya mwaka 2015 imeeleza kuhusu suala la serikali yetu ya awamu ya tano kutenga sh milioni 50 kwa kila kijiji hivyo kutokana na hilo ndiyo maana yeye akabuni njia ya kuwawezesha wajasiliamali ambao tayari walishapaya mafunzo kupitia kwake.

Aliongeza kuwa jumla ya vikundi 18 ambapo wapo wanachama 205  vya mkoa wa Tabora ambavyo walikabidhiwa hundi ya sh milioni 150 toka benki ya Posta (TPB Bank PLC) na walikuwa wamejiwekeza akiba yao ya sh milioni 50,000,000.

 

 

hastinliumba@gmail.com-0788390788