Home Habari MWELEKEO MPYA WA MAGUFULI

MWELEKEO MPYA WA MAGUFULI

2077
0
SHARE

NA GABRIEL MUSHI


RAIS Dk. John Magufuli ameonesha dalili za mwelekeo na aina mpya ya kiutendaji inayoakisi dhamira yake ya kutaka wasaidizi wake kwenda na kasi anayoitaka katika kuwatumikia wananchi. RAI linachambua.

Kauli zilizobeba ukosoaji, maagizo na makatazo kwa wasaidizi wake alizozitoa mwanzoni mwa wiki hii, zinabeba dhana nzima ya mwelekeo mpya ndani ya mwaka mpya wa fedha wa 2018/19 ambao yeye mwenyewe kwa kauli yake aliuita mwaka mpya alioutoa sadaka kwa wateule wake akiwataka wafanye kazi.

Dalili za mwelekeo mpya wa kiutendaji za Rais Magufuli zilianza kuonekana Julai mosi mwaka huu kwa kuteua Makatibu Wakuu wa wizara, manaibu waziri pamoja na kumtumbua aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani, Dk. Mwigulu Nchemba na kuwabadilisha wizara baadhi ya mawaziri.

Akiwa katika mwaka wa pili na nusu wa utawala wake Julai 2, mwaka huu, akiwaapisha mawaziri na viongozi wengine 16 Ikulu jijini Dar es Salaam, alidhihirisha kuwa hafanyi mzaha katika mwelekeo wake huu mpya baada ya kutoa maelekezo mazito kwa wateule wake, pamoja na kuwakosoa waziwazi baadhi ya viongozi bila kuwataja majina.

Hata hivyo, kutokana na kauli alizokuwa akizitoa ni wazi ukosoaji huo ulielekezwa kwa Mwigulu, aliyeonekana kushindwa kuitumikia vema nafasi yake ya uwaziri, Andrew Chenge kwa kuonekana kuitumia vibaya nafasi yake ya Mwenyekiti wa Bunge hasa kwenye mjadala wa Korosho, Nape Nnauye na Hawa Ghasia ambao walikuwa mstari wa mbele katika kukosoa nia ya Serikali ya kutaka kuchukua  asilimia 65 ya ushuru wa mauzo ya Korosho nje ya nchi.

Rais ameonekana kutokuwa na hofu ya chama chake kupoteza wabunge 17 wa majimbo ya Kusini na ni wazi mwelekeo wake mpya unamtenganisha na viongozi wengi wa vyama vya siasa wanaojali masilahi ya vyama zaidi.

Ukweli wa hilo umemfanya kuwasema hadharani wabunge wake akiwamo Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa bila chembe ya mzaha. Na kwakuwa amedhamiria alisema anaamini ujumbe umefika na umepokelewa (message sent and delivery).

MAAGIZO KWA MAWAZIRI

Inaendelea……….. Jipatie nakala ya gazeti la RAI