Home Habari MWIGULU WAZIRI WA 25 ‘KUTUMBULIWA’ MAMBO YA NDANI

MWIGULU WAZIRI WA 25 ‘KUTUMBULIWA’ MAMBO YA NDANI

2108
0
SHARE

NA HILAL K SUED


DK. MWIGULU Nchemba ameingia kwenye orodha ya mawaziri 25, waliopata kuhudumu kwenye wizara ya Mambo ya Ndani tangu kupatikana kwa uhuru wa Tanganyika na baadae Tanzania Desemba 9, 1961.

Hatua ya Rais Dk. John Magufuli kumtumbua Mwigulu mwishoni mwa wiki iliyopita, kunamfanya mwanasiasa huyo kuwa Waziri wa 25 ndani ya wizara hiyo, huku mrithi wake Kangi Lugola akiwa wa 26.

Wachambuzi wa mambo wanaitazama wizara hiyo kama wizara ngumu inayowiana ugumu kwa karibu na wizara ya Maliasili na Utalii na iliyokuwa wizara ya Nishati na Madini, ambayo sasa imegawanywa.

Ugumu wa wizara ya Mambo ya Ndani unahalalishwa na vipindi vifupi vifupi walivyopata kukaa mawaziri wengi waliokalia kiti hicho, kama ilivyokuwa kwa Mwigulu ambaye aliteuliwa Juni 11, 2016 na kutenguliwa Julai 2, 2018.

Wakati wizara ya Mambo ya Ndani ikiwa na mawaziri 26 hadi sasa, Maliasili na Utalii yenyewe imeshaongozwa na mawaziri 23, huku kiti cha iliyokuwa wizara ya Nishati na Madini kilikaliwa na mawaziri 27, wa mwisho akiwa Prof. Sospeter Muhongo.

Mwigulu anaungana na baadhi ya mawaziri waliowahi kukalia nafasi hiyo akiwamo waziri wa kwanza wa wizara hiyo, George Kahama aliyehudumu kwa mwaka mmoja wa 1961/62.

Wengine ni Oscar Kambona (1962/63), Saidi Maswanya (1967/73), Ali Hassan Mwinyi (1975/77), Dk. Salmin Amour Juma (1979/80), Augustine Mrema (1990/94) na Muhammed Seif Khatib (2000/02).

HISTORIA

Baada ya Muungano kati ya Tanganyika na Zanzibar wizara hii iliwekwa kuwa miongoni mwa wizara za Muungano, kuanzia katikati ya miaka ya 1970 ilikuwa ikiongozwa na Waziri kutoka Visiwani.

Miongoni mwao alikuwamo Mwinyi, Hassan Nassor Moyo (1977/78) Salmin Amour na Abdallah Natepe (1980/83).

Wazanzibar wengine waliopata kuongoza wizara hiyo ni Ali Ameir Mohamed (1995/99), Muhammed Seif Khatib (2000-02) na Shamsi Vuai Nahodha (2010/12).

Inaendelea…………. Jipatie nakala ya gazeti la RAI