Home Habari kuu Nahendra Modi katika mkakati wa kuistaajabisha dunia

Nahendra Modi katika mkakati wa kuistaajabisha dunia

994
0
SHARE

Mwandishi Wetu Na Mashirika

WAKATI Dunia ikiwa katika taharuki inayotokana na kasi ya kusambaa kwa virusi vinavyosababisha ugonjwa wa corona (Covid-19), kila nchi imekuwa ikichukua hatua kwa kadiri inavyoonekana itasaidia kulinda watu wake dhidi ya mlipuko huo.

Tumewahi kuandika hapa kuhusu namna ambavyo maamuzi ya kupambana na ugonjwa huu yanavyotegemea wanasiasa na viongozi wakuu wa nchi, kusimamia hatua muhimu za kupambana na usambaji wa virusi hivi.

Wakati viongozi katika nchi nyingi duniani wakiendelea kuchukua hatua za kuzuia mikusanyiko, kuhamasisha wananchi wao kunawa mikono kila wakati kwa kutumia sabuni maalumu (sanitizers), kuepuka matumizi ya usafiri wa umma, kuweka vizuizi katika mipaka, viwanja vya ndege kwa kuhakikisha kila anayeingia anapimwa na wengine hata kuzuia safari za ndege, nchi nyingine zimejitokeza kuchukua hatua za ziada.

Nchi kadhaa duniani, ikiwemo Uingereza, Afrika Kusini, Italia na zimechukua hatua za ziada za kuhakikisha watu wote wanasalia ndani katika nyumba zao na kuhakikisha kuwa vyombo vya usalama vinatumika kutoa huduma kwa wananchi katika maeneo yao.

Lakini, hatua iliyochukuliwa na Waziri Mkuu wa India, Narendra Modi jana imeonekana kuwa ngumu zaidi baada ya kutangaza zuio la watu kutotoka katika nyumba zao kabisa.

Modi ameagiza wananchi wote kukaa nyumbani kwa muda wa siku 21 kuanzia jana, mkakati unaolenga kudhibiti maambukizi ya Covid-19 nchini humo ambapo hasi sasa watu zaidi ya 500 wameripotiwa kuwa na maambukizi na 11 wamefariki dunia.

Kutokana na agizo hilo la Modi, sehemu za ibada, maduka, masoko na ofisi zote nchi nzima zitafungwa. Huduma na usafiri wa umma nazo zitasitishwa kwa muda wote ambao nchi nzima imewekwa karantini.

Hatua hiyo ya Modi ni ya kipekee na kwa sasa kuna maswali mengi yanaulizwa kwamba kama nchi ikifungwa kabisa, hali inakuwaje? Hasa ikizingatiwa ukubwa wa nchi hiyo na idadi kubwa ya watu, wanaozidi bilioni 1.3.

India ni kati ya mataifa ambayo yana watu wengi zaidi duniani lakini sasa nayo imejumuka na nchi nyingine kama Mauritius, Uingereza na Afrika Kusini kutangaza marufuku ya watu kutoka nje.

Umuzi huo unaibua pia maswali ya namna nchi hiyo itakavyoweza kudhibiti watu hao bilioni 1.3 kutotoka nje na namna watakavyopata huduma zao, lakini tayari uamuzi umeshatolewa ikiwa ni baada ya Serikali kujiridhdisha kuwa itaweza kukabiliana na hali hiyo.

Waziri Mkuu wa India, Modi ametangaza zuio la watu kutotoka nje nchi nzima ikiwa ni hatua ya kuzuia maambukizi ya virusi vya corona, katazo ambalo limeanza kutekelezwa kuanzia usiku wa kuamkia jana, muda wa India na litadumu kwa muda wa siku 21.

“Hakuna mtu atakayeruhusiwa kutoka nje ya nyumba yake kabisa. Nchi nzima itafungwa kabisa. Hatua hii imechukuliwa ili kuokoa Taifa la India, raia wake wote na familia zote kwa ujumla… kila mtaa, kila jirani anapaswa kujifungia. Itatubidi kulipia uchumi, hili ni jukumu la kila mmoja wetu,”anasema.