Home Makala NATALIA ZANANA: JPM SAIDIA KUNDI LA VIJANA WALIOKATA TAMAA

NATALIA ZANANA: JPM SAIDIA KUNDI LA VIJANA WALIOKATA TAMAA

1776
0
SHARE

NA HARRIETH MANDARI


NATALIA Zanana ni mhitimu wa ngazi ya shahada katika masuala ya bima na utunzaji wa kumbukumbu (Bachelor of Insurance and Record Managememnt) katika Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) mwaka 2015.

Hata hivyo, kutokana na tatizo sugu la upatikanaji wa ajira, ameweza kuyakwamua maisha yake kwa kuuza juisi biashara ambayo inamfanya kuelekea kuwa milionea.

Jambo hili linamsukuma kuanza kuwasihi vijana hasa wale ambao wamehitimu na kukakaa vijiweni wakisubiri kupata ajira na wale walio bado masomoni, kuondokana na dhana kuwa maisha ni kuajiriwa pekee.

RAI wiki hii lilizungumza naye katika eneo lake la biashara lililoko Mikocheni, jijini Dar es Salaaam, ambako wateja wanafurika kufuata vinywaji katika mgahawa huo, ambao ni maarufu kwa utengenezaji wa juisi za matunda asilia, ijulikanao kama ‘Zanana juice box’.

Anasema tangu akiwa anasoma mwaka wa kwanza, alijiwekea malengo ya kuanza kujishughulisha na biashara hivyo kuweza kudhihirisha na kutimiza ndoto yake.

Mgahawa huo ambao ni maalumu kwa ajili ya viywaji vya asili mbalimbali vikiwamo juisi za matunda, ‘smoothies’, Saladi za matunda, Kahawa, pia amekuwa mbunifu zaidi kwa kuanzisha aina ya michanganyiko zaidi ya 70 ambapo huchanganya matunda na kutengeneza, ambapo ipo ambayo inaimarisha kinga ya mwili (immune system), ambayo hupendelewa sana na wateja wengi na wa rika mbalimbali.

Anasema amejijengea utamaduni wa kujisomea vitabu hasa vya afya na vya aina tofauti tofauti za matunda na kazi zake mwilini, kupitia hilo ameweza kubuni utengenezaji wa aina mbalimbali za vinywaji kama kuchanganya matunda na kupata juisi zenye virutubisho ambazo hupendwa sana na wateja wake.

“Kazi hii nilianza kabla hata sijamaliza chuo nilikuwa mwaka wa kwanza, kwani  nilijiwekea mtizamo kuwa ni lazima niwe na kitu nafanya hata baada ya kumaliza chuo badala ya kusuburi kupata ajira,” anasema.

Anasema anauchukia umasikini kupita kitu kingine chochote duniani, hivyo alianza kutafuta wazo la biashara ambalo lingeweza kumwingizia kipato na ambayo itapendwa na wateja na ndipo alipoamua kutengeneza  juisi.

“Nilianza kwa kutengeneza juisi ya kawaida tu na si kama ilivyo sasa, ambavyo nina aina nyingi sana za juisi,” anasema.

Natalia anaongeza kuwa biashara yake na mtaji wa shilingi 5,000 tu na akishirikiana na pacha wake walienda kununua maembe katika soko la Tandale wakanunua matunda na sukari na pia kwa pesa hiyo hiyo waliweza kupata na kilo ya sukari wakatengeneza  lita tano ambazo wateja waliiifurahia na ikaisha.

Anasema hali hiyo ilizidi kuwahamamsisha na walianza kuuza bidhaa hiyo kwa wateja kwa kutembeza barabarani na waliwauzia mafundi ujenzi  katika jengo wakati huo lilikuwa linaitwa Mlimani Tower.

“Kwanza kabisa mara baada ya kutengeneza juisi nilihakikisha mimi na ndugu yangu tunavaa vizuri na wasafi na pia kinywaji chetu tulikihifadhi vizuri kwa kisasa, hivyo kuweza kuvutia wateja wetu,” alisema.

Mtazamo wake juu ya wadada wanaopenda kupata fedha kwa njia ya haraka, anasema walipoanza tu kuuza juisi baadhi ya wateja walianza kuwaambia kuwa hawaendani na biashara hiyo, kwani wao ni warembo hawatakiwi kufanya kazi hiyo jambo ambalo Natalia anasema aliichukulia kama hamasa ya kuzidi kujibidiisha na kuwa mbunifu sana.

Kwanini alichagua kuuza kinywaji hicho

Anasema  kila mtu anayetaka kuanzisha biashara ni lazima kuanzisha ile ambayo utaiona ni fursa na pia iliyo ndani ya uwezo wake (mtaji).

Bidhaa nyingine ambazo Natalia anauza katika mgahawa wake

Natalia anasema mbali na utengenezaji wa kinywaji aina ya juice, pua hutengeneza Ice -cream mbalimbali, kahawa na pia saladi za aina mbalimbali za matunda.

Changamoto alizokuutana nazo katika safari yake ya biashara

Anasema wakati anaanza kuuza kinywaji hicho na kuanza kupata wateja wengi, baadhi ya watu walianza kusema wanafanya biashara ya kujiuza jambo ambalo anasema linamuuma sana.

“Ilifikia hata wakati watu walianza kutubeza na kusema kuwa tunauza unga na pia tunatafuta wanaume, kwa kweli Watanzania ipo haja ya kupata elimu zaidi ya ujasiriamali kwani bado watu wengi wanadhani ili kufanikiwa kibiashara ni kwa kupitia njia za mkato hawajui kuwa hata mbuyu ulianza kama mchicha,” anasema.

Mafanikio ambayo ameyapata hadi hivi sasa

Anasema jambo analojivunia mpaka hapo alipofikia ni kupanuka kwa biashara yake na pia kuweza kupata wateja wengi. Vilevile, Natalia anasema anajivunia kuweza kuajiri vijana wengine watano ambao wamejipatia ajira na sasa wananweza kusaidia familia zao kupitia kazi hiyo.

Wito wake kwa vijana hasa wa kike nchini

Kwa wanawake wenzangu hasa kundi la vijana wa kike nchini,  acheni kubweteka na pia wasichana waache kuishi maisha ya kuigiza.

“Unakuta mdada yuko radhi akope shilingi 5,000 ili na yeye ende akaonekane akiwa kwenye  hoteli  kubwa hapa mjini,  akajipige picha na kuituma mitandaoni ili naye aonekane ana maisha ya hali ya juu,  jambo ambalo si la busara na halileti tija katika maisha yake,” anasema.

Natalia anaongeza kuwa iwapo angedunduliza fedha kidogo kidogo angeweza kupata mtaji na kuanzisha biashara ndogo ndogo.

Wito wake kwa Serikali ya awamu ya tano:

Anatoa wito kwa Rais John Magufuli, kulikumbuka kundi la vijana hasa wale wanaomaliza elimu ya juu, kwa kuanzisha programu  za mafunzo ya ujasiriamali  nchini ili kujishughulisha wabadilike mitizamo na kuanza  kujishughulisha na kuanzisha biashara badala  ya kukaa vijiweni na kulaumu serikali.

“Siri ya mafanikio ni kufanya kazi kwa bidii na vilevile kuwa wabunifu kulingana na aina ya  biashara ambayo kijana atakuwa ameamua kuifanya anasema.