Home Makala Ndayishimiye atakuwa mkombozi, ‘jinamizi’ jingine Burundi?

Ndayishimiye atakuwa mkombozi, ‘jinamizi’ jingine Burundi?

605
0
SHARE

Leonard Mang’oha

CHAMA Tawala nchini Burundi CNDD-FDD kimempitisha Meja Jenerali Evariste Ndayishimiye, kuwa mgombea urasi wa chama hicho katika uchaguzi wa nchi hiyoi utakaofanyika Mei mwaka huu na kuhitimisha mihula mitatu ya Rais wa sasa, Piere Nkurunzinza.

Meja Jenerali Ndayishimiye anayetoka mkoa wenye ushawishi katika siasa za Burundi wa Gitega amekuwa Katibu Mkuu wa chama tangu 2016 na mshauri wa masuala ya kijeshi wa Rais Nkurunzinza.

Mshirika huyo wa karibu wa Rais Nkurunzinza ni miongoni waliotiliana saini mwaka 2013 kumaliza vita ya wenyewe kwa wenyewe ya mwaka 2005.

Itakumbukwa kuwa mwaka 2015 Taifa hilo liliingia katika machafuko baada ya Rais Nkurunzinza kutanganza kuwania mhula wa tatu wa uongozi kwa madai kuwa katika ya inamruhusu kufanya hivyo kwa sababu mhula wake wa kwanza haukuwa wa kikatiba.

Kutokana na tangazo hili nchi hiyo iliingia katika machafuko yaliyosababisha Taifa hilo kurejea katika mgogoro wa wenyewe ambapo maelfu ya raia wake walilazimika kuihama nchi yao kutafuta hifadhi katika mataifa jirani ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Rwanda na Tanzania.

Tume ya uchunguzi ya Umoja wa Mataifa iliyopewa jukumu la kufuatilia ukiukwaji wa haki za binadamu nchini humo ilieleza kuwa kumekuwa na ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu, ikiwa ni pamoja na uhalifu dhidi ya ubinadamu, kati ya mwaka 2017 na 2018.

Tume hiyo iliundwa Septemba 2016 kutokana na azimio la Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa na ripoti yake iliwasiliwa katika baraza hilo Septemba 2018.

Hata hivyo baadaye mwaka 2018, Rais Nkurunziza alitangaza kuwa hatagombea mhula mwingine wa urais wa Burundi.

Nkurunzinza aliyezaliwa mwaka 1963, ni kama kielelezo cha utawala wa usiofuata misingi ya utawala bora katika ukanda wa Afrika Mashariki ambapo utawala wake umekubwa na malalamiko kutoka kwa makundi mbalimbali ndani ya Burundi na jumuiya za kimataifa kama ilivyo kwa Rais Paul Kagame wa Rwanda na Yoweri Museveni ya Uganda.

Kuteuliwa kwa Ndayishimiye kuwa mgombea urais katika uchaguzi wa mwaka huu unaelezwa kupokewa kwa furaha na wafuasi wengi wa CNDD-FDD wakimwona kuwa ni mkombozi mpya katika Taifa hilo.

Hata hivyo kunaendelea kuwapo hali ya wasiwasi kutokana na ukaribu baina yake na Rais wa sasa ambapo baadhi ya wachambuzi wa masuala ya siuasa za Burundi wanautazama uteuzi wake kama kusalia madarakani kwa Nkurunzinza katika sura nyingine.

Ikiwa Ndayishimiye atafanikiwa kuingia madarakani atakabiliwa na jukumu zito la kujenga umoja wa kitaifa uliovurugika kwa miongo kadhaa kutokana na vita ya kikabila iliyohitimishwa kwaka 2005 na kisha vurugu za baada ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2005.

Hili itakuwa hatua muhimu kwa maendeleo ya Taifa hilo katika ili kuwafanya wananchi wake kuwa wamoja na kushiriki shughuli za maendeleo kikamilifu.

Miongoni mwa matatizo yanayoikabili Burundi ni pamoja na kuwa na idadi kubwa wakimbizi kutoka nchi hiyo walioikimbia nchi yao kutokana na machafuko ya baada ya uchaguzi. Kwa mujibu wa Shirika la Kuhudumia Wakimbizi la Umoja wa Mataifa (UNHCR) hadi katikati ya mwezi Aprili mwaka 2015 zaidi ya raia 8000 wa nchi hiyo waliripotiwa kuomba hifadhi katika nchi jirani zikiwa ni wiki mbili tu tangu yalipozuka mjachafuko ya baada ya uchaguzi huku idadi ya watu walioikimbiua nchi hiyo kwa ujumla wakikadiriwa kuwa ni zaidi ya 400,000.

Kutokana na hatua kadhaa ambazo zimekuwa zikichukuliwa na Serikali ya Nkurunzinza baadhi ya raia wa walikuwa wakiishi uhamishoni baada ya kukimbnia machafuko wameanza kurejea wakiwamo wale walikuwa wamepewa hifadhi hapa nchini.

Kwa vipindi tofauti Taifa hilo limepitia katika misukosuko ya kisiasa baada ya mapinduzi ya mwaka 1993 alipouawa aliyekuwa Rais wa kwanza wa kuchaguliwa wa nchi hiyo, Melchoior Ndadaye, kutoka katika kabila la wahutu na kusababisha kuzuka kwa vita ya wenyewe kwa wenyewe iliyodumu hadi mwaka 2005.

Vita hiyo ya wenyewe kwa wenyewe ilitokea wakati wa uongozi wa Rais wa zamani wa nchi hiyo, Pierre Buyoya, ambaye aliiongioza kwa vipindi viwili tofauti kuanzia mwaka 1987 hadi 1993 kisha mwaka 1996 hadi 2003.

Zaidi ya watu 300,000 wanaelezwa kuuawa katika vita hiyo iliyohusisha ya jeshi lenye watutsi wa ya walio wachache dhidi ya waasi kutoka kabia la wahutu jamii iliyo ya wengi nchini Burundi.

Buyoya aliingia madarakani kwa mapinduzi ya kijeshi mwaka 1987 kabla ya kukubali kushindwa katika uchaguzi wa mwaka 1993 aliposhindwa na Ndadaye ambaye hata hivyo alikaa madarakani kwa miezi minne tu kabla ya kuuawa na kundi la wanajeshi Watutsi wenye misimamo mikali, katika jaribio la mapinduzi lililoitumbukiza Burundi katika mgogoro wa kikabila.

Buyoya 69, ni miongoni mwa waliohusika katika mchakato wa amani uliomaliza vita vya wenyewe kwa wenyewe na kuongoza uchaguzi uliomweka madarakan aliyekuwa kiongizo wa waasi wa kihutu na Rais wa sasa, Nkurunziza hapo mwaka 2005.

Katika miaka ya karibuni Serikali ya Kabila imekuwa ikiendesha mpango wa kutaka kumkamata Buyoya na maofisa wengine 16, wakihusishwa na mauaji ya Ndadaye, hata hivyo mpango huo umekuwa ukipingwa vikali na jumuiya za kimataifa kwa madai kuwa kunaweza kuzusha hisia za kikabila ambazo zinaweza kuliingiza Taifa hilo katika machafuko mengine.

Burundi kupitia kwa mwendesha mashtaka wake imekuwa ikieleza kuwa uchunguzi uliofanyika umebainisha kuwa watu hao walihusika katika kupanga na kutekeleza mauaji dhidi ya Ndadaye.

Swali ni je, ikiwa Ndayishimiye ataukwaa urais wa nchi hiyo ataendeleza mpango huo na ikiwa atauendeleza nini athari zake katika Taifa hilo la Jumuiya ya Afrika Mashariki. Kuendeleza ama kutoendeleza mpango huo pamoja na kushughulikia masuala mengine muhimu yanayoihusu Burundi kutatoa taswira halisi kama Ndayishimiye ni mkombozi ama jinamizi jingine Burundi.