Home Makala NI JESHI PEKEE LAWEZA KUAMUA HATMA YA JAMMEH

NI JESHI PEKEE LAWEZA KUAMUA HATMA YA JAMMEH

719
0
SHARE

DAKAR, SENEGAL


Akizungumza kupitia runninga baada ya uchaguzi wa Desemba 1 mwaka jana Rais wa Gambia Yahya Jammeh alimpogeza mpinzani wake Adama Barrow aliyeshinda na kusema: “Nakutakia kila la kheri, wananchi wa Gambia wameamua.”

Tangazo hili la kushindwa lilipokewa kwa hisia za kushangaza na za furaha pia katika mitaa ya nchi hiyo. Baada ya mashambulizi makali dhidi ya wapinzani na kukataa kwake kuwepo kwa watazamaji wa kimataifa, wananchi wengi walidhani Jammeh angetafuta tu namna ya kushinda, potelea mbali matokeo ya hesabu za kura.

Na wengi waliona ukingo wa utawala utawala wake – kupitia sanduku la kura – wa miaka 22 ya ukandamizaji wa demokrasia ulionekana kama ni ushindi mkubwa kwa misingi hiyo hiyo ya demokrasia nchini Gambia na kwingineko Barani Afrika.

Hata hivyo sherehe zilizimwa wiki moja baadaye pale Jammeh alipofuta kauli yake ya kushindwa akidai kuwepo kwa ukiukwaji mkubwa mno katika mchakato mzima wa uchaguzi na katika kuhesabu kura.

Kuharibika kwa ghafla mchakato wa kuachiana madaraka nchini Gambia kuliwaibua viongozi wanne wa nchi za magharibi mwa Afrika kama sehemu ya umoja wa ECOWAS kumtembelea Jammeh katika jaribio lao lilioshindikana la kumshawishi akabidhi madaraka kwa mpinzani wake Adama Barrow.

Na wakati hayo yakijiri, Umoja wa Afrika (AU), Umoja wa Mataifa (UN), Umoja wa Ulaya (EU), Marekani na nchi nyingine wamekuwa wakipaza sauti zao kumuunga mkono Barrow. Na msukumo mkubwa umekuwa ukiongezeka nchini Gambia kwenyewe wakati Umoja wa Wafanyabiashara (Chamber of Commerce), vyama vya walimu, wanahabari, na Tume ya Uchaguzi wakimtuhumu Jammeh kwa kubadilisha uamuzi wake.

Hata hivyo, wakati Jammeh akishikilia uamuzi wake, kuna kundi moja muhimu nchini humo ambalo bado linaonekana kumuunga mkono – jeshi na vikosi vya usalama vya nchi hiyo.

Wakati Jammeh alipokubali kushindwa mkuu wa majeshi wa nchi hiyo Jenerali Badjie alitangaza utii kwa Barrow, lakini Jammeh alipobadilisha kauli, naye pia alifanya hivyo na hapo hapo alituma vikosi kukamata makao makuu ya Tume ya Uchaguzi.

Swali la kujiuliza kwa nini jeshi linaendelea kumuunga Mkono Jammeh? Jibu moja la swali hili ni kwamba vikosi vyote vya ulinzi na usalama vimelelewa katika hali ya utii mkubwa kwa Jammeh. Kupandishwa (na kushushwa vyeo) huamuliwa na suala la utii, si kutokana na uwezo, ukakamavu, uzoefu au muda katika utumishi.

Wale ambao wanaonekana ni watiifu kwa Jammeh hupandishwa vyeo kwa ngazi kadha, hata kutokea katika ukuruta na kufikia uofisa. Na wakati huo huo wale askari ambao uaminifu wao na utii si mzito sana hujikuta wakiteremshwa vyeo, kufukuzwa, kufungwa, au hata nyakati nyingine kunyongwa. Mtandao mkubwa wa kikachero miongoni mwa wanajeshi huwafanya kuwa katika hali ya wasiwasi mkubwa siku zote.

Hata hivyo hudaiwa kwamba sehemu kubwa ya utiifu kwa Jammeh hutokana na kuajiriwa kwa raia wa nchi za nje katika jeshi la nchi hiyo – kama vile ilivyo katika idara ya mahakama.

Jammeh anadaiwa kuajiri watu wa kikundi cha MFDC, kikundi kinachopigania kujitenga cha jimbo la Casamance kusini mwa nchi ya Senegal.

[Ikumbukwe nchi ya Senegal imeizunguka kabisa nchi ndogo ya Gambia isipokuwa sehemu ndogo tu ya mto Gambia unapoingia Bahari ya Atlantic.]

Hii ni njia mojawapo ya Jammeh kuhusishwa na uasi wa watu wa Casamache dhidi ya serikali ya Senegal. Hivyo askari wanaoajiriwa kutoka sehemu hiyo huwa hawana masilahi na kile kinachoendelea kwa wananchi wa Gambia kwa ujumla na daima huwa tayari kumuunga mkono Jammeh.

Njia nyingine anayoitumia Jammeh kujihakikishia utiifu ni kwamba siku zotehuwa mwangalifu katika kuwaweka maafisa wa ngazi za juu kwa muda mrefu katika nyadhifa zao kwa hofu kwamba wanaweza kuwa tishio kwa masilahi yake.

Na wakati huo huo anafahamu kwamba vikundi vya maafisa anaowafukuza kazi wanaweza kumletea matatizo baadaye. Hivyo wengi wa hao anaowafukuza jeshini huwapa kazi za uwaziri au ubalozi nchi za nje. Hivyo ushawishi mkubwa wa vikosi vya usalama na ulinzi hauishii tu katika kambi za jeshi, bali nje pia.

Hivyo maafisa wengi ndani ya jeshi, wanahofu hatma ya taasisi yao iwapo itaangukia chini ya rais mpya. Chini ya urais wa Dawda Jawara (aliyepinduliwa na Jammeh mwaka 1994), jeshi lilionekana kama vile lilisahaulika kabisa.

Jammeh alipotwaa madaraka alilikuza jeshi lake na kulipa zana za kisasa ni malipo mazuri na hali nzuri ya maisha. Aidha aliunda kundi la kijasusi la National Intelligence Agency (NIA) na lile la wanamgambo wakorofi linalojulikana kama ‘Jungulars‘.

Chini ya Jammeh, askari wa vikosi vya ulinzi wana kinga chini ya sheria. Sheria tata ya Kinga ya 2001 inampa rais uwezo wa kutoa kinga ya kutoshitakiwa kwa askari wa vyombo vya usalama wakati wa hali ya hatari.

Sheria hii iliusukumwa na azma ya kuwalinda polisi waliowafyatulia risasi wanafunzi walioandamana mwaka 2000 wakiwaua wanafunzi 12.

Aidha ipo hofu pia kwa maafisa wa vikosi vya ulinzi na usalama kuhusu hatma yao iwapo utawala mpya utaingia. Mara baada tu ya uchaguzi viongozi wa upinzani walianza kusikika wakisema uwepo wa uwezekano wa kufanya uchunguzi wa ukiukwaji wa haki za binadamu chini ya utawala wa Jammeh.

Uchunguzi wa namna hii ungeibua madai mengi ua utesaji na mauaji dhidi ya wanahabari, wafuasi wa upinzani, viongozi wa dini na wengineo yaliyokuwa yakifanywa na vikosi vya usalama.

Lakini hata hivyo, pamoja na ukweli kwamba maafisa wengi katika jeshi wana wasiwasi ya hatma yao iwapo Jammeh ataachia madaraka, lakini wapo baadhi yao wamekuwa hawaridhiki kabisa na utawala wa Jammeh.

Tangu atwae madaraka, Jammeh amenusurika na majaribio manane ya kupinduliwa na jeshi, jaribio la mwisho lilikuwa mwaka 2014.

Hii pekee ni kielelezo tosha kwamba kuna vikundi katika jeshi ambavyo vuitafurahi kumuona Jammeh aondoke madarakani. Hali kadhalika kuna matukio mengi ya askari na maafisa wa jeshi kujiondoa wenyewe jeshini.

Isitoshe upendeleo utokanao na masuala ya kikabila ndani ya jeshi umeleta mgawanyiko mkubwa ndani ya vikosi hivyo. Jammeh amewapa vyeo vingi vya juu watu wa kabila lake dogo la Jola.

Sasa hivi Mkuu wa majeshi, vikosi vya ulinzi vya rais, na vile vya kijasusi ni wa kabila lake la Jola.