Home KIMATAIFA “NKHOSI SIKELEL’AFRIKA” na uchaguzi mkuu Afrika Kusini

“NKHOSI SIKELEL’AFRIKA” na uchaguzi mkuu Afrika Kusini

276
0
SHARE

Na Comred Mbwana Allyamtu

Taifa la Afrika Kusini mnamo tarehe 8/5/2019, lilitekeleza wajibu wa  kikatiba yake ya 1994, kwa wananchi wake kuwachagua Wawakilishi wa Mikoa (Provincial legislature) na Wabunge.

Zaidi ya raia million 17.76 sawa na 65.99% walipiga kura kati ya watu milioni 27.7 walio jiandikisha katika mikoa yote tisa (9). Vyama 30 vilishiriki katika uchaguzi wa mikoa na 27 katika uchaguzi wa Wabunge.

Uchaguzi ulifanyika kwa usalama na hakuna kitendo chochote cha uvunjifu wa amani kilicho ripotiwa, katika mikoa yote isipokuwa Kwa Zulu Natal ambako iliripotiwa kuwa jumla ya watu 30, kwa mujibu wa maofisa wa Tume Huru ya Uchaguzi  (IEC), walishikiliwa kwa makosa ya kupiga kura zaidi ya mara moja.

Kwa mujibu wa sheria ya uchaguzi, mtu mmoja kupiga kura zaidi ya mara moja ni kitendo cha jinai. Iwapo mtu atakutwa na kosa hilo anaweza kufungwa kwa miezi sita, au faini ya Rand 2000. 

Waangalizi mbali mbali kutoka jumuiya tofauti walituma waangalizi, huku ECOWAS ikimteua raisi wa zamani wa Nigeria, Goodluck Jonathan kuwa mwangalizi ma Umoja wa Afrika (AU), ulimteua Dk. Jakaya Kikwete, rais mstaafu wa awamu ya tatu wa Tanzania, kuwa kiongozi wa jopo la waangalizi wa umoja huo.

Mchakato wa kuhesabu kura ulifanywa kwa mfumo wa elekitroniki na ilichukua siku tatu (tarehe 9-11) kwa Tume kuanza kutoa matokeo ya jumla kwa mikoa yote pamoja na yale ya Bunge. Jumla ya kura milioni 17.76, sawa na asilimia 65.99% ya kula zote zilizopigwa zilihesabiwa. Asilimia 1.33% ya kura ndizo zilizoharibika. 

Katika uchaguzi huu, mikoa iliyoshiriki kwenye uchaguzi wa majimbo ni Western Cape, Eastern Cape, Northern Cape, Northern East, Free State, Kwa Zulu Natal, Gauteng, Mpumalanga na Limpopo. Katika mikoa hii vyama hivyo vilishiriki katika kutafuta viti vya Mabaraza ya Kutunga Sheria ya Mikoa. 

Katika mikoa yote, ANC kilishinda katika mikoa minane kwa 22.41% , huku chama cha DA kikikamata mkoa wa Western Cape kwa ushindi wa 55.42% na EFF kwa kikipata 3.79% katika jimbo la Western Cape na ANC kuwa chama pinzani katika mkoa huo wenye wakaazi wengi Wazungu.

Pamoja na ushindi huo, ANC kimeporomoka kutoka 62.35%  (mwaka 2014) hadi 57.8% katika uchaguzi huu. 

Kwa upande wa upinzani pia imeonyesha kushuka kwa ushawishi wa chama kikuu cha upimzamani—DA kimeporomoka kutoka 22.32%  (2014) mpaka 21.0% katika uchaguzi huu sawa na anguko la  1.32%.

Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi, Gren Mashinini alisema kuwa jumla ya vyama 27 vilivyoshiriki katika uchaguzi huu, ni vyama 14 pekee vilivyofanikiwa kupata Wabunge, mavyo ni ANC, DA, EFF, IFP, VF PLUS, COPE, AL JAMAA, CDP, ATM, GOOD, PAC, NFP, UDM na AIC.

Kati ya vyama hivyo, vitano ndivyovilikuwa juu—ANC iliyopata 57.8%, DA 21.0%, EFF 11.79%, IFP  3.3% na VF Plus kikipata 2.5%

Katika matokeo hayo ya Bunge, ANC kilifanikiwa kutetea nafasi yake ya kuendelea kudhibiti Bunge kwa kupata jumla ya viti 230, kati ya 201. Upande wa pili uliongozwa na DA ambacho kilipata viti 84, EFF viti 44  na IFP cha Chief Buthalezi, kikipata viti 14 na chama cha VF Plus kinachoongozwa na  Pieter Groenwald, kikipata viti 10.

Kwa matokeo haya, ANC imepoteza viti 19 kutoka viti 249 ilio kuwa navyo tangu 2014 mpaka 230 katika uchaguzi wa mwaka huu. DA pia ikipoteza viti 5 kutoka viti 89 ilivyo kuwa navyo mpaka viti 84 katika uchaguzi wa mwaka huu. EFF kimeongeza viti kutoka 25 mpaka 44 mwaka huu. Nje ya kuongeza viti katika Bunge la Taifa, pia kimeongeza nguvu kwa kutwaa majimbo matatu ya Mpumalanga, kwa kushika nafasi ya pili nyuma ya ANC, Northwest Provincial Legislature kwa kupata 18.64% na mkoa wa Limpopo kwa kupata 14.38%.

EFF kimepata mafanikio makubwa ya karibu 90% kwa kupata jumla ya kura 1.35 milioni, na Wabunge 44 katika Bunge la Taifa na kuwa ngome kuu ya upinzani (official opposition) katika mikoa mitatu (3). Mafanikio haya ni makubwa ukizingatia na umri wa chama hicho ambacho kilianzishwa mwaka 2013, tofauti na DA ambacho kilianzishwa mwaka wa 1959 (kikitokana na chama tanzu cha Nationalist), lakini kikabadilishwa jina baada ya muungano wa vyama viwili—Nationalist na Liberal. 

DA kina ngome katika maeneo yanayokaliwa na jamii za watu Wazungu—hasa Western Cape, Northern Cape na Free State. 

Mbali na DA pia chama tawala cha  ANC tangu Uchaguzi Mkuu wa kwanza wa mwaka 1994, ndicho chenye  pesa na miundombinu, ukilinganisha na EFF, lakini pamoja na hayo, ANC kimeendelea kupoteza mvuto kwa wananchi. Takwimu inaonesha kwamba ANC kimekuwa kikiporomoka kwa kila baada ya uchaguzi. ANC kimekuwa kikishuka kati ya 4% – 5% kila uchaguzi. 

DA kimeporomoka kwa kati ya asiliia 2-3 tangu 2014 baada ya kuundwa kwa EFF. Hata hivyo, EFF ndio chama pekee katika uchaguzi huu ambacho kimepata mafanikio kwa ongezeko la 5% kutoka 6.35% tangu 2014 na kufikia  11% katika uchaguzi huu. Ikiwa ni ongezeko la 5%-6%.  Kutokana na takwimu hizi inakifanya chama cha EFF kuwa ndio chama pekee kilicho kuwa na kuimarika katika uchaguzi huu.

Uchaguzi huu ni wa sita toka kumalizika kwa utawala wa kibaguzi mwaka 1994, na kupitishwa kwa azimio la amani na maridhiano iliyofuatiwa na mkataba wa uhuru (Freedom Charter), na Nelson Mandela alichaguliwa kuwa rais wa kwanza, akifuatiwa na Thabo Mbeki mwaka wa 1999 ambaye alilazimishwa kujiuzhuru mwaka 2008 kwa sababu ya mzozo wa kisiasa ndani ya ANC. Kgalema Motlanthe aliteuliwa kuwa rais wa mpito na mnamo Mei, 2009,  Jacob Zuma aliachauliwa kuwa rais. Lakini mwaka jana, jana Zima naye alijiuzuru kutokana na kashafya na kurithiwa na Cyril Ramaphosa.

Afrika Kusini inatumia mfumo wa Bunge wenye Wabunge 400 wanaochaguliwa moja kwa moja na wananchi (direct vote). Halafu kuna Bunge lenye Wabunge 200 ambao huchaguliwa kutoka katika miji na wengine 200 ambao wanachaguliwa kutoka katika mikoa.

Baada ya uchaguzi kumalizika, Rais wa anachaguliwa na Bunge baada ya chama chenye viti vingi (viti 201), kupendekeza jina.

Katika Bunge la Mkoa, ambalo hutofautiana kwa ukubwa na Bunge la Taifa,Wabunge wa mikoa ni lati ya 30 hadi 80, kutegemea kutegemea idadi ya asilimia ya kila chama ilichopata. Wawakilishi wa kila jimbo watachaguliwa na Bunge husika la mkoa, huku Baraza Kuu la Taifa la Mikoa (National Council of Provincial Legislature) lina wajumbe 90, 10 kutoka mikoa yote tisa, ambao huchaguliwa na kila Bunge la Mkoa. 

Katika uchaguzi huu, kumekuwa na ongezeko la 14% ya wapiga kura ukilinganisha na mwaka 2014. Tume ya Uchaguzi imesema kuwa wapiga kura wa mwaka huu ni milioni 27.7, wapiga kura wa ndani (local voters) wakiwa milioni 26.15 na walioko nje ya nchi (International Voters) 171,134.

Matokeo haya yamekipa ushindi ANC wa viti 230, sawa na asilimia 57.8%. Kikatiba na kikanuni rais wa sasa, Cyril Ramaphosa anatazamiwa kuendelea na muhura wake wa pili endapo ataidhinishwa na Bunge.

Cyril Ramaphosa amewahi kuwa makamu wa raisi wa Afrika Kusini chini ya serikali ya Jacob Zuma toka mwaka 2014 mpaka mwaka 2019 alipo chukua nafasi ya urais baada ya Zuma kulazimishwa kujiuzulu baada ya kile kilichoitwa “mgogoro wa Zuma ndani ya chama.” 

Ramaphosa ni mwanasiasa mwenye ukwasi mkubwa wa Dola za Kimarekani 450 milioni (£340 milioni)

Pamoja na kuwa bepari wa kutupwa, alikuwa mwanachama wa ANC na kiongozi mkuu wa Kamati ya Utendaji ya Taifa, nafasi ambayo, wakosoaji wake wanasema ilimpa habari za ndani za chama na kuitumia nafasi hiyo myeti kujijenga kibiashara na kujiimarisha kisiasa.

Ramaphosa akiwa Mkurungezi wa Lonmin, kampuni ya kimataifa inayomilki mgodi huo huko Marikana, alituhumiwa kwa kuwasaliti wafanyakazi ambao kwa wakati mmoja aliwatetea na kuwa upande wao. Mashtaka haya yalikuja baada ya polisi kuwaua wachimba mgodi 34 wakiwa kazini mwezi wa Agosti 2012 katika mgodi wa Marikana, huku hili likiwa ndio tukio baya kuwahi kushuhudiwa tangu kumalizika kwa utawala wa Makaburu mwaka 1994. 

Uhusika wake ulianza kupata nguvu baada ya kuzuka kwa barua pepe zinazo muonyesha Ramaphosa kuwa ndiye aliye toa amri ya kutaka hatua kuchukuliwa dhidi ya wachimba mgodi kwa kushiriki katika ‘mgomo kali’ mgomo ambao uliokumbwa na ghasia.

Japo kuwa baadae uchunguzi wa tume maalumu iliyoundwa na raisi Zuma ulimsafisha Ramaphosa dhidi ya kesi ya mauaji ya huko Marikana. Lakini Mpaka sasa kiongozi wa chama cha Economic Freedom Fighter (EFF) Julias Malema anasisitiza kuwa Ramaphosa alihusika na mauaji ya Marikana na kumtaja Ramaphosa kama kibaraka wa watu weupe.

Hata hivyo, Ramaphosa, ambae anatajwa na jarida la uchumi la Forbes kuwa mmoja wa wafanyabiashara wakubwa mwaka 2014 aliamua kuachana na biashara baada ya kuchaguliwa kuwa makamu wa rais wa nchi hiyo, baada ya kuteuliwa kuwa makamu wa raisi wa nchi hiyo aliamua kuachana na shughuli za kibiashara na kuingia kwenye siasa tena, gazeti la kifedha la kimataifa la Forbes, lilimnukuu akisema, “aliachana na shughuli zake za biashara ili kuepuka migogoro ya kiutawala” huyu ndie Cyril Matemela Ramaphosa,  raisi wa awamu ya tano wa taifa la Afrika kusini.

Mungu ibariki Afrika ibariki Afrika……”Nkhosi Sikelel’Afrika