Home Maoni NSSF KUINGIZA SEKTA ISIYO RASMI UWE MPANGO ENDELEVU

NSSF KUINGIZA SEKTA ISIYO RASMI UWE MPANGO ENDELEVU

4392
0
SHARE

 


UWAMUZI wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) umechelewa sana. Tunasema hivyo kwa sababu, NSSF ni shirika lililorithi mikoba ya iliyokuwa National Provident Fund (NPF), shirika ambalo lilikuwa halibagui wafanyakazi—wenye ajira za kudumu, ajira za muda, na wakiokuwa wanafanya vibarua vya mikataba.

NSSF ilipoanzishwa kwa Sheria ya Bunge Namba 28 ya mwaka 1997, ikajikita zaidi kushughulika na waajiriwa, kwa sababu ya urahisi wa kuwapata—maana kampuni au taasisi yoyote yenye kuajiri watu wengi, inalazimika kisheria, kuwaingiza wafanyakazi wake kwenye mfuko huu.

Katika miaka ya nyuma, Sekta isiyo Rasmi ilikuwa bado kushamiri, lakini baada ya Sera ya Soko Huria kuanza kufanya kazi, sekta hiyo imeonekana kuwa muhimu kwa kuwa inaajiri watu wengi.

Utafiti kuhusu ajira uliofanyuka 2014, unaonesha kwamba Sekta hii ilikwa ya pili baada ya Sekta ya Kilimo, kuajiri asilimia 10 ya waajiriwa wote Tanzania. Kati ya 2006 na 2014, ajira katika Sekta isiyo Rasmi  iliongezaka kutoka watu milioni 1.6 hadi 4.3. Hii ni idadi kubwa ya watu kuachwa nje ya mfumo wa hifadhi ya jamii. Ndio maana tunasema NSSF wamechelewa kufanya uwamuzi wa kuwaingiza watu walio katika sekta hii.

 Kinachotakiwa sasa ni kwa NSSF kujipanga kutoa elimu kwa kundi hili na kuhakikisha kwamba watu wengi zaidi wanajiunga na mfuko, ili waweze kufaidi mafao mbali mbali na huduma, ikiwa ni pamoja na malipo ya tiba, uzazi, elimu kwa watoto na pensheni ya uzeenu.

Huduma ya hifadhi ya jamii kwa wote, liwe ndilo lengo la NSSF ili kuhakikisha kwamba Watanzania wanaishi maisha bora zaidi wakiwa bado ni vijana, na wakizeeka wawe ni watu wenye matumaini ya kuendelea kuishi vizuri.

Ikiwa huduma ya hifadhi ya jamii itawafikia wananchi wote—katika sekta binafsi na Sekta isiyo Rasmi—wakulima, wajasiriamali, wavuvi, wachimba madini, mamalishe, wauza mitumba, bodaboda na mafundi mchundo, Tanzania itakuwa imepiga hatua kubwa sana.

Tunaamini kuwa mpango huu wa kuwashirikisha wananchi waliojiajiri, au walioajiriwa katika Sekta isyo Rasmi, ndio jibu sahihi la kupambana na kupunguza umaskini miongoni mwa Watanzania.

Tujua fika kwamba NSSF linatoa fursa myingi kwa vikundi vya wajasiriamali, kuwawezesha kujenga au kununua nyumba ambazo wanachama watazilipia kidogo kidogo, au chukua mikopo yenye riba ndogo kwa ajili ya kusomesha watoto wao, au kujiendeleza kielimu wao wenyewe.

Pia tunaamini kwa kutumia ubunifu, ujuzi  na uwezo walionao, viongozi wa NSSF, wataipa kipaumbele Sekta isyo Rasmi na kuwaongoza wajiriwa na waliojiajiri katika kuwasaidi kupanga mambo yatakayo leta tija na mafanikio katika maisha ya mtu mmoja mmoja au vikundi.

Tuna amini kuwa NSSF ipo kwa ajili ya kuonesha njia ya ukombozi kwa wananchi watakao kubali kujiunga na mfuko huu. Tuwawatakia kila la kheri katika safari hii muhimu waliyoianza.