Home Makala Prof. Kabudi kaanza kama Ajibu

Prof. Kabudi kaanza kama Ajibu

1562
0
SHARE

Ile mechi kati ya Lisu na Prof Kabudi tayari imeashaanza na aliyeuanza mpira huo ni Prof Kabudi kapiga mpira nje kama alivyofanya Ajib kwenye match ya raundi ya kwanza vs Simba.

Kabudi kaanza kwa kusema kuna watu wanaisema nchi vibaya huko nje na ni bora wakae kimya.

Lisu ameonekana kutulia na kuurudisha mpira uwanjani tayari ameshajibu kuwa kuna tofauti kati ya nchi na Serikali.

Rais wa 26 wa Marekani aliwahi kusema namnukuu “Patriotism means to stand by the country. It does not mean to stand by the president” (Uzalendo ni kusimama na nchi yako, Uzalendo haumaanishi kusimama na Rais) Niwakati wa kupima sasa hivi Lisu anaikosoa Serikali au nchi? Lisu anaitukana Tanzania au Serikali? Je kwa sheria zetu Lisu kavunja sheria?

Mwelekeo!

Kabudi anataka kuelekea mwelekeo ule ule wa kina Musiba na wengineo. Tulichokikosa awali vilikuwa ni vitu viwili kwanza mtu Credible ambaye angeweza kujibu hoja za Lisu lakini cha pili tunajibu kwa kupambana naye au tunamsaidia kupata wahalifu wake.

Serikali ina jukumu la kusaidia na kuonyesha dunia kuwa haihusiki. Aidha, iwe watatumia upelelezi dhahiri au watadanganya lakini mwelekeo wa ushindi wetu ni kulaani mashambulizi dhidi ya Lisu na kumsaidia katika kuwabaini waliomdhuru.

Kwa kufanya hivyo tungeishinda hii game mapema sana…. Huu ndio mwelekeo wa ushindi.

Rais wetu leo kafungua ukurasa mpya ambao ndio mwelekeo anaoutaka. Suala la Mo kutekwa limemuongezea wafuasi mno kwa namna Rais alivyolizungumzia.

Huo ndio mwelekeo unaohitajika, Kabudi ana la kujifunza labla ya kuanza kuattack hoja za issue ya Lisu. Nilijua yupo aggressive sana na angeanza na issue hii. Jana nilisema kuwa ujio wake unabeba agenda gani kwenye hii Wizara na ataanza na issue ya Lisu na kama nikivyotabiri yametimia.

Katoa mpira njee….umerudishwa kati haya tunaangalia kwanza Ball possession. Ole Mushi