Home Makala Kimataifa Samor Machel kutoka Ruvuma mpaka Maputo

Samor Machel kutoka Ruvuma mpaka Maputo

1473
0
SHARE

NA COMRED MBWANA ALLYAMTU

na Afrika Kusini, tena upande wa ndani ya Afrika Kusini; yeye Kamanda Samora Machel na watu wengine 33 walipoteza maisha huku watu 9 waliokuwa wamekaa viti vya nyuma ya ndege wakinusurika.

Inaaminiwa kwamba ndege yake ilidunguliwa na utawala wa Kibaguzi wa Afrika Kusini wa wakati huo. Safari ya mwisho ya maisha ya Samora Moisés Machel wa Msumbiji ikawa imeishia hapo. Pamoja na historia hiyo ya Samora Machel sasa tuitazame Ruvuma na umuhimu wake katika harakati za ukombozi wa Msumbiji.

“KUTOKA RUVUMA MPAKA MAPUTO”.

HUWEZI kuzungumzia historia ya Uhuru wa  Msumbiji pasipo kutaja mkoa wa Ruvuma mahali ambapo vuguvugu zote za ukombozi kwa sehemu kubwa zilifanyika kuhakikisha Msumbiji inakomboka. Eneo la (Mkenda) lililopo Kijiji cha Nakawale Kata ya Muhukuru mkoani Ruvuma ni sehemu muhimu kabisa katika historia ya msumbiji na ndio maana katika makala hii yangu ya “………Kutoka Ruvuma mpaka Maputo” ni sehemu muhimu ya kuitmbua Msumbiji lakini pia kujua na kutambua mchango wa Tanzania katika ukombozi wa msumbiji hasa mkoa wa Ruvuma. 

Eneo hilo lililopo kiasi cha  kilometa  124 hivi kutoka Songea mjini  kwa kizazi kipya ni eneo ambalo huenda likaonekana halina “umuhimu kabisa” wala umuhimu wowote ule, lakini kwa wazee wanaofuatilia historia za majirani wa Tanzania ni kijiji chenye historia  iliyozama katika vichwa. 

Binafsi nilifika eneo hilo nilipokuwa safarini kuelekeza Maputo mapema mwaka 2016 eneo hilo alijulikani sana kwa baadhi ya watanzania.

Pengine ni kutokana na ukweli huo  kijiji ncha jirani mara tu ukivuka mpaka wa Tanzania na msumbiji kuna hifadhi nzuri inayoelezea mipango ya kwanza ya mashambulio dhidi ya Wareno kutokea mto Ruvuma. Kwa namna yoyote ile eneo hilo ambalo ni kitongoji  ni muhimu katika historia ya Msumbiji na hata Tanzania lakini  ukiachia mbali maelezo ya wakazi wenye umri mkubwa hakuna  jitihada zozote zinazoonekana kufanywa kuhifadhi historia mwanana katika ukuombozi wa Afrika hasa taifa la Msumbiji na Tanzania na hili nimekuwa nikilieleza mara kwa mara katika makala zangu.

Katika kijiji cha Mkenda mkoani Ruvuma ni eneo ambalo wapigania uhuru wa Msumbiji waliokuwa wakiongozwa na Rais wa chama cha Frelimo wakati huo miaka ya 1960 Eduardo  Mondrane, walipoanzia safari yao yenye furaha na majonzi papo hapo mkoani Ruvuma, na safari ya kwenda kuanza mapambano ya kumng’oa Mreno. 

Inaelezwa na wakazi wa eneo hilo kuwa hapo ndipo wapigania uhuru wa Msumbiji na vikosi vya kusaidi kutoka Tanzania katika miaka ya 1968  wakiongozwa na Rais wa chama cha Frelimo Eduardo Mondlane  na mkuu wa majeshi Samora MaChel waliweka kambi kabla ya kuingia eneo la Congreso. Ilibidi wafanye kituo hapo kujipanga na kutuma watu wa mwanzo kuangalia mahali ambapo walikuwa watengeneze kambi nyingine ya kujipanga wakati wa kusubiri kuanza kwa mashambulizi kwa lengo la ukombozi.

FRELIMO katika harakati za ukombozi ilijituma na Ilikuwa ni kazi kubwa lakini, viongozi ambao ndio wapiganishaji walikuwa na muda mwingi wa kuchora namna watakavyoendesha vita ya Msumbiji na mahali pa kujihami baada ya  mapigano ya mwanzo. Pamoja na kwamba kwa sasa kuna daraja la Mkenda linalounga Tanzania kwa upande wa Songea na  Congress kwa upande wa Msumbiji, kijiji cha Mkenda yenyewe imebaki tupu kabisa katika historia kwani siku zinavyoenda, simulizi zinavyozidi kuchakachuliwa eneo hilo linabaki katika roho za waliokumbana na kashikashi ya kwanza ya vita vya Msumbiji na kizazi kipya hakina cha kufanya. Ukivuka Mkenda na kuingia Msumbiji , hali ni tofauti sana.

Wao wameweka kumbukumbu zao la tukio la siku ya kwanza baada ya kuvuka mto Ruvuma. Na kuanza safari za kwenda Maputo kwa ukombozi Katika eneo hilo la Congreso zipo mpaka nyumba zilizokuwa zikitumika kulala viongozi mbalimbali pamoja na magogo waliyokuwa wakikalia wakati wa mikutano ya kwanza ya mipango ya vita hivyo vya ukombozi. Mimi nakumbuka nilipo fika Msumbiji kupitia hapo kijijini nilishuhudia upande wa Tanzania kudolola kiuchumi huku upande wa msumbiji kukiwa kumehifadhi historia zake za ukombozi.

Na kumbuka nilipo kutana na Alexandre Jalarne mtunza makumbusho hayo ya Taifa ya Msumbiji katika eneo la Congresso akielezea kwa  maringo na kujiamini alisema kuwa viongozi mbalimbali wa ndani na nje ya nchi hiyo wamekuwa wakifika katika makumbusho hayo kwa ajili ya kuangalia  kumbukumbu mbalimbali zilizohifadhiwa kiasili. Ikumbukwe kuwa Msumbiji hasa kijiji cha Mkenda mkoani Ruvuma ni muhimu sana kwa ukombozi wake na ndio maana Joaqim Chisano aliitaja Msumbiji kuwa ni muhimili wa ukombozi wa Msumbiji. Pamoja na sisi kuipuuza historia hiyo katika mkoa wetu wa Ruvuma sasa wao watu wa Msumbiji hawa hawapati  ulazima wa kuvuka mpaka kuja Tanzania hasa kutokana na kwamba hakuna mahali pa kuona wapi akina Machel walikuwapo kabla ya kuvuka mipaka na kuingia Msumbiji kuanza kazi ya kuikomboa Msumbiji kwa kumkabili Mreno.

Hali ya eneo hilo haijabughudhiwa ukiiangalia kwa makini, kwani hata mtu wa kawaida ukifika hapo unaweza kabisa ‘kunusa’ kwa kutumia akili uwepo wa majemedari hao wa zamani wakati wakipanga fyeko la kwanza kwa Wareno. Katika mazungumzo  kuelewa siri ya eneo hilo kubaki bado na harufu ya majemedari hao pamoja na miaka mingi kupita, Jalarne alisema  kuwa kinachosaidia eneo hilo kubakia katika hali ya uhalisia ni jinsi  wananchi wa nchi hiyo wanavyoheshimu na kuogopa sheria za nchi hiyo ambazo ni kali. ‘’Sheria zetu ni kali sana katika uhifadhi wa mali asili, tena unaweza kujikuta umehukumiwa kunyongwa kama utabainika kukata miti katika hifadhi kama hizi, ndio maana unaona miti inaanguka yenyewe na hakuna hata mtu wa kukata kuni’’ Alisema Jalarne. 

Aliendelea kusema kuwa Wapigania uhuru wa Msumbiji walifanya mkutano wao wa kwanza Juni 22 hadi 25 mwaka 1962 mkutano wa kujadili jinsi ya kupata uhuru mkutano uliofanyika Jijini Dar es Salaam nchini Tanzania. Na baadae wakaanza mikakati yao mkoani Ruvuma kwa ajili ya ukombozi.

Mtunza makumbusho huyo aliendelea kusema kuwa ilipofika  mwaka 1968 wapigania uhuru wa nchi hiyo walifika katika kijiji cha (Mkenda)   katika mkoa wa Ruvuma na kuweka kambi kabla ya kuingia mkoa wa Congreso Msumbiji kwa ajili ya kufanya mkutano wake wa pili kwa ajili ya kuanza safari ya kwenda kutafuta Uhuru wao nchini Msumbiji. Na ndio maana makala hii nimeipa jina la *”NI SAMORA MOSÉS MACHEL NA SAFARI YA KUTOKA RUVUMA MPAKA MAPUTO”* Kwa mantiki kuwa mkoa wa Ruvuma ni muhimu sana kwa ukombozi wote wa msumbiji. 

Ukiangalia kwa undani zaidi utaona kuwa Eneo la kijiji cha Mkenda kilichopo Ruvuma lingeweza kuwekwa kumbukumbu ya kitaifa kutokana na historia hiyo muhimu kabla Msumbiji haijapata uhuru wake mwaka 1975. Na nimekuwa nikisema kuwa Tanzania kama ingeamua kuwekeza katika *”urithi wa vivutio vya kihistoria”* pekee tunge ingiza fedha nyingi sana za kigeni na kuchangia katika pato la Taifa kwani nchi ya Misri pekee huingiza fedha nyingi sana karibu 40% ya pato lote hutegemea utalii wa urithi wa historia.

Pamoja na Ruvuma kubeba historia kubwa ya nchi jirani na  kujitolea kwa watanzania  kupitia wakazi wake wa kijiji cha Mkenda na maeneo yake ya jirani lakini mpaka leo eneo hili halina hata chembe ya ukubwa wa historia yake katika vichwa vya wapigania uhuru na hata hao alioshiriki katika mapambano hayo. Hata hivyo, historia hiyo ambayo ilistahili kufanyiwa kazi na kuenziwa inakwamba zaidi kutokana na eneo hilo kutoendelezwa kwa namna yeyote . Ukifika eneo hili miundombinu yake ni duni, mawasiliano hakuna jambo linalowalazimu wananchi wa eneo hilo kutumia mtandao wa simu wa nchini msumbiji. 

Mwalimu Salvius Nindi ni miongoni mwa wakazi wa kitongoji cha Mkenda  anasema ni kama vile wako katika kisiwa kutokana na kutokuwa na huduma muhimu kama mawasiliano na miundombinu mibovu hasa ya barabara. Hali hiyo huenda ndiyo inayofanya hata watu kutoka Msumbiji wenye hamu ya kuja kuangalia mwanzo wa harakati hizo kushindwa kufanya hivyo. Kuwepo kwa makumbusho eneo hilo ambayo yanaweza kuungwa na mapambano ya wana Frelimo kumng’oa  Mreno kwa kuunganisha na maeneo mengine kama makazi ya Mondlane  yaliyopo wilaya ya Temeke, Dar es salaam, kambi za kufunza wapiganaji za  Nachingwea huko mkoani Ruvuma. Kwa yamkini kabisa mkoa wa Ruvuma ndipo kitovu cha ukombozi wa Msumbiji.

Kama taifa tulihitaji kuwekeza mkoa wa Ruvuma kwa kuendeleza kumbukumbu ya sisi watanzania kutambua juhudi zetu katika ukombzi wa msumbiji Hali hiyo ingeliwezesha watanzania nao kuuona ushiriki wao katika kumng’oa Mreno. Na kwa kuweka makumbusho na kuboresha miundombinu katika maeneo hayo nchi ingeweza kujipatia pato kubwa la taifa kutokana wananchi wengi wa Msumbiji kufuatilia historia yao ambapo wangelifika Mkenda na maeneo mengine yaliyoungwa katika njia ya mapambano ya uhuru wa Msumbiji. ‘’Kungekuwa na makumbusho ya Taifa hapa serikali ingeweza kupata fedha nyingi, si mnaona mimi  nilijenga nyumba ya kulala wageni na sasa najenga nyumba ya kitalii, kama serikali ingewekeza ingepata pato kubwa’’ alisema Mwalimu huyo. Serekali kupitia kwa Mkuu wa mkoa wa Ruvuma imekuwa ikisema kuwa serikali inafanya jitiada za kuboresha miundombinu katika maeneo yote yenye vivutio vya utalii ili kuweza kuwavutia watalii.

Serikali ilikuwa ikisema kuwa tayari serikali imejenga daraja kubwa la Mkenda linalounganisha nchi hizo mbili lengo likiwa ni kurahisha mawasiliano na pia kuunga udugu wa nchi hizi mbili ulioanzia katika mapambano ya kudai uhuru wa Msumbiji. Pamoja na kukiri kwamba taifa limechelewa sana kufikiria kuunganisha makumbusho ya Msumbiji na Mkenda kwa ajili ya majukumu ya kutoa simulizi la kweli la historia ya maeneo hayo katika kudai Uhuru wa Msumbiji, bado masuala hayo yanaweza kufanyiwa kazi na Makumbusho ya taifa na hivyo kuunga  makumbusho ya Mkenda na yale ya Congresso. 

Na hii ndio umuhimu wa Ruvuma katika historia ya ukombozi wa Msumbiji na ndio maana tukaiita *” Ni Somora Machel na kile kilichoitwa Kutoka Ruvuma mpaka Maputo”*.

“Mungu ibariki Afrika, Mungu ibariki Msumbiji, Mungu baliki Tanzania, Mungu baliki fikra za Waafrika”.