Home Habari Sarwatt mwasisi haki huru ndani ya Bunge la Tanzania huru

Sarwatt mwasisi haki huru ndani ya Bunge la Tanzania huru

997
0
SHARE

NA DK. Albanie Marcossy

Siku moja januari 1944, Herman Sarwatt alimpokea shuleni mwanafunzi kijana mwenziwe kutoka Marangu kwa jina la Edwin Mtei. Alikuwa amefungasha nguo zake na kuzifunga bundu kwenye kilemba cha mama yake, amepakata kwapani.

Edwin, kama alivyojulikana sana baadae shuleni, aliongozana na Mareale Jr mtoto wa Chifu Mareale aliyekuja kuwa shemeji yake baadae. Herman sarwatt na Edwin Mtei walikaa bweni moja namba 14 nyumba ya Kibo.

Walipendana na kuishi pamoja sana ukizingatia mdogo wa Edwin aliitwa Hermas Mtei. Mwaka 1958 Herman Sarwatt alitaka kugombea Ubunge kwa tiketi ya TANU; akashinda kwenye kura za maoni lakini viongozi wa TANU wakamuengua.

Akagombea na kushinda akiwa Mgombea Huru. Alikuwa mwiba sana ndani ya Bunge la Tanganyika.

Aliwaongoza wabunge wengine kama Sheikh Thabit Kombo, Ndugu Mtaki, Ndugu Siyovelwa, Ndugu John Wambura na Ndugu P. Mbogo kutoa woga na kuichachafya serikali na wabunge wa ‘ndiyooooo’ kwa hoja hadi akawa maarufu.

Mwl Nyerere alimpenda Sarwatt na mara kadhaa alimuita Ikulu kushauriana naye.

Ndiye Mbunge huria wa kwanza na pekee hata sasa. Hakuwa ametoka TANU na kwa kuona nguvu na uwezo wake ndani ya Bunge, TANU walimuomba kugombea kwa tikati ya TANU uchaguzi wa 1965.

Baadaye alikuwa Spika wa Bunge la Afrika Mashariki (1974 – 1977) wakati huo rafiki yake Edwin Mtei alikuwa Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Herman Sarwatt na Edwin Mtei waliamini katika uhuru wa mawazo, mijadala ya hoja na mfumo wa haki za kiuchumi katika kujenga jamii iliyo imara na yenye mafanikio.

Herman Sarwatt ndiye alikuwa karibu sana na Edwin Mtei wakati wa mgogoro wake na Mwl Nyerere ulioplekea Edwin Mtei kujiuzuru kama Waziri wa Fedha mwanzoni mwa 1983. Waliungana katika maisha mitaani mjini Arusha.

Baadae Edwin Mtei aliteuliwa kuwa Mkurugenzi wa IMF kwa Afrika kabla ya kuwa Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa IMF.

Akiwa mgonjwa sana na Mzee, Herman Sarwatt alimtembelea rafiki yake Edwin Mteio jijini Washington ambako alilazwa na kufariki akiwa anapatiwa matibabu.

Edwin Mtei alikuwa pembeni ya kitanda cha rafiki yake hata mauti yalipomkuta.

Mjadala wao wa mwisho kabla ya kufariki ulikuwa namna ya kuunda chombo chenye mtazamo chanya kuwaongoza watanzania katika kupambana na umasikini kwa kutumia rasilimali zao na uzoefu wao kwenye uhuru.

Chombo cha kidemokrasia na kinachozingatia haki za binadamu: ndio wazo lililozaa Chama cha Demokrasia na Maendeleo – CHADEMA.

Unataka kujua zaidi?? Jiandae kusoma Kitabu cha *100 Years of the Parliament of Tanzania: Bunge* by Dr. Albanie Marcossy, PhD.

(Coming soon)

Dr. AlbanieMarcossy, PhD pia ameandika Kitabu cha Why is Tanzania poor? Kinapatikana madukani au agiza kupitia 0712417307 kwa Tshs 30,000 tu.