Home Habari Serikali yaandaa agenda ya uwajibikaji wazazi

Serikali yaandaa agenda ya uwajibikaji wazazi

1655
0
SHARE

NA MWANDISHI WETU

UTAFITI wa hali ya ukatili dhidi ya watoto uliofanywa na Wizara ya Afya, Maendleo ya Jamii. Jinsia, Wazee na Watoto kwa kushirikiana na Shirika la Kimataifa linaloshughulikia Watoto (UNICEF) mwaka 2011 unaonyesha kuwa mtoto mmoja kati ya watatu wa kike na mmoja kati ya saba wa kiume walifanyiwa ukatili wa kingonokabla ya kufikia umri wa miaka 18.

Pia asilimia 72 ya wasichana na asilimia 71 ya wavulana walifanyiwa ukatili wa kimwili na vilevile robo ya watoto walifanyiwa ukatili wa kiakili.

Na matokeo hayo yalipekea Tanzania kama mwanachama wa Umoja wa Mataifa na Mwanachama wan chi huru za Afrika kuchukua hatua za kukabiliana na vitendo hivi ambapo Desemba 2016, Seerikali kw a kushirikiana na wadau ilizindua mpango kazi wa kitaifa wa kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto.

Mpango huu ni wamiaka mitano na una maeneo makuu manane ya utekelezaji, mojawapo ya eneo la utekelezaji ambalo ndilo linabeba lengo kuu ni Agenda ya Malezi, kuimarisha mahusiano na kuziwezesha familia.

Ni kupitia eneo hilo la utekelezaji ambapo Wizara imeweza kuandaa ajenda ya kitaifa ya wajibu wa wazazi/ walezi katika malezi na matunzo ya familia ambayo imezinduliwa rasmi Juni 16, mwaka huu na Waziri wa Afya Ummy Mwalimu.

Ni matarajio ya wengi kuwa uandaaji wa ajenda hii itakuwa ni chachu kama siyo mwarobaini wa kutokomeza vitendo vya ukatili katika jamii kwani ni wazi kuwa hali halisi ya sasa inaonyesha kuwapo kwa ongezeko la changamoto zinazomkabili mtoto hasa zinazoania katika ngazi ya familia.

Kwani pamoja na jitihada ambazo zimekuwa zikichukuliwa na Wizara ikiwamo kuelimisha jamii kupitia kuzindua kitini cha elimu ya malezi ya familia cha mwaka 2015 ili kueneza juhudi za kuzuia ukatili dhidi ya watoto lakini bado changamoto imeendelea kuwa kubwa licha ya juhudi nzuri za serikali.

Kwa mujibu wa Katibu Mkuu Wizara ya Afya (Idara kuu ya Maendeleo ya Jamii), Dk. John Kingu, hadi kufikia juni mwaka huu Wizara imefanikiwa kutoa mafunzo kwa halmashauri 132 za Mikoa 17 ambapo jumla ya washiriki 635 walinufaika na mafunzo hayowakiwamo maafisa Maendeleo ya jamii, Ustawi, wanahabarina wlaimu.

Pia anasema kupitia mafunzo hayo, jumla ya Vikundi vya malezi ya kijamii 1,184 vimeundwa.

“Vikundi hivi vinasaidia jamii kushiriki kikamilifu katika malezi ya watoto katika maeneo yao pia wizara imeweza kuratibu uundwaji wa kamati za ulinzi kwa wanawake na watoto katika mikoa 26 halmashauri 176, kata 1,640 na vijijini na mitaa 5,609.

“Hivyo ni matarajio yetu kuwa iwapo kamati hizi zitatumiwa vizuri basi zitasaidia kuwalinda wanawake na watoto na kuwa na jamii iyostarabika na yenye kutoa maadili mema kwa jamii,” anasema Dkt Kingu.

Hata hivyo Dk. Kingu anakiri kuwa kumekuwa na ongezeko la changamoto zinazokabili familia zikiwamo za kukithiri kwa vitendo vya ukatili dhidi ya watoto na wanawake hali ambayo kwa kiasi kikubwa inatokana na kukithiri kwa mmomonyoko wa maadili kwa wanafamilia na kutowajibika kikamilifu kwa wazazi walezi hasa pale inapotokea migogoro ya ndoa.

“Takwimu za wizara ya Afya zinaonyesha kuwa kwa kipindi cha kmiezi tisa kuanzia julai mwaka jana hadi mwachi mwaka huu jumla ya mashauri ya migogoro ya ndoa 16, 832 ilipokelewa ikilinganishw ana mashauri 13, 382 mwaka 2017/18.

“Hivyo ni wazi kuwa migogoro hiyo inaathiri ukuaji wa watoto, ustawi na maeneleo ya familia,” anasema Dkt Kingu.

Anaitaja changamoto nyingine kuwa ni kukosekana kwa usawa wakijinsia katika familia zinazopambana na kuondokana na umaskini hali ambayo imepekea kuongezeka kwa migogoro ya ndoa ambapo mwisho wake wanaoathirika Zaidi ni watoto na vijana waliokatika umri wa balehe ambao hatima yao huwa ni katika kufanya vitendo hatarishi.

“Sababu nyingine ni Kuhamahama kwa wazazi kichumi nako kumesababisha wanafamilia hususan wazazi na walezi kusahau wajibu wao katika familia zilizo mbali naokusambaratika kwa familia na kupelekea changamoto ya ongezeko la watoto wanaoishi na kufanya kazi mitaani.

“Hivyo ni wajibu kwa kina baba ambao wanajikita Zaidi katika kusaka mahitaji ya familia, huku wakiacha jukumu la kulea watoto kwa kina mama na walezi wengine, hivyo wanapaswa kubadilika na kuwekeza muda na kushiriki katika kujishughulisha na malezi ya watoto wao,” anasema.

Hata hivyo ni ukweli uliobayana kuwa matukio na vitendo vya kikatili vinaweza kupungua kama siyo kuisha kabisa iwapo familia kama taasisi muhimu itasimama imara na kutimiza wajibu wake.

“Kwa mujibu wa taarifa ya matokeo ya ukatili za jeshi la polisi kwa mwaka jana matokeo ya ukatili 14,419 ymaeripotiwa kukiwa na ongezeko la asimilia 7.7 ya vitendo vya ukatili kwa watotonchini ukiwamo ubakaji5,557, mimba 2,692, kulawiti 1,159, shambulio965 na kujeruhi 705.

“Na katika ripoti hiyo mikoa kinara ni Tanga 1,039, Mbeya 1,001, Mwanza 809, Arusha 792 na Tabora618 ikilinganishwa na mwkaa 2017 ambapo jumla ya matukio ya ukatili 13,457 yaliripotiwa ikiwamo ukatili wa kingoni 3,583 na mimba za utotoni 1,323,” anasema Dkt Kingu na kuongeza kuwa mikoa ya kipolisi yenye takwimu kubwa za ukatili ni Kinondoni (2,426), Dodoma 1,283, Tanga1,064, Temeke 984 na Arusha 972.

Anasema ujio wa ajenda hiyo ambayo  ni ya kila mtu inalenga kuziwezesha familia zote zilizo katika changamoto na zilizo katika hatari zya kuingia kwenye matatizo ili zipate msaada wa haraka hasa zile zilizoathirika na ukatili.

Nyingine ni zile zilizobaguliwana kujikunyata kwa familia na zile zilizo katika mazingira hatarishi kama vile zilizoathirika na umasikini, maambukizi ya Virusi vya Ukimwi na zenye elimu duni ili zijengewe uwezo wa kutoa malezi bora.

“Agenda hii imejengwa katika nguzo kuu tano amabzo ni matunzo, kulinfa/ulinzi, mawasiliano, upeno na kujenga familia zikihusisha baba, mama na watoa huduma kwa mtoto chini ya miaka 18.

“Serikali itaendelea kushirikiana na wadau waote katika ngazi mbalimbali  ili kuhakikisha kuwa Agenda hii inapokelewa na inatekelezwa kw auzito wake na ujumbe uliobebwa ndani yake ili kumfikia kila mwananchi,” anasema Dkt. Kingu.