Home Makala SIDO KICHOCHEO CHA KWELI CHA UCHUMI WA VIWANDA

SIDO KICHOCHEO CHA KWELI CHA UCHUMI WA VIWANDA

900
0
SHARE

NA SAFINA SARWATT, KILIMANJARO


SHIRIKA la viwanda vidogo vidogo nchini SIDO imekuwa kikocheo kikubwa ya kiuchumi wakati nchi inaelekea katika uchumi wa viwanda.

Ni ukweli usiopingika kwamba SIDO imekuwa kikocheo cha kiuchumi na mkombozi wa wajasiriamali ambao hawana ajira rasmi kutokana na uhaba wa ajira nchini.

Hata hivyo, shirika hilo imechangia kwa kiasi kikubwa kuimarisha uchumi wa wananchi hali ya chini na wa kati kupitia usidikaji wa vyakula na uchakataji bidhaa mbalimbali.

Aidha, SIDO imekuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha uchumi wa nchi unakua licha ya kuwepo na changamoto mbalimbali ya upatikanaji wa soko la uhakika kwa bidhaa zinazotengenezwa na wafanyabiashara wa wadogo wadogo yaani wajasiriamali.

Meneja wa SIDO mkoa wa Kilimanjaro, Hamwel Meena anasema kwamba shirika hilo mkoani Kilimanjaro imekuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha kwamba wanatoa huduma bora kwa wananchi.

“Sisi SIDO kazi yetu kubwa ni kuhudumia viwanda vidogo vidogo hapa nchini na lengo kubwa ni kuchochoa maendeleo katika sekta ya viwanda na kukuza uchumi wa wananchi na taifa,”alisema.

Anasema kuwa asilimia kubwa ya wananchi mkoani humo wanafanya shughuli ndogo ndogo ikiwemo ujasiriamali wa bidhaa mbalimbali tofauti na mikoa mingine.

“Kilimanjaro na Arusha ni miongoni mwa mikoa ambao asilimia kuwa wa wananchi wake ni wabunifu katika biashara ndogo ndogo toauti wa mikoa mingine na hayo ndiyo yamechangia mikoa hiyo kupiga hatua kimaendeleo,”anasema Meena.

Anasema kuwa SIDO imeendelea kuwaelimisha wajasirimali jinsi ya kuboresha bidhaa wanazochakata ili ziwe na ubora unatakiwa katika soko la ndani na nje.

“Wajasiriamali wameendelea kupatiwa elimu juu ya usindikaji wa vyakula pamoja na bidhaa mbalimbali wanazozalisha lengo ni wananchi kujikwamua kiuchumi ,”alisema.

Hata hivyo, anasema kuwa wajasirimali wametakiwa kuwa wabunifu na kujiendeleza kielimu ili kuzalisha bidhaa bora yenye viwango vinavyatakiwa katika soko la ndani na nje, nakuweza kuingia kwenye ushindani wa kibiashara.

“Ili bidhaa zikubaliwe kwenye soko la ndani na nje viwe vimekidhi vyote vya ubora unatakiwa na kwamba lazima wa wajasirimali wanapaswa kuzifuata hatua hizo za ubora pia wanatakiwa wawe wabunifu,”alisema.

Pia aliwataka wajasiriamali kutumia frusa zilizopo katika nchi , ili waweze kujikwamua kiuchumia na kuondokana na umaskini na hali ya utegemezi.

“Sido imekuwa ikiwasaidia wajasiriamali katika kuboresha biashara zao ili waweze kuingia kwenye ushindani wa soko la kimataifa lakini changamoto kubwa ni mwamko mdogo wa wafanyabiashara hao kutokana na shindwa kuboresha biashara,”anasema.

Aidha, anasema Sido imeanzisha utaratibu wa kutoa mikopo ya masharti nafuu kwa wajasiriama lengo ni kuwasaidia kuboresha biashara na kuongeza mitaji itakayowasaidi kufikia malengo makubwa kibiashara.
Akizungumzia maonyesho ya 14 ya kanda ya kaskazini anasema kwamba wanatarajiwa kufanyika Desemba 18 hadi 22 mwaka huu ambayo kikanda yanafanyikia mkoani Kilimanjaro alisema kwamba wanategemea kupata zaidi ya wajasiriamali 300 kutoka mikoa ya Arusha, Tanga na Kilimanjaro .

Anasema kwamba maonyesho ya mwaka huu yatafanyikia mkoani Kilimanjaro na kwamba bidhaa zote zitakazo kuwepo ni zile tu ambazo zinazalishwa na wajasiriamali na siyo bidhaa za uchuuzi.

“Manonyesho ya mwaka huo pia tumewaalika mwenzetu wa nchi jira ya Kenya na Uganda na tunahakika kwamba bidhaa zitakazo kuwepo kwenye maonyesho zimetegenezwa na wajasiriamali wenyewe siyo bidhaa za wachuuzi,” anasema.

Anasema kuwa maonyesho ya mwaka huu yameonyesha kuwa mwamko mkubwa wajasirimali kutokana na kwamba mpaka sasa tayari baadhi yao wameanzakujiandaa kwa ajili ya ushiriki.

“Watu wameshajiandaa kwa maonyesho kwani maonyesho ya mwaka huu ni sawa maonyesho ya kitaifa kutokana idadi hiyo kubwa ya watu tofauti yamaonyesho yaliyopitia,”anasema.

“Mwaka huu tumewapa maelekezo kwamba haitaruhusiwa bidhaa za uchuuzi hivyo yeyote atakaye bainika anabidhaa za kichuuzi hatoruhusiwa kushiriki maonyesho kwani Maonyesho ni kuhamasishaji wa uzalishaji wa bidhaa na siyo kuuza mali ghafi ili kufikia malengo ya nchi ya uchumi wa viwanda,”anasema Meena.

Anasema kawa hili litasaidia kuongeza thamini ya bidhaa badala ya bidhaa kuuza katika mali ghali bdala yake inauzwa bidhaa zilizochatwa na inasaidia kuongeza ajira.