Home KIMATAIFA Silaha za Baolojia,kemikali tishio jipya usalama wa binadamu

Silaha za Baolojia,kemikali tishio jipya usalama wa binadamu

1797
0
SHARE

NA MARKUS MPANGALA

UTAMADUNI wa matumizi silaha za baolojia na kemikali umezidi kushamiri katika nchi mbalimbali kadiri miaka inavyosonga mbele. Matumizi ya silaha za baolojia na kemikali ndiyo mbinu mpya ya kisasa katika uwanja wa mapambano baina ya pande mbili za maadui.

Mwishoni mwa mwaka 2010 majasusi 100 walipelekwa katika nchi za Syria,Malaysia na Salisbury, ambapo kwa miaka 100 utamaduni wa kutumia silaha za baolojia na kemikali ndiyo hatari kubwa inayoukabili ulimwengu kwa sasa.

Hatari hii inaanzia kwenye mataifa makubwa na madogo ambako yanalindwa masilahi yao ya kiulinzi, usalama na uchumi. Mathalani mji mdogo wa Melksham ulipo katika mji Wiltshire unasifika kwa kuzaliwa kiwango kikubwa cha gesi.

Jirani na mji huo kuna kiwanda cha kutengeneza kofia za kuzuia silaha za sumu kwa njia hewa. Biashara ya kofia za kuzuia silaha za sumu ilianza rasmi karne ya 19. Nchi zinazoongoza kununua ni Marekani, Canada, India ikiwa na maana uzalishaji wa silaha za kemikali katika nchi hizo umekuwa wa juu zaidi.

Uchunguzi uliofanywa hivi karibuni na gazeti la The Telegraphy unaonyesha kuwa zama mpya za uzalishaji wa silaha za maangamizi zimeshika kasi kuliko wakati wowote. Silaha ambazo watu wanaweza kutumia kwa njia ya hewa,kushikana mikono au kuguswa sehemu yoyote ya mwili.  

Aimen Dean alikuwa mtengeneza mabomu mahiri wa kundi la kigaidi la Al Qaeda. Lakini kwa upande mwingine alipandikizwa kuwa jasusi wa  Shirika la M16 ndani ya kundi hilo.

Kupitia kitabu chake cha “Nine Lives” anaeleza kuwa kikundi hicho kiliwahi kuandaa mipango ya kutengeneza silaha za kemikali au sumu kwa malengo ya kuziweka kwenye milango mbalimbali ya magari ya kifahari nchini Uingereza.

Baada ya shambulio la kigaidi la Septemba 11 mwaka 2001, Aimen Dean alipata taarifa kuwa Abu Khabab alikuwa Mhandisi wa silaha wa kundi la A Qaeda, ambaye alifanikiwa kuunda silaha za sumu kwa njia hewa na kupanga kuiteka katika barabara ya jiji la New York.

Mpango huo haukutekelezwa.  Hii ina maana hata magaidi  wapo kwenye mipango ya kutengeneza na kutumia silaha za baolojia na kemikali kuwadhuru maelfu watu wasio na hatia. Agosti mwaka 2018 idara ya usalama ya Australia ilifanikiwa kuzuia gesi yenye sumu iliyotegwa na magaidi wa ISIL.

Mwezi huo huo vyombo vya dola nchini Ujerumani vilimtia mbaroni Seif Allah Hammami mwenye umri wa miaka 29 na raia wa Tunisia aliyefanikiwa kutengeneza silaha za sumu aina ya Ricin ambapo awali ilitengenezwa na Marekani wakati wa vita vya kwanza vya dunia. Matumizi ya silaha za kemikali yanakatazwa kwa mujibu wa sheria iliyosainiwa mwaka 1925.

Hatari ya matumizi ya silaha za kemikali ilionekana tena desemba mwaka 2016 nchini Syria ambapo shambulio moja lilisababisha vifo vya watu 1,500.

Tukio jingine lilitokea katika wa ndege wa Kuala Lumpur baada ya sumu aina ya kemikali aina ya VX kutumika katika mauaji ya Kim Jong-nam, ambaye ni kaka wa kiongozi wa Korea kaskazini, Kim Jong-un, baada ya wanawake wawili kupuliza sumu hiyo mwilini mwa Jong-nam.

Machi 4 mwaka 2018 maofisa usalama wa Urusi wanadaiwa kutumia kemikali za sumu ya Novichok dhidi ya jasusi wa Uingereza, Sergei Skripal na binti yake Yulia.

Vipo vifo vingine vya kimya ambavyo vinatokana na matumizi ya silaha za kemikali ya Novichok, ambapo baadhi ya wahanga ni Charlie Rowley (45) na  Dawn Sturgess (44), waliofariki dunia katika eneo la Amesbury, barabara ya kutoka mjini Salisbury, Uingereza.

Silaha nyingine hatari ya kemikali ni Toxic nayo kazi yake ni kama Novichok au VX kuharibu mifumo ya mishipa na fahamu kisha kusababisha kifo. Mfumo mzima wa upumuaji wa mtu mtu anayeshambuliwa kwa kemikali hizo huathirika dnani ya dakika moja tu.

Toxic pia inazalishwa na majeshi mbalimbali duniani kupambana na wapinzani wao. Mashambulizi kwa njia ya silaha za baolojia, kemikali na nyukilia yanaharibu mataifa kwa kasi mno, na kila mmoja linahangaika kutafuta ujuzi wa kumiliki silaha kama hizo. Hii ndio hatari inayozungumzwa na wataalamu kama tishio jipya la uhai wa viumbe hai hususani mwanadamu.