Home Michezo Stars kukataa au kuendeleza unyonge kwa Kenya?

Stars kukataa au kuendeleza unyonge kwa Kenya?

1445
0
SHARE

NA MOHAMED KASSARA

TIMU ya Taifa Tanzania, Taifa Stars leo itashuka dimbani kumenyana na Kenya (Harambee Stars)katika mchezo wa pili wa hatua ya makundi fainali za Mataifa Afrika (Afcon) utakaochezwa Uwanja wa June 30, jijini Cairo, Misri.

Stars itashuka dimbani kuivaa Harambee Stars ikitoka kupokea kichapo cha mabao 2-0 kutoka kwa Senegal katika mchezo wa kwanza wa kundi C, uliochezwa Jumapili iliyopita kwenye Uwanja huo.

Kenya nayo, itaingia uwanjani ikitoka kupokea kichapo cha mabao 2-0 kutoka kwa Algeria, katika mchezo wao wa ufunguzi wa michuano hiyo uliochezwa  Jumapili iliyopita kwenye uwanja huo.

Mchezo huo ni muhimu kwa timu zote mbili, kwani kila mmoja itakuwa ikisaka ushindi ili kuweka hai matuimani ya kufuzu hatua ya 16 bora ya michuano hiyo.

Timu itakayopoteza mchezo huo, itakuwa imeyaaga rasmi mashindano hayo, kwani itasubiri kucheza mechi yake ya mwisho kukamilisha tu ratiba kabla ya kurejea nyumbani.

Mchezo huo utakuwa na ushindi kwa sababu mbili, moja ni kuzikutanisha timu zinafahamiana vema, huku pia zikiwa katika kiwango sawa tofauti na wenzao wawili kwenye kundi lao, Senegal na Algeria.

Pili, kila timu kuhitaji ushindi ili kufufua matumaini yao upya baada ya kuanza vibaya, hivyo makocha wa timu hizo watakuja na mbinu tofauti na zile walizotumia  katika michezo zao za awali.

Hadi sasa timu hizo zimekutana mara 48 katika mechi za mashindano yote, Kenya imeshinda michezo 20, sare 14 na Stars ikishinda 14, Kenya imefunga mabao 62, huku Stars ikifunga mabao 43.

 Mara ya mwisho timu hizo zilikutana mwaka 2017 katika mchezo wa nusu fainali ya Kombe la Afrika Mashariki na Kati (CECAFA) na Kenya kuibuka ushindi wa bao 1-0.

Rekodi za jumla starsVS Harambee

04 Sep 1964 Tanzania 1-0 Kenya Kombe la Afrika Mashariki
26 Sep 1965 Kenya 0-2 Tanzania Kirafiki
07 Oct 1965 Kenya 4-2 Tanzania kirafiki
23 Feb 1967 Kenya 2-0 Tanzania Kombe urafiki Afrika
09 Okt 1967 Kenya 5-3 Tanzania Kombe la CECAFA
05 Jan 1969 Kenya 2-1 Tanzania Kombe urafiki Afrika
15 Feb 1969 Kenya 0-1 Tanzania Kufuzu Afcon
02 Mar 1969 Tanzania1-1 Kenya Kufuzu Afcon
01 Oct 1969 Kenya 0-3 Tanzania Kombe la CECAFA
27 Sep 1970 Tanzania 2-1 Kenya Kombe la CECAFA
27 Sep 1973 Tanzania 2-1 Kenya Kombe la CECAFA
30 Jun 1974 Tanzania 0-0 v Kenya Kombe la CECAFA
07 Nov 1975 Tanzania 2-3 Kenya Kombe la CECAFA
06 Nov 1976 Kenya 1-1 Tanzania Kombe la CECAFA
15 Oct 1978 Tanzania 1-0 Kenya kirafiki
20 Oct 1978 Kenya 0-0 Tanzania kirafiki
03 Nov 1979 Kenya 0-0  Tanzania Kombe la CECAFA
05 Jul 1980 Kenya 3-1 Tanzania Kufuzu Kombe la Dunia
19 Jul 1980 Tanzania 5-0  Kenya Kufuzu Kombe la Dunia
20 Nov 1981 Tanzania 1-0 Kenya Kombe la CECAFA
28 Nov 1981 Kenya 1-0 Tanzania Kombe la CECAFA
18 Nov 1983 Kenya 0-0 Tanzania Kombe la CECAFA
08 Oct 1985 Kenya 3-2 Tanzania Kombe la CECAFA
16 Dec 1987 Kenya 3-2 Tanzania Kombe la CECAFA
10 Nov 1988 Kenya 0-0 Tanzania Kombe la CECAFA
05 Dec 1989 Kenya 2-1 Tanzania Kombe la CECAFA
09 Nov 1991 Tanzania 1-1 Kenya Kirafiki
16 Nov 1991 Tanzania 0-2 Kenya kirafiki
01 Dec 1994 Kenya 0-1 Tanzania Kombe la CECAFA
01 Oct 1997 Tanzania 0-0 Kenya Kirafiki
25 Oct 2000 Kenya 2-0 Tanzania Kombe la Castle Lager
27 Oct 2001 Tanzania 3-1 Kenya Kombe la Castle Lager
11 May 2002 Kenya 1-0 Tanzania kirafiki
18 May 2002 Tanzania 0-5  Kenya kirafiki
30 Nov 2002 Tanzania 1-0 Kenya Kombe la CECAFA
14 Dec 2002 Tanzania 2-3 Kenya Kombe la CECAFA
22 Mar 2003 Kenya 4-0 Tanzania kirafiki
11 Oct 2003 Tanzania 0-0 Kenya Kufuzu kombe la Dunia
15 Nov 2003 Kenya3-0 Tanzania Kufuzu kombe la dunia
30 Sep 2006 Tanzania 0-0  Kenya kirafiki
08 Dec 2007 Tanzania 2-1 Kenya Kombe la CECAFA
11 Jan 2009 Kenya 2-1 Tanzania Kombe la CECAFA
11 Aug 2010 Tanzania 1-1 Kenya kirafiki
23 Nov 2010 Tanzania 1-0 Kenya kirafiki
10 Dec 2013 Tanzania 0-1 Kenya Kombe la CECAFA
29 May 2016 Kenya 1-1 Tanzania kirafiki
11 Dec 2017 Kenya 1-0 Tanzania Kombe la CECAFA