Home Makala TANZANIA IJIFUNZE KUTOKA MOROCCO

TANZANIA IJIFUNZE KUTOKA MOROCCO

406
0
SHARE
Rais John Magufuli akijadiliana jambo na Mfalme wa Morocco, Mohamed VI

NA MOSES NTANDU


Tanzania imekuwa ikiboresha mahusiano yake na nchi mbalimbali duniani ikiwa ni pamoja na kuangalia fursa mbalimbali ambazo zinaweza kuboresha uchumi wa Taifa.

Pamoja na kutembelewa na marais na viongozi mbalimbali kutoka mataifa mengi duniani, hivi karibuni tumeshuhudia Tanzania na Morocco zikiboresha mahusiano yao kwa kasi huku Morocco ikifungua ubalozi wake hapa nchini.

Hali hii imefungua milango ya kushirikiana katika sekta mbalimbali baina ya nchi hizi mbili japo bado Tanzania haijatumia ipasavyo fursa zinazopatikana nchini Morocco, ikiwa ni pamoja na uzoefu na mbinu mbalimbali za kitaalam na wataalam wenyewe.

Pamoja na harakati za kisiana na viongozi wa kisiasa kuwa na mahusiano ya kisiana baina ya nchi na nchi kama sehemu ya uhamasishaji wananchi katika kuboresha hali zao za kiuchumi na mahusiano mbalimbali baina ya nchi na nchi.

Miezi kadhaa iliyopita tulishuhudia Mfalme Mohammed wa 6 wa Morocco akizuru nchini Tanzania na kushuhudia Morocco na Tanzania zikitiliana saini mikataba ya ushirikiano kwenye maeneo zaidi ya 21, mikataba ambayo ilikusudia kuimarisha uhusiano wa nchi hizi mbili.

Mfalme wa 6 wa Morocco alipotembelea Tanzania alishuhudia nchi yake iliingia katika mikataba kadhaa ya maendeleao na Tanzania jambo ambalo ni faida kubwa sana kwa taifa kwani kwa dhima iliyopo sasa ya Tanzania ya viwanda kuna mengi kujifunza ktika kwa taifa hilo ambalo ni miongoni mwa mataifa yaliyopiga hatua kubwa sana katika sekta hiyo ya viwanda barani Afrika.

Suala ambalo ni la msingi sana hapa tunapaswa kuijiuliza je, wafanyabiashara wetu na wajasiriamali wametumia kwa kiwango gani fursa zilizojitokeza katika makubaliano hayo yaliyoingiwa na wakuu wa mataifa haya mawili?

Binafsi naona kuwa kuna dhamira njema na ya kweli kutoka kwa taifa la Morocco kwa Tanzania kwani takribani wiki mbili tatu zilizopita taifa hilo la Morocco lilimtuma Naibu Waziri wao wa Masuala ya Kigeni na mahusiano ya kimataifa Mounia Boucetta kuja nchini Tanzania kufuatilia utekelezaji wa mikataba ambayo wakuu wa mataifa hayo walitiliana miezi kadhaa iliyopita.

Kwa hali hiyo inadhihirisha umakini na dhamira yao safi waliyonayo kwa taifa letu kwani ni nchi ngapi zimeshaingia makubaliano na Tanzania hata kabla ya Morocco lakini hakuna ufuatiliaji wa yale yote waliyokubaliana na kutiliana saini.

Taifa la Morocco lina uzoefu mkubwa sana hasa katika masuala ya nishati ya umeme wa jua na upepo ambapo hadi kufikia mwaka jana 2016 taifa hilo lilikuw alinazalisha nishati ya umeme wa nguvu ya jua 180MW na nishati ya umeme wa upepo 800MW huku ikielezwa kuwa uzalishaji huo utaongezeka hadi kufikia 4000MW kwa maana ya 2000MW kwa nishati ya jua na 2000MW kwa nishati ya upepo kufikia mwa 2020.

Kwa sasa taifa letu lina mahusiano mazuri na taifa hli la Morocco je, tunatumiaje fursa hizi ili nasi tuweze kuchangia kitika harakati ya Tanzania ya viwanda ambapo ndoto hiyo ya Tanzania ya viwanda bila ukakika wa nishati ya umeme haiwezi kutekelezeka.

Fursa za uzalishaji nishati ya umeme wa upepo na jua kwa Tanzania ni kubwa san a rais mno kwani rasilimali hizo tumejaaliwa na Mungu zipo tele upatikanaji wa upepo wa kutosha mikoa ya kati hasa Singida, suala la jua nchini kwetu ni la uhakika.

Hapa suala ni kuunganisha mahitaji yetu na wataalamu na uzoefu kutika kwa nchi kama hii ya Morocco ambayo imefanikiwa sana katika sekta hii kuhimu.

Licha ya kutazama sekta hii ya nishati ya umeme bado kuna sekta nyingi wenzetu haw awa Morocco wamepiga hatua kubwa sana ambapo sisi Tanzania tupo katika hatua za awali kabisa mfano reli ya kisasa taifa hili la Morocco lipo mbele sana na ntunaweza kujifunza mengi toka kwao sio lazima kwenda nje ya bara letu.

Pamoja na mahusiano haya ya nishati nna miundombinu yake pia bado mahusiano ya kisiana baina ya Tanzania na Morocco yanaimarika jambo ambalo linatoa fursa nyingi hasa hata katika masuala ya kielimu na kitabibu.

Katika makubaliano ambayo serikali ya Tanzania ilikubalaina na serikali ya Morocco ni vyema wafanya biashara wa kitanzania na wajasiriamali kutazama fursa zinazojitokeza na kuzifanyia kazi badala ya kusubiri kila lambo kufanywa na serikali kwani serikali zote mbili kwa upande wao zote zilishafungua milango ya fursa hizo.

Fursa hizo zipo wazi kutokana na kile ambacho wakuu wan chi nhizi walikifanya hasa katika sekta ya kiuchumi, kwa kuwa wakuu hao walikubaliana kuimarisha biashara baina ya nchi hizi mbili, hasa katika bidhaa za kilimo, pamoja na kutafuta maeneo zaidi ya uwekezaji ambayo yatazinufaisha nchi zote mbili.

Hili ni jukumu letu wananchi kutumia fursa hizi na kuanza kuzifanyia kazi kwani Tanzania ina mazao na bidhaa mbalimbali zitokanazo na kilimo. Pia Tanznaia iko juu sana katika masuala ya Utalii ambapo kuna muunganiko mzuri sana wa kitalii baina ya nchi yetu na Morocco.

Katika fursa ambazo kwa kiwango kikubwa Tanzania inaweza kunufaika kutoka kwa Morocco ambayo pia ilijadiliwa na wakuu wa nchi hizo mbili ni pamoja na sekta ya uvuvi, madini, mbolea za kilimo, masuala ya bima, elimu na afya, ambapo nchi hizo zilikubaliana kubadilishana wataalamu na kuwezeshana kufikia maelengo endelevu kwa wananchi wake.