Home Habari Teknolojia inavyotumika duniani kusaka kinga dhidi ya coronavirus

Teknolojia inavyotumika duniani kusaka kinga dhidi ya coronavirus

1370
0
SHARE

 NA FREDERICK FUSSI 

WAKATI ambapo maambukizi ya virusi vya corona hapa nchini yakizidi kuongezeka siku hadi siku na kwingineko ulimwenguni, wanasayansi wa tiba na kinga wanaendelea kusaka kinga dhidi ya virusi hivyo vya corona. 

Shirika la Afya Duniani (WHO) ambalo linapokea ruzuku kutoka mataifa yaliyoendelea na kutoka kwa Shirika la Bill and Melinda Gates Foundation, nao pia wanaendelea kufadhili miradi mbalimbali ya watafiti wanaotafuta kinga dhidi ya ugonjwa huu ambao umekuwa tishio la usalama wa ulimwengu. 

Mkurugenzi wa WHO, amenukuliwa na vyombo mbalimbali vya habari akisema kuwa nchi zaidi ya 70 zimeungana na WHO katika majaribio ya kuongeza kasi katika matibabu, wakati taasisi na makampuni karibuni 20 yamejitosa katika harakati za kisayansi kusaka kinga dhidi ya virusi vya corona. 

Mtandao mmoja wa habari za kuaminika RFI, umezitaja baadhi ya kampuni na nchi zilizoko na hatua zinazochukua katika kusaka kinga. Nchini Marekani kampuni kadhaa zimejitosa kusaka kinga. Kampuni hizo ni pamoja na Moderna, hii ni kampuni kubwa ya kinga duniani yenye makao yake makuu katika Jimbo la Massachusetts. 

Aprili 16 mwaka huu, kwa mujibu wa tovuti ya kampuni ya Moderna ( HYPERLINK “https://www.modernatx.com/” https://www.modernatx.com/) wametangaza kuwa wamepokea ruzuku ya Dola za Kimarekani 483 kutoka Serikali ya Marekani kupitia wakala wake BARDA ili liweze kuharakisha utafiti wa kinga dhidi ya virusi vya corona. 

Kampuni ya Moderna inatarajia kuajiri watafiti wapya 150, ambao watasaidia juhudi za kusaka kinga. Kampuni hii inatajwa ulimwenguni kuwa mbele wa kampuni nyinginezo katika bioteknolojia ya kusaka kinga dhidi ya virusi hivyo kama ambavyo teknolojia hiyo imetajwa kuwa ni mRNA-1273.

Katika tovuti yao Moderna wanaendelea kusema kuwa bioteknolojia ya mRNA-1273, imeonesha matumaini katika majaribio ya kitabibu zaidi ya 1,000 yaliyowahi kufanyika miaka ya nyuma dhidi ya aina nyingine ya virusi vinavyoambukizwa kwa njia ya mfumo wa hewa kama vile mlipuko wa homa za mafua za RSV, hmPV na PIV3. 

Wanadai kuwa miaka minne iliyopita walifanya majaribio ya kitabibu takribani tisa juu ya kinga za mRNA. Katika tovuti yao pia Moderna wametaja washirika mbalimbali wanaoshirikiana nao katika kazi zao za kusaka kinga mbalimbali, washirika wao wakubwa wanaowapatia ruzuku za utafiti wa kinga ni pamoja na shirika la Bill and Melinda Gates Foundation. 

Shirika hili la Bill and Melinda Gates Foundation linalomilikiwa na Mwanzilishi wa Kampuni ya kuzalisha kompyuta duniani Bill Gates, Januari mwaka 2016 liliingia makubaliano na Kampuni ya Moderna katika kuendeleza bioteknolojia ya kinga ya mRNA ili kukabiliana na mlipuko wa magonjwa mbalimbali yanayoambukizwa, kwa mfano Bill and Melinda Gates Foundation, iliwapa kampuni ya Moderna ruzuku ya Dola za Kimarekani milioni 20 ili kuzalisha kingamwili (antibody) zinazosaidia kupunguza makali vya virusi vinavyosababisha upungufu wa kinga mwilini maarufu Ukimwi. 

Tovuti hiyo ya Moderna katika ukurasa wake wa habari imeendelea kutoa taarifa kuwa Shirika la Bill and Melinda Gates Foundation limekusudia kutoa fedha zaidi hadi kufikia Dola za Kimarekani milioni 100 ili kukabiliana na magonjwa ya mlipuko katika kusaka kinga. 

Hivyo March 16 mwaka huu, kampuni hii ya Moderna ilitangaza kuanza majaribio ya kitabibu ya kinga dhidi ya virusi vya corona ambapo walifanya majaribio kwa wagonjwa wenye afya 45 na wanatarajia kuendelea na majaribio huku wakitazamia kuwa majaribio yanaweza kukamilika ndani ya miezi 12 mpaka 18 ili kuthibitisha uimara wa kinga hiyo endapo inafanya kazi ipasavyo. 

Kampuni nyingine inayofanya utafiti wa virusi vya corona inayotajwa kwenye tovuti ya RFI ni pamoja na kampuni za Gilead Sciences na Inovio Pharmaceuticals zote ni kampuni za nchini Marekani, CureVac ya nchini Ujerumani, Pasteur Institute, Sanofi na IHU – Institut hospitalo-universitaire zote za nchini Ufaransa, Clover Biopharmaceuticals ya nchini China, na Fujifilm Biotechnologies ya nchini Japan. 

Nchini Marekani Jaridi la habari za Kibiashara ‘Wall Street Journal’ limeripoti kuwa Serikali ya Marekani na Kampuni kubwa ya Kompyuta ya IBM (International Business Machines Corp) na wameanza kutoa ruhusa kwa watafiti wa kinga dhidi ya corona duniani kutumia kompyuta zenye uwezo mkuu yaani ‘Supercomputers” takrabani 16 ili kuharakisha kazi ya kuchambua taarifa na takwimu mbalimbali zinazotokana na utatifi wa kinga ya virusi vya corona. 

Machi 28 mwaka huu, watafiti mbalimbali wanaweza kuwasilisha takwimu za miradi yao ya utafiti katika tovuti ya  HYPERLINK “http://www.xsede.org” www.xsede.org ili kujiunga na muungano wa utafiti wa kinga dhidi ya coronavirus uitwao “COVID-19 HPC Consortium” tovuti hiyo imetoa maelekezo kwa wanasayansi na watafiti wote wanaotaka kutumia ‘supercomputers’ kufanya utafiti kwa kuainisha mambo manne katika maombi yako ikiwemo mahitaji yao ya kisayansi au kitaalamu, kiasi cha uwezo wa kompyuta wanachotarajia kutumia pamoja na uwezo wa kutunza kumbukumbu wanaoutaka, mahitaji yao ya kiufundi na kuainisha majina, weledi, elimu na timu ya watafiti wanaohusika katika utafiti huo. 

Kwanini Kompyuta zenye uwezo mkuu yaani supercomputers zinatumika kutafuta kinga? Profesa wa Chuo Kikuu Kishiriki cha London (University College London), Profesa  HYPERLINK “https://www.ucl.ac.uk/quantum/people/prof-peter-coveney” \t “_blank” Peter Coveney amenukuliwa na mtandao wa Science focus akisema kuwa “kwa kawaida makampuni ya kuzalisha kinga dhidi ya magonjwa huchukua muda wa miaka 12 na takribani Dola za Kimarekani bilioni mbili kuzalisha dawa ya aina moja na kuiingiza kwenye soko, lakini wanaandika upya kanuni zao kwa kutumia uwezo mkuu wa kompyuta kutatufa kinga na dawa katika muda mfupi na kuokoa gharama”.

Kwa kawaida dawa au kinga huwa zinapewa kwa mgonjwa ama kwa njia ya kumeza kidonge au kwa njia ya kuchomwa sindano. Sasa Teknolojia duniani imeendelea sana na kuna mabadiliko makubwa sana yametokea katika bioteknolojia ya kuwapa dawa wagonjwa. 

Chuo kikuu cha Teknolojia nchini Marekani cha Massachusetts yaani ‘Massachusetts Institute of Technology’ katika tovuti yao wameripoti kutengeneza bioteknolojia ya sindano isiyoonekana kwa macho mpaka ikuzwe na vifaa vya kukuzia yaani ‘microneedle”. 

Katika Mtandao wake Shirika la Bill and Melinda Gates foundation limetaja matumizi ya ‘microneedle’ katika kinga dhidi ya Polio katika hatua za majaribio na matumizi ya ‘microneedle’ katika kuchukulia sampuli za damu kwa ajili ya kutafiti magonjwa. 

Sindano hizo ndogo sana haziumi endapo mtu akichomwa nazo. ‘Massachusetts Institute of Technology’ katika tovuti yao ya http://news.mit.edu wamesema kuwa mwaka 2019 sindano hizo zilifanyiwa majaribio kwa nguruwe kwa kuwachoma dawa za inshulini. Mtandao wa  HYPERLINK “https://www.prnewswire.com/” https://www.prnewswire.com/ uliripoti kuwa mwaka 2017 Shirika la Bill and Melinda Gates foundation lilitoa ruzuku ya dola milioni 6 kwa kampuni ya Vaxess Technologies ili wafanye uzalishaji wa ‘microneedle’ hizo kwa ajili ya kinga dhidi ya Polio. 

Wadadisi mbalimbali wa mambo wametaja uwepo wa makusudio ya matumizi ya sindano hizo za “microneedle” katika kufanikisha matarajio ya kufikisha kinga ya virusi vipya vya corona maeneo yote ulimwenguni endapo kinga ya ugonjwa huo itapatikana. 

Mmoja wa wadadisi hao ni Robert F. Kennedy Jr, ambaye ni mwanasheria wa mazingira ni mpwa wa aliyekuwa Rais wa Marekani John F. Kennedy, amejitokeza kwenye ukurasa wake wa mtandao wa Instagram akidadi matamanio ya tajiri Bill Gates katika kutaka kumiliki biashara ya kinga duniani. Akisema kuwa Bill Gates ndio mtu wa pili kutoa fedha nyingi za ruzuku wa Shirika la Afya duniani baada ya nchi ya Marekani. 

Katika majibu yake Robert kwa mwandishi wa habari wa jarida la New York Times, aliyoyachapisha katika ukurasa wake wa Instagram, Robert anadai kuwa “Bill na Melinda kupitia shirikal lao wamewekeza dola zaidi ya milioni 21 katika kutengeneza teknolojia ya sindano isiyoonekana kwa macho yaani microneedle” ambayo mtu anachomwa chini ya ngozi ikiwa na rekodi za uwepo wa kinga, ambazo zinaweza kusomwa kupitia mwanga wa infrared kupitia teknolojia ya simu ya mkononi, huku akidai kuwa nchini humo Marekani teknolojia hiyo itawapa nguvu watumishi wa afya kumtambua mtu endepo amechomwa sindano hiyo ya kinga.