Home Makala Kimataifa TEKNOLOJIA ‘INAYOWATAMBUA’ WAPENZI WA JINSIA MOJA YAJA

TEKNOLOJIA ‘INAYOWATAMBUA’ WAPENZI WA JINSIA MOJA YAJA

1906
0
SHARE

Utafiti ambao unafanyia majaribio teknolojia inayodaiwa kuwa na uwezo wa kutofautisha watu wapenzi wa kawaida na wapenzi wa jinsia moja umezua mzozo mkali kati ya waliotayarisha teknolojia hiyo na watetezi wa haki za wapenzi wa jinsia moja.

Watafiti hao kutoka Chuo Kikuu cha Stanford nchini Marekani wanadai kwamba wameunda programu ya kompyuta ambayo inaweza kuangalia uso wa mtu na maumbile yake na kutofautisha kati ya wapenzi wa jinsia moja na wapenzi wengine.

Programu hiyo inaweza kutambua mambo ambayo mtu wa kawaida hawezi kuyabaini, wanasema.

Lakini watetezi wa haki za mashoga wameshutumu utafiti huo na kusema ni “hatari” na “sayansi isiyo na manufaa”.

Lakini wanasayansi wanaohusika wamesema wanaopinga programu hiyo hawajaielewa vyema.

Maelezo ya kina kuhusu mradi huo yatachapishwa katika jarida moja kuhusu sifa za watu na saikolojia ya kijamii.

Gari la mwendo wa kasi zaidi duniani laanza majaribio

Gari lililoundiwa nchini Uingereza linaloweza kukimbia kasi ya kilomita 1,610 kwa saa, linafanyiwa majaribio yake ya kwanza huko Cornwall.

Bloodhound SSC linafanya mikimbio ya mwendo wa chini ya hadi kilomita 320 kwa saa katika uwanja wa ndege wa Newquay.

Likiendeshwa na Andy Green, gari hilo linalenga kuvunja rekodi ya dunia ya mwendo wa kasi zaidi ardhini.

Jaribio hilo litafanywa kwenye barabara maalum iliyojengwa eneo la Nothern Cape nchini Afrika Kusini.

“Tumeunda gari lisilo la kawaida kabisa, lenye uwezo mkubwa na kasi ya juu zaidi katika historia.” Andy Green aliambia BBC.

Kampuni kutumia 3D kuunda nywele

Kampuni moja nchini Ufaransa imesema kwamba teknolojia sawa na ile inayotumiwa kupiga chapa vitu vya uhalisia, 3D, huenda ikatumiwa kuunda nywele za binadamu na hivyo kufaa wenye upara.

Nywele hizo baadaye zitaweza kupandikizwa kwenye watu waliopoteza nywele.

Kampuni ya L’Oreal inashirikiana na kampuni ya kupiga chapa viumbe hai ya Poietis, ambayo imeunda teknolojia ya kupiga chapa kwa kutumia laser ambayo inaweza kuunda sehemu za seli za viumbe.

Vinyweleo vya nywele havijawahi kuundwa kwa njia hii awali lakini kampuni hizo mbili zinatarajia kwamba zitaweza kustawisha teknolojia na kuwezesha kuundwa kwa vinyweleo hivyo katika kipindi cha miaka mitatu ijayo.

Hata hivyo, shirika moja linaloangazia watu wanaopoteza nywele limesema bado ni mapema mno kwa watu kuanza kushangilia.

L’Oreal tayari hutumia ngozi iliyoundwa kwa teknolojia ya 3D kufanyia utafiti bidhaa za kutumiwa kwenye ngozi.

Kiti cha gari chenye uwezo wa kutambua jasho

Nissan imeuzindua kiti cha gari chenye uwezo wa katambua jasho la binadamu ambacho kampuni hiyo inasema kuwa kitasaidia kupunguza ajali za barabarani.

Teknolojia hiyo inayojulikana kama Soak, hubadlisha rangi ikiwa itatambua kuwa dereva atakuwa ameishiwa maji mwilini.

Utafiti wa walia uliofanywa na taasisi za European Hydration Institute na Loughborough University uligundua kuwa madereva wanaoishiwa na maji mwilini huwa na makosa mengi sawa na madereva walevi.

Ngozi hiyo ya kiti iliyoundwa na kampuni moja nchini Uholanzi pia itawekwa kwenye usukani wa gari na viti vya mbele vya gari

“Hii ni sehemu ya mpango mzima ambao sio tu wa kufuatilia tu gari bali pia dereva.” alisema Prof Peter Wells.