Home KIMATAIFA Trump agoma kuhojiwa na Bunge

Trump agoma kuhojiwa na Bunge

2478
0
SHARE

NA MITANDAO

Kati ya jumla ya hati za wito (subpoenas) tisa ambazo Kamati za Bunge la Baraza la Wawakilishi la Marekani zilimpelekea Rais Donald Trump kuhudhuria kwa ajili ya kuhojiwa, rais huyo amezipinga karibu zote.

Rais Trump aliwaambia waandishi wa habari nje ya Ikulu ya nchi hiyo (Whitehouse) kwamba anazipinga hati zote za wito kutokana na haki yake kikatiba.

 HYPERLINK “https://marjoriecohn.com/national-lawyers-guild-calls-on-boalt-hall-to-dismiss-law-professor-john-yoo-whose-torture-memos-led-to-commission-of-war-crimes/” John Yoo, mtaalamu mmoja nchini humo wa masuala ya mamlaka ya Rais (Presidential Powers) alisema wiki iliyopita: “Kitu ambacho si cha kawaida ni kuzipinga kwake kiujumla hati zote hizo za wito. Analifanya Bunge la Marekani kama ni Wachina au chama cha wafanyakazi wanaojenga moja ya majengo ya yake.” 

Tarehe 2 May, baada ya William Barr, Mwanasheria Mkuu wa Marekani kuhudhuria kikao cha Kamati ya Senate ya masuala ya sheria (Senate Judiciary Committee) alikataa wito wa kuhudhuria kikao kama hicho cha Bunge la chini la Baraza la Wawakilishi (House of Representatives).

Baadaye May 9 Kamati ya Bunge ya masuala ya usalama wa taifa (House Intelligence Committee) ilitoa hati ya wito kwa Barr kumtaka aitoe Ripoti ya Robert Mueller, kama Mwanasheria Maalum kuhusu uchunguzi wa uingiliaji wa Urusi katika uchaguzi mkuu wa nchi hiyo wa 2016.

Machi 22 mwaka huu Mueller alitoa ripoti yake kwa Mwanasheria Mkuu William Barr, ripoti ambayo Baraza la Wawakilishi linataka kuiona kwa ukamili wake kwani wanahisi kuna ushahidi unaofichwa, kwamba Trump, au watu wake wa karibu wanahusika katika kashfa hiyo kuhusu Urusi, na kwamba mamlaka za nchi hiyo zilimsaidia Trump kumshinda Hillary Clinton katika uchaguzi ule.

Na Trump alikwenda mbali zaidi. Baada ya Kamati ya Baraza la wawakilishi ilipotoa hati ya wito kwa mwanasheria wa zamani wa Ikulu ya Marekani Don Mcgahn kutoa ushahidi pamoja na hati, Trump alimkataza asiende, akitaja haki ya upendeleo (executive privilege) aliyokuwa nayo rais.

Wakati huo huo, kamati za mabunge yote mawili (Baraza la Wawakilishi na Senate) ya masuala ya sheria zimetoa hati za wito kuhojiwa kwa Robert Mueller.

Wajumbe 19 wa chama cha Democratic ambao wamo katika Kamati ya Senate ya masuala ya sheria waliandika barua kwa mwenyekiti wa kamati hiyo Lindsey Graham, wakimuomba kwamba kamati hiyo imhoji Mueller. Walitaja maswali 60 ambayo yana utata kuhusu ripoti yake na wangependa kumuuliza Mueller. Barr, Mwanasheria Mkuu alisema hana pingamizi kwa Mueller kuhojiwa na kamati hiyo.

Lakini hapo hapo Trump aliandika ujumbe katika akaunti yake ya Twitter akisema Mueller hatatoa ushahidi kwa kamati hiyo, anamuachia Mwanasheria wake Mkuu (Barr) kazi ya kutoa maamuzi kuhusu suala hilo.

Takriban waendesha mashitaka 800 wa serikali kuu kutoka vyama vyote viwili walitia saini andiko likisema kwamba ingekuwa siyo msimamo wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu kwamba Rais aliye madarakani hawezi kushitakiwa, Trump alikuwa ni mtu wa kushitakiwa kwani anazo tuhuma kadha dhidi yake za kumfanya apande kizimbani bila wasiwasi wowote. Tuhuma kubwa ni kuzuia haki isitendeke.

Aidha jumla wa Wamarekani milioni 10 wametia saini ombi (petition) la wito kwa Baraza la Wawakilishi kuanzisha mchakato wa kumshitaki Rais Trump (impeachment procedures).

Baraza la Wawakilishi ambalo linadhibitiwa na chama cha upinzani cha Democratic lina kura tosha za kumuona Trump mwenye hatia. Baada ya hapo suala linapelekwa Senate kwa ajili ya kesi yenyewe (trial) ambapo theluthi mbili ya Maseneta lazima wakubali kumtia Trump hatiani na kumuondoa madarakani. Hilo ni vigumu kufanyika kwa sababu Senate iko chini ya udhibiti wa chama tawala cha Republican.