Home Habari TUCTA yaimwagia pongezi OSHA

TUCTA yaimwagia pongezi OSHA

952
0
SHARE

Na MwandishiWetu

Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi (TUCTA) limeeleza kuridhishwa kwake na utendaji wa Wakalawa Usalama na Afya Mahali pa Kazi (OSHA) katika kusimamia utekelezaji wa Sheria ya Usalama na Afya Mahali pa Kazi ya mwaka 2003.

Kauli hiyo imetolewa na Katibu Mkuu wa shirikisho hilo, Dkt. Yahya Msigwa, katika salamu zake alizozituma kwa OSHA hivi karibuni baada ya kuhitimishwa kwa shughuli mbalimbali za maadhimisho ya sikukuu ya wafanyakazi (Mei Mosi) pamoja na maadhimisho ya siku ya Usalama na Afya mahali pa kazi duniani.

“Wafanyakazi wa Tanzania tunajivunia kuwa nanyi kwa usalama wa afya zetu, ulinzi na maelekezo. Tunawashukuru sana kwa kuwajirani nasi, kutufanyia maonesho kutuelimisha juu ya usalama mahala pa kazi,” ameeleza Dkt.Msigwa katika salamu zake alizomtumia Mtendaji Mkuuwa OSHA.

Aidha, Katibu Mkuu huyo ameupongeza uongozi wa OSHA kwa maandalizi mazuri ya maadhimisho ya siku ya Usalama na Afya mahali pa kazi duniani pamoja na ushiriki wao mzuri katika shereheza Mei Mosi zilizofanyika kitaifa mkoani Mbeya.

“Kwa niaba ya uongozi mzima wa TUCTA na kwa niaba ya wafanyakazi wote nchini, nachukua nafasi hii adhimu kabisa kukupongeza kwa dhati wewe binafsi, Mwenyekiti wa Bodi na uongozi mzima wa OSHA kwa maandalizi mazuri ya wiki ya Usalama,” alisema Mtendaji huyowa TUCTA.

Hata hivyo alitoa wito kwa uongozi wa OSHA kuendeleza jitihada za kumlinda mfanyakazi dhidi ya magonjwa, ajali na vifo vinavyoweza kusababishwa na mazingira ya kazi yasiyozingatia viwango stahiki vya kiusalama na afya.

OSHA ni Wakala chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Ajira, Vijana na wenye Ulemavu) wenye dhamana ya kusimamia utekelezaji wa Sheria Na. 5 ya Usalama na Afya Mahali pa Kazi ya mwaka 2003. Wakala huu ndio huratibu maadhimisho ya siku ya Usalama na Afya mahali pa Kazi duniani kwa hapa nchini ambayo huadhimishwa Aprili 28 ya kila mwa