Home Habari Tukiacha siasa tunaweza kutunza mazingira

Tukiacha siasa tunaweza kutunza mazingira

2122
0
SHARE

NETHO C. SICHALI

UTAFITI uliofanywa na jarida kubwa duniani la The Economist ambao ulitengeneza kitabu cha “Megachange: The World in 2050” unasema ifikapo mwaka 2050 dunia itakuwa kwenye mapambano makubwa ya maji.

Hii ina maana kiwango cha maji kitakwua kidogo lakini mahitaji ya watu yatakuwa makubwa kuliko uwezo.

Uafiti huo unaeleza kuwa bara la Afrika litakuwa na idadi kubwa ya watu pamoja na mataifa kama Nigeria kuwa na idadi kubwa kuliko Marekani.

Utafiti huo unaongelea suala la maji ambalo moja kwa moja linagusa maisha yetu kwenye mabadiliko tabia nchi na mazingira.

Eneo la mazingira ni muhimu katika ukuaji wa uchumi pamoja na kulinda anga la dunia yetu.

Njia mojawapo ni kuhakikisha upandaji wa kti linakuwa suala mtambuka kwa kila kaya. Suala ambalo ambalo linatakiwa kupigwai upatu kwa kiasi kikubwa. Kama dunia itakuwa na uhaba wa maji ifikapo mwaka 2020 maana yake upandaji w amity unatakiwa kufanyika kwa kiwango kikubwa.

Nasema hilo nikiwa mmoja watu wanaosisitiza matumizi bora ya mazingira. Nasisitiza namna ya kulinda mazingira huku nikishiriki moja kw amoja kwenye masuala hayo.

Hivi karibuni wilaya ya Nyasa iliyopo mkoani Ruvuma imeridhia kuongeza eneo la upandaji miti ya kibiashara kutoka hekari 3,905 hadi 20000 katika Kata ya Mpepo na Liparamba ili kupunguza utegemezi wa misitu ya asili na kuongeza chanzo cha mapato ya serikali, kulinda vyanzo vya maji na mazingira kwa ujumla.

Akizungumza wakati wa makubaliano hayo, Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa, Dougras Ruambo wakati akiwasilisha taarifa ya upandaji miti ya kibiashara aliyoitoa wakati wa kikao cha kamati ya ushauri cha Wilaya ya Nyasa kilichofanyika hivi karibuni katika Ukumbi wa Kapteni John Komba Mbamba-bay Wilayani Nyasa alisema kuna miradi miwili ya upandaji miti ambayo ina manufaa makubwa kwa jamii na taifa.

Miradi hiyo ni shamba la Mpepo linalosimamiwa na Wakala wa Huduma za Misitu (TFS) na mradi wa upandaji miti wa watu binafsi unaofadhiliwa na Serikali ya Finland kwa kushirikiana na Serikali ya Tanzania kupitia mradi wa panda miti kibiashara na lengo la mradi huu ni kutekeleza sera ya misitu ya mwaka 1998 lenye dhumuni la usimamizi wa misitu na upatikanaji endelevu wa mazao na huduma za misitu.

Mkurugenzi Ruambo aliongeza kuwa shamba la miti la Mpepo lina ukubwa wa hekta 3905, katika kuboresha usimamizi shamba limegawanyika katika sehemu tatu ambazo ni mapera (ipo katika kijiji cha Mtetema) likiwa na ukubwa wa hekta (815) sehemu ya kizota (ipo katika vijiji vya kihulunga, Mtetema na Lunyele) yenye ukubwa wa hekta 2728 na sehemu ya Ndondo ina ukubwa wa hekari 362.

Aliongeza kuwa ili kutimiza ufanisi wa madhumuni ya uanzishwaji  shamba na uwekezaji wa Serikali wenye tija, lengo ni kufikia ukubwa wa hekari 20,000 hivyo juhudi kubwa ya pamoja inahitajika ili kufikia malengo haya.

Aidha kwa mwaka wa fedha 2017/2018 serikali kupitia TFS ilitenga fedha na kupanda miti na mpaka sasa jumla ya miti 222,200 sawa na hekta 200, aliitaja miti iliyopandwa ni aina ya misindano, pinusna, pinus, telcunumanii, patula miti hii imepandwa katika kijiji cha sehemu ya mapera iliyopo kijiji cha Mtetema.

Hata hivyo katika mpango kazi wa shamba wa mwaka 2018/2019 TFS imepanga kupanda hekta 300 za miti aina ya misindano (pines). Hekta hizi zipo kijiji cha Mtetema (200) na kijiji cha Mpepo (100) ili kufanikisha mpango huu tayari eneo hili limeandaliwa na hatua ya upandaji zimeanza hivyo upandaji huu utakamilika katika msimu huu wa mvua na hivyo jumla ya hekta 500 za miti ya pine zitakuwa zimepandwa.

Wakala wa huduma za misitu Tanzania kupitia shamba la miti Mpepo umekuwa mstari wa mbele katika kuchangia huduma za jamii katika maeneo yanayozunguka shamba la miti Mpepo.

Aliyataja mafanikio hayo kwa ni umeboresha Miundombinu ya barabara na umetoa mabomba rola 17 na bati 60 kwa ajili ya kijiji cha Mtetema na umetoa saruji mifuko 60  kwa ajili ya kijiji cha Kihulunga.

Aliitaja michango mingine ni viriba kilo 40 mbegu za miti kilo 42 aina ya misindano na mikaratusi kwa ajili ya vijiji vya Lunyere, Kihurunga, Mtetema na Mpepo na Wilaya ya Mbinga.

Utaalamu wa kuitunza miti hiyo unaendelea na wananchi wanaoishi kuzunguka eneo la upandaji miti wananufaika na ajira.

Kama nilivyotangulia kusema, tukiacha siasa tunaweza kuyalinda mazingira yetu kwa ufasaha. Kwa sababu mara nyingi amsuala ya kulinda mazingira yamekumbana na matukio mengi ya kisiasa.

Wananchi huwa wanavamia maeneo ya hifadhi, hali ambayo inawalazimu wenye mamlaka kuwaondoa kinguvu. Tukishafika hapo utaona wananchi nao hawakubali kuhama kwakuwa wamezoea kujitwalia maeneo bila idhini. Mwishowe wanasiasa wanaingilia kati kwa kigezo cha kuwalinda wapiga kura wao ili kuhakikisha wanalinda sifa zao za kisiasa.

Sikatazi wanasiasa kuwalind awapiga kura wao, lakini inafaa kuwaelimisha kuwa mazingira wanayovamia na kuyaharibu yanasababisha matatizo kwao moja kwa moja.

Kwa mfano, kama wananchi wakiachwa waharibu vyanzo vya maji, kukata miti, kuvamia mapori ya hifadhi au kuvuna wanyama bila kuzingatia athari za mazingira ni kigezo cha kwanza ambacho kinatuingiza kwenye siasa.

Ili kuepukana na siasa ni muhimu kuzingatia ushauri wa wataalamu kuwa mazingira ni sehemu ya uhai wa mwanadamu. Mazingira yanapokuwa bora yanachochea kuibuka kwa jamii bora na kuwalinda.

Kama tutaharibu mazingira leo, kisha tukajikuta mwak 2050 tunakabiliwa na uhaba wa maji, tutafanya nini? Jawabu hapa ni kwamba makosa yameshafanyika ya kuharibu mazingira ambayo ni ukataji hovyo wa miti, uharibifu vyanzo vya maji ambavyo husababisha kunyauka mito na kukosa maji.

Nimalize kwa kusema, pamoja na kupanga miradi mingi ya kupanda miti, bila kuchukua hatua stahiki ya kulinda mambo niliyotaja hapo juu bila shaka tutakuwa tumejiwekea njia nzuri ya kuangamia.

Misitu ni uhai. Tutumie vizuri sera, elimu sheria na kanuni zetu kuhakikisha tunaondoa migogoro ya namna yoyote y mazingira nchini ili kujihakikishia taifa lenye usalama wa maji,  chakula na hewa safi.