Home Makala BAYPORT: Tumedhamiria kuwakwamua Watanzania kwa fursa za mikopo

BAYPORT: Tumedhamiria kuwakwamua Watanzania kwa fursa za mikopo

1106
0
SHARE

NA GABRIEL MUSHI

NI dhahiri kuwa uwapo wa taasisi mbalimbali zinazotoa mikopo nchini, umechangia Watanzania kupiga hatua kimaendeleo kutokana na baadhi ya taasisi hizo kuwawezesha kukopa kwa riba nafuu na kutekeleza majukumu yenye tija kwa ustawi wa familia.

Hata hivyo, kumekuwapo na changamoto mbalimbali kutoka kwa taasisi hizo ambazo baadhi hazidumu kutokana na usimamizi finyu na thabiti wa kifedha kwa kuzingatia kuwa biashara ya mikopo inahitaji umakini yakinifu.

Licha ya uwepo wa hali ngumu katika mzunguko wa kifedha miongoni mwa Watanzania tangu uongozi wa awamu ya tano kuingi madarakani, baadhi ya taasisi ambazo sasa ziweza kuvuka kihunzi hicho na sasa zimewafikia Watanzania wengi ni Taasisi ya Kifedha ya Bayport Financial Services, ambayo Novemba 9 mwaka huu, iliadhimisha sherehe ya kutimiza miaka 10 tangu walipoanza kutoa huduma za mikopo ya fedha nchini.

Tasisi hiyo ambayo imeshawafikia Watanzania zaidi ya 60,000 imekuwa mkombozi kwa wananchi wa kada mbalimbali bila kubagua aina ya ajira ya mkopaji jambo ambalo limekuwa likiwaongezea ufanisi.

Akizungumzia miaka 10 ya taasisi hiyo, Mkurugenzi Mkuu wa Bayport Financial Services, John Mbaga, anasema ni dhahiri kuwa wamepiga hatua kubwa katika sekta ya mikopo kutokana na utendaji bora wenye dhamira ya kuwakomboa Watanzania kwa kupitia mikopo.

“Tangu mwaka 2006 tumeweza kuhudumia wateja zaidi ya 60,000 wakipata huduma zetu kwa kupitia matawi zaidi ya 80 ambayo tunayo katika wilaya na mikoa ya Tanzania Bara, bila kusahau mawakala wetu zaidi ya 1000 walioenea nchini.

“Hii inaifanya Bayport iendelee kupiga hatua kubwa na hakika tunajivunia kuaminiwa kwa kiasi kikubwa na wateja wetu pamoja na Watanzania kwa ujumla, ambapo ukiacha Tanzania, Taasisi hii pia inahudumia katika nchi za Zambia, Uganda, Ghana, Botswana, South Africa, Mozambique, Colombia na Mexico,” Anasema Mbaga.

Mbaga anasema kwamba huduma zinazotolewa na taasisi yao ni pamoja na mikopo ya fedha taslimu kwa watumishi wa umma na wafanyakazi wa kampuni binafsi zilizoidhinishwa ambapo mikopo hiyo haina amana wala dhamana kwa kila mtu mwenye sifa ya kupata huduma kwao.

Anasema huduma nyingine ni pamoja na mikopo ya viwanja vyenye hati katika maeneo ya Kibaha, Bagamoyo, Kilwa, Kigamboni ambapo huduma hiyo inahusisha watu wote wakiwamo watumishi wa umma na wajasiriamali waliokuwa wakiachwa nyuma katika fursa mbalimbali za mikopo.

Anasema huduma hizo ni nafuu kwa sababu zimeanzishwa ili kuwakomboa wananchi katika suala zima la kumiliki ardhi inayopanda thamani siku hadi siku, huku gharama za maisha zikishika kasi, hivyo kuwafanya wananchi waishi kwa kubangaiza bila kuijua kesho yao.

“Huduma zetu nyingine tunazotoa ni pamoja na Bima ya Elimu kwa Uwapendao, mikopo ya bidhaa na ‘Nipe Boost’ ambapo mteja wetu anaweza kujisajili na kuanza kukopeshwa kwa kupitia simu yake ya mkononi.

“Huduma ya Nipe Boost ni nafuu na haraka mno kwa sababu mtu anaweza kukopa kiasi kisichozidi 100,000, huku tukiamini itakuwa mkombozi kwa watu wote kwa sababu haina haja ya kusubiri mshahara hadi utakapoingia ili utatuwe tatizo lako maana utakopa Bayport kwa njia ya Nipe Boost na baadaye utalipa kulingana na utaratibu nafuu kwa watu wote,” Anasema Mbaga.

Mbali na kutoa huduma bora kwa Watanzania, taasisi hiyo pia haipo nyuma katika kusaidia jamii ambapo katika mwelekeo wa kusherehekea miaka 10 ya huduma zao, imewakabidhi majengo ya madarasa matatu na ofisi ya walimu kwa Kituo cha yatima cha Kibaha Children Village Centre.

Mbaga anasema ingawa wamekuwa wakijitolea kwa mambo mbalimbali kijamii kama vile vitabu na madaftari kwa shule za wanafunzi, kukarabati majengo na kupaka rangi shule, lakini mradi wa Kibaha Children Village Centre unaoendeshwa pia na Equal Opportunity For All Trust Fund (EOTF) ni mkubwa zaidi.

Anasema mradi huo umegharimu jumla ya Sh milioni 200 na kujenga majengo ya kisasa ambayo yamezingatia ubora na upeke kwa ajili ya kusaidia watoto yatima na wale watakaosoma hapo kulingana na sera ya kituo hicho kwa dhamira ya kusaidia jamii nzima.
“Niwahakikishia Watanzania huduma bora na kuwataka waendelee kutuunga mkono kwa kupata huduma za mikopo kutoka kwenye taasisi yetu ili wajikwamue kiuchumi,” anasema.

Pamoja na mambo mengine anasema katika kipindi cha mwaka 2015 na 2016 wamekopesha Sh bilioni 48.

Aidha, akizungumzia miaka 10 ya taasisi hiyo, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Angellah Kairuki, anaipongeza Bayport kwa huduma bora ya mikopo nchini Tanzania.

Anasema huduma zinazotolewa na Bayport zimechangia kuboresha maisha ya watumishi wa umma wanaotumia taasisi hiyo katika suala la mikopo ambayo serikali inaamini na kutambua juhudi za sekta ya taasisi za kifedha kwa manufaa ya nchi kwa ujumla.
“Serikali inatambua huduma bora za mikopo inayotolewa na Bayport sambamba na kushukuru pia namna mnavyoshiriki katika kazi mbalimbali za kijamii zinazoambatana na kusaidia jamii yenu, hivyo sisi kama serikali tunawapongeza na kuahidi kushirikiana na nyie kwa namna moja ama nyingine.

“Endeleeni kutoa huduma bora zinazojali maslahi ya wateja wenu kwa kubuni huduma rafiki ili Watanzania waendelee kiuchumi kwa sababu ndio lengo la serikali kuona nchi yetu inapiga hatua kubwa, hivyo tunaamini kwa kupitia nyie Bayport kila kitu kinawezekana,” anasema.

Aidha, anawataka Bayport kutafuta namna ya kupanga marejesho nafuu ili watu wengi waweze kukopa katika taasisi yao kwa ajili ya kuongeza kipato katika maisha yao, ukizingatia kwamba wapo watu wengi wanashindwa kupata fursa ya mikopo kwa kushindwa uwezo wa kulipa mkopo wake.

Maadhimisho ya mwaka huu ya taasisi hiyo yalikuwa na lengo la kuonyesha baadhi ya wageni waalikwa namna taasisi yao ilivyopiga hatua kutokana na kutoa huduma bora tangu ilipoanzishwa nchini Tanzania mwaka 2006.