Home Makala TUSIGEUZE BUNGE KUWA SEHEMU YA ‘VITA’

TUSIGEUZE BUNGE KUWA SEHEMU YA ‘VITA’

454
0
SHARE

NA FARAJA MASINDE,

MOJA ya maamuzi ambayo yamejiri bungeni siku chache zilizopita na kuwaacha wananchi wengi vinywa wazi ni juu ya uamuzi uliochukuliwa na Spika wa Bunge, Job Ndugai wakutangaza kuwafungia kutokuhudhuria vikao vyote vya mkutano wa saba wa Bunge wa nane na ule wa tisa kwa kudharau mamlaka ya Spika  Mbunge wa jimbo la Kawe, Halima Mdee na Mbunge wa jimbo la Bunda Mjini, Esther Bulaya wote kutoka Chadema.

Kwa rungu hilo la Spika wabunge hao sasa watakosa vikao vya Bunge hadi mkutano wa 10 mwakani katika bunge la Aprili 2018/2019. Maamuzi hayo yalifikiwa na bunge hilo baada ya kukubaliana  na hoja ya kubadilisha maazimio ya Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bungeiliyowasilishwa na Mbunge wa viti maalum, Juliana Shonza(CCM).

Mbali na ‘kitimoto’ cha wabunge hao, pia Spika Ndugai alisema kikosi cha askari  kilichokuwapo  bungeni hapo june 2 mwaka huu na kusita kuchukua hatua za kumtoa nje kwa wakati Mbunge wa Kibamba, John Mnyika(Chadema) kimeondolewa na kuletwa kingine, kikosi hicho kinadaiw akuwa na askari 10.

Kwa mujibu wa bunge kosa lilofanywa na Mbunge Bulaya ni lile la kudaiwa kudharau mamlaka ya Spika kwa kukaidi maelekezo yaliyomtaka kutulia kuruhusu mjadala wa Wizara ya Nishati na Madini uendelee, ambapo alionekana akitangatanga na kuhama sisha wabunge wa upinzani kutoka nje ya ukumbi wa Bunge.

Upande wa mbunge, Mdee anatuhumiwa kudharau mamlaka ya kwa kufanya fujo kwa askari waliokuwa wameamuliwa kumtoa nje mbunge Mnyika kwa kuwavuta sare zao za kazi kwa nia ya kuwazuia kutekeleza agizo lililotolewa na Spika.

Binafsi sijakuunga mkono uamuzi huu wa kukaa nje ya bunge kwa muda wa mwaka mmoja kwani hii ni sawa na kuwaondolea wananchi haki yao ya kikatiba ya kuwa na mwakilishi bungeni.

Si pingi kwamba wabunge hawa huenda walikosa kwa namna moja ama nyingine lakini siamini kwamba adhabu hii iliyofikiwa na bunge ya kuwaweka nje ya viunga hivyo vya bunge ndio ulikuwa uamuzi wa mwisho na bora kuliko mwingine.

Hii ni sawa na kuwaadhibu wananchi wa majimbo ya Kawe na Bunda Mjini kwa kosa ambalo lingeweza kutafutiwa adhabu mbadala kuliko kuwaadhibu wananchi hawa kwa kipindi ncha mwaka mmoja.

Kwani sote tunatambua kuwa wananchi ndio wanaoumia kwenye uamuzi huu kufuatia hatuo hiyo ya wawakilishi wao kupewa adhabu ya kitokuhyudhuria vikao hivyo.

Inaumiza kuona kwamba bunge limeamua kupitisha adhabu hii ya kumfungia mbunge kutokuhudhuria vikao kadha wa kadha kama njia bora zaidi ya kufundisha na kuonya kwa baadhi ya wabunge wanaoenenda kinyume ilihali kuna namna nyingine mbayo wabunge hawa wangeweza kuadhibiwa kwa kuzingatia kanuni za bunge.

Safari yetu hii huenda isiwenjema sana iwapo tutatumia mabavu na nguvu hata mahala pasipohitaji uzito huo, nah ii itapelekea kuibua chuki baina ya wananchi na Bunge jambo ambalo halitakuwa na afya kwa ustawi wa taifa letu kwa ujumla.

Vitisho, ukali, jaziba, hasira siyo miongozo sahihi sana ambayo unapaswa kuendelea kutumiwa na viongozi hususan wa bunge katika kutoa maamuzi, kwani licha ya kuwa na nia ya kutaka kuheshimiwa lakini inaweza kupelekea kuwa mzizi wa chuki kwa wananchi kufuatia kuadhibiwa vilivyo kwa wawakilishi wao ambao adhabu hizo wangeweza kuzikabili kwa namna nyingine mbali na kuzuiwa kuhudhuria vikao.

Inawezekana adhabu hii ikawa haina ukakasi wowote kwa mbunge husika kwa vile bado atakuwa na uhakika wa kupokea nusu ya mshahara wake kila mwezi pamoja na posho nusu kwa mujibu wa kanuni ya 75 ya kanuni ya kudumu za Bunge kama zilivyofanyiwa marekebisho januari, 2016.

Lakini pia viongozi wa bunge hawana budi kuongoza chombo hicho kwa kufuata haki na usawa kwani inaonyesha chombo hicho muda mwingine kimekuwa kikienda mlama kutokana na kelele nyingi za wapinzani kushindwa kusikilizwa.

Hali hii itajenga hofu kubwa kwenye bunge letu hususan wabunge wa upinzani ambao watakuwa hawako huru kutoa kile wanachokiamini kuwa hakiko sawa.

Turejeshe muamko wa bunge wa kuwa sehemu bora ya kushindana kwa hoja, tutoe uhuru uliosawa kwa kila upande ili kama ni kupingana watu tupingane kwa hoja kwani kwa namna hali ilivyo ni ngumu kwa bunge kuweza kurejesha hadhi yake kama mhimili muhimu kufuatia kuwapo kwa mpepesuko huu wa haki na kanuani ambazo zimekuwa zikishambulia upande mmoja zaidi.

Kusimamia sheria pasi kuwa na upendeleo ndio silaha pekee ambayo itarejesha heshima ya bunge tofauti na sasa ambapo pana taka kuonekana kama nni sehemu ya vita kwa wabunge kutolewa kwa nguvu bila ya kujali hadhi aliyonayo mbunge.

Heshima hii tunayowavunjia wabunge hawa kwa kuwasukuma kama ‘mwizi’ ndio mwanzo kuendelea kulishushia hadhi bunge letu hili ambalo kwa miaka mingi ambayo limekuwapo ilikuwa nadra kushuhudia vitendo hivi  vya wabunge kuondolewa kama watu wasio na mchango katika taifa hili.

Chuki hizi tunazozitengeneza haziwezi kuwa na msaada wowote katika kujenga taifa na badala yake itakuwa ni kichocheo cha mpasuko tu baina ya pande mbili ambao hata hivyo hautakuwa na faida yoyote kwa taifa.

Binafsi nafikiri ipo haja ya kujifunza kwenye mabunge yaliyoendelea namna ambavyo wamekuwa wakiwashughulikia wabunge ambao wanaenenda kinyume na maamuzi ya spika ili kuleta afya kwenye bunge letu kuliko kubakia na hii moja tu ya kuwafungia vikao na kuibua chuki zisizo za lazima bila kujua kuwa tunawaumiza wananchi wetu majimboni ambao wanakero nyingi zinazowakabili na ndio waliowapa ridhaa wabunge hao.

Sitaki kuamini kuwa changamoto za jimbo la Kawe au Bunda mjini kuwa zimekwisha malizika, hivyo naamini uamuzi wa namna hii utafikiriwa tena ili kuzingatia mahitaji makubwa ya wananchi hawa ambao wanaamini kuwa ni wabunge wao pekee ndio wanaoweza kuwasaidia kufikisha vilio vyao serikalini.

Tunajenga nyumba moja ambayo ni Tanzania, hivyo sidhani kama ni sahihi kuanza kujenga mpasuko kwa sababu tu ya itikadi zetu za vyama.

Hivyo natarajia kuona busara za Spika zikitumika katika kuhakikisha kuwa wawakilishi hawa wa wananchi wanaadhibiwa kwa namna nyingine tofauti na hivi ilivyo hivi sasa.

Inawezakana pia wakapewa namna nyingine ya kutumikia adhabu yao huku wakiendelea kuwawakilisha wananchi wao ambao ndio waliowapa ridhaa kwani ndio waliowaweka hapo walipo.

Vile vile itakuwa ni busara pia kwa ‘watuhumiwa’ hawa ambao wamekuwa wakinyooshewa kidole cha kuwa na lugha zenye kuudhi mamlaka pamoja na matendo yao, kujirekebisha na kurejea kwenye mstari ulionyooka kwa manufaa ya taifa kwa ujumla.

Pia hili linatakuwa kuwa angalizo kwa wabunge wengine kwani tayari Rais Dk John Magufuli amebariki wabunge wote wataoenenda kinyume kushuguliwa ipasavyo na Spika.

 Naomba kuwasilisha.