Home Makala UCHAGUZI MBOVU UTAENDELEZA MAUMIVU YA WASOMALIA

UCHAGUZI MBOVU UTAENDELEZA MAUMIVU YA WASOMALIA

869
0
SHARE

NA HILAL K SUED


UHALALI wa mchakato wa uchaguzi nchini Somalia umo katika mtihani mkubwa kutokana na tuhuma nyingi zilizozagaa za kuwepo kwa udanganyifu na vitisho.

Chaguzi zinazoendelea – zilizoanza mwezi Oktoba mwaka jana na zinazohusisha ‘wapigakura’ 14,025 waliotakiwa kuchagua Wabunge 275 – ulitakiwa uwe kama ishara muhimu katika njia nyofu ya kupita kuelekea democrasia ya sanduku la kura. Lakini madai ya ukiukwaji mkubwa katika chaguzi hizo umetishia uhalali wa mchakato mzima.

Wagombea kadha wa Ubunge wamekuwa wakipambana na vitisho na hata kushambuliwa na magenge ya wapinzani wao ili wajitoe. Na katika hatua nyingine, mamia ya miongoni mwa wagombea wamejitoa na na kubakia mmoja tu.

Katika tukio moja, mwanamama mmoja, Mumunio Saeed Mursal – mgombea katika Bunge la Juu amesema alikamatwa na kupigwa na askari, na baadaye akakukta jina lake limeondolewa kutoka kwenye kinyang’anyiro kutokana na barua aliyodai ya kughushi kutoka kwake.

Katika maeneo mengine, wagombea wamedaiwa kuhjiusisha na rushwa ambapo fedha nyingi zinatumika katika kununua kura.

Wiki iliyopita Mkaguzi Mkuu wa Mahesabu Nur Jimale Farah amesema baadhi ya kura hununuliwa kwa bei ya Dola za Kimarekani 5,000, 10,000 hadi 20,000 au 30,000 kwa ‘mpigakura’ mmoja. Ameongeza kwa kusema kwamba kuna viti viwili vilivyogombaniwa sana ambapo kila mshindi wa viti hivyo alitumia zaidi ya Dola za kimarekani 1.3 milioni katika kutoa milungula kwa ‘wapigakura’.

Alisema hiki kinatokea wakati duru jipya la ukame nchini linatishia maelfu wa Wasomali katika baa kubwa la njaa.

Na madai yote haya ya rushwa ya kura  yameenea karibu kila eneo na mamlaka inayosimamia mchakato huo – Indirect Electoral Dispute Resolution Mechanism (IEDRM) umeagiza kufanyike uchunguzi iwapo baadhi ya matokeo ya upigaji kura yafutwe.

Hata hivyo, viti 14 vya awali vinavyotakiwa vichunguzwe, vilipunguzwa hadi kuwa 11 bila ya maelezo yoyote kutolewa. Isitoshe mwezi uliopita – Desemba 2016, taasisi moja inayoundwa na wanasiasa inayoratibu mchakato huo wa uchaguzi – National Leadership Forum (NLF) – iliamua kutupilia mbali agizo la kufuta matokeo yote yale yalitiliwa shaka ya kuwepo kwa udanganyifu.

Na jinsi Umoja wa Mataifa (UN), Umoja wa Afrika (AU) na Umoja wa Ulaya (EU) zinavyozidi kuwa katika hali ya kutoridhishwa na nchi nyingine yanayoendelea mwezi uliopita waliamua kutoa kauli ya kipamoja.

Kauli hii ilibeba maneno makali kuliko taarifa nyingine zilizowahi kutolewa. Ilisema: “Kama washiriki wa kimataifa tunaamini kwamba uhalali wa mchakato mzima wa uchaguzi uko katika hati hati kubwa. Ucheleweshaji na kushindwa kuchukua hatua kwa wote waliohusika na vitendo vya ukiukwaji na udanganyifu unazidisha kutufanya kupoteza imani katika kuisaidia nchi hiyo katika kusimika demokrasia halisi.”

Baadaye, nchi za Sweden, Uingereza na Marekani nazo zilikuja na kauli ya kipamoja ya kuikumbusha Somalia kuhusu suala la uraia wa nchi mbili kwamba vitendo vyote vya ufisadi vinavyofanywa na Wasomali wanaoishi katika nchi hizo bado vianaweza kushughulikiwa chini ya nchi zao.

Hata hivyo Desemma 27 Jaji Mkuu wan chi hiyo aliwaapisha Wabunge 243, pamoja na wale walituhumiwa katika ukiukwaji wa sheria za uchaguzi hususan utoaji wa milungula kwa wapigakura.

Njia ambayo Somalia imechukua kuhusu mchakato wa chaguzi za kidemokrasia umekuwa unatia wasiwasi sana iwapo kweli nchi hiyo ina dhamira ya kujinasua kutoka katika miongo kadha ya vurugu, mauaji, kutoweka kwa utawala wa sheria na hata uwezo wa ubunifu wa kuchukua njia nyofu ya kuyaondoa hayo.

  • Makala hii imetayarishwa kwa msaada wa vyanzo mbali mbali vya Intaneti.