Home Uchambuzi Afrika UINGEREZA YAPIGANIA KOLONI LAKE LA MWISHO  AFRIKA

UINGEREZA YAPIGANIA KOLONI LAKE LA MWISHO  AFRIKA

4256
0
SHARE

NA HILAL K SUED


Jumatatu ya wiki iliyopita Mahakama Kuu ya Kimataifa ya Haki (International Court of Justice -ICJ) ilyopo The Hague, Uholanzi ilianza kusikiliza kesi ambayo inaweza kuamua hatima ya Visiwa vya Chagos – ambavyo ni koloni lake lililobakia la Uingereza katika Bara la Afrika.

Nchi 22 zimepeleka maombi kwenye mahakama hiyo ya kuomba kuhusishwa na sxhauri hilo. Wanaoiunga mkono Uingereza katika dai lake la kuendelea kukalia visiwa hivyo ni Marekani, Australia, na Israel.

Marekani inamiliki kituo kikubwa cha kijeshi cha baharini katika kisiwa cha  Diego Garcia, ambacho ni kimojawapo cha visiwa hivyo, sehemu ya dunia ambayo imekaa vyema kimkakati katika masuala ya ulinzi kwa majeshi ya baharini.

Kwa upande wao, Wanaopinga Uingerteza kuendele kuvikalia visiwa hivyo ni Mauritius, ambayo inadai kwamba visiwa hivyo vinapaswa kuwa chini ya himaya yake.

Mataifa mengine 17 yanaiunga mkono Mauritius – Belize, Botswana, Brazil, Cyprus, Germany, Guatemala, India, Kenya, Marshall Islands, Nicaragua, Nigeria, Serbia, Afrika ya Kusini, Thailand, Vanuatu na Zambia. Umoja wa Afrika (AU) pia umetuma wawakilishi kuunga mkono Mauritius.

ICJ inasikiliza kesi hiyo baada ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kupiga kura kuunga mkono Azimio lililodhaminiwa na Mauritius kutaka maoni ya kisheria kutoka mahakama hiyo. Hata hivyo hukumu ya mahakama hiyo utakuwa wa ‘kiushauri” tu na hautakuwa na mkazo wa sheria.

Miaka 250 iliyopita, wahamiaji walianza kuingia visiwa hivyo, wengi wao wakiwa ni watumwa kutoka Bara la Afrika na pia vibarua kutoka India. Wakati wa kipindi cha ukoloni, visiwa hivyo vilichukuliwa kama sehemu ya Mauritius na utawala wake uliendeshwa kutoka huko.

Kutokana na udogo wake kieneo na kukosekana kwa mali asili, visiwa hivyo havikuwa vinatiwa maanani sana na mataifa mengine, ya mbali nay a jirani.

Lakini mambo yalianza kubadilika kwa haraka sana baada ya Vita Baridi kushika kasi. Marekani ilitambua kwamba eneo la upweke (kiumbali) la Visiwa vya Chagos lilikuwa ni sehemu muafaka kwa ajili ya kituo cha kijeshi katika Bahari ya Hindi.

Uingereza nayo, mshirika mkuu wa Marekani katika hiyo Vita Baridi ilikuwa tayari kutoa ushirikiano, na hatimaye mkataba ukasainiwa uliokodisha Marekani eneo la Diego Garcia kwa miaka 50 kwa kodi ya Dola moja ya Kimarekani kwa mwaka.

Hata hivyo kulikuwapo ugumu mmoja: kipindi hicho kilikuwa ni kipindi cha kudai uhuru kwa nchi za Bara la Afrika, na mwaka 1968 Mauritius ilikuwa ikikaribia kutoa uhuru kwa koloni lake la Mauritius. Swali lilikuwa ni je, serikali mpya huru ya Mauritius inaweza ikapewa uangalizi wa kituo hicho cha kijershi?

Ili kuondoa wasiwasi huo, serikali ya Uingereza ilivivamia Visiwa vya Chagos na kwa nguvu iliwaondoa wakazi wote wapatao 2,000 wa visiwa hivyo, ambao rasmi walijulikana wakati huo kama “Tarzans” na “Man-Fridays” ili kutoa ulinzi kamili wa kituo hicho cha kijeshi cha Diego Garcia. Uhamishaji wa nguvu wa wakazi hawa ulichukuwa miaka kadha na uliambatana na ukatili mkubwa.

Mwanahistoria wa elimu ya viumbe David Vine alielezea kilichotokea: “Maafisa wa Uingereza, wakisaidiwa na wale wa jeshi la baharini waliwakusanya mbwa wote wa wakazi hao, waliwapa sumu na kuwachoma moto katika mabanda yaliyofungwa.

“Baadaye waliwaamrisha wakazi wote waliobakia kuingia katika meli za mizigo  zilizojazana watu. Wakati wa uondoshaji huo ambao ulifanyika kwa hatua hadi Mei 1973, wakazi wengi wa visiwa hivyo walikuwa wanalala katika sehemu ya mizigo juu ya kinyesi cha ndege.

“baada ya safari ya siku tano, matapishi, mikojo na kinyesi vilitapakaa sehemu zote za meli, na mwanamke mmoja aliharibu mimba.

“Walipowasili Mauritius na Visiwa vya Shelisheli wahamishwaji hao walitelekezwa bandarini, walikuwa hawana makazi, kazi na hawakuwa na fedha, na wala fedha za kuwasaidia hazikutolewa.