Home Latest News Usalama wa mashabiki viwanjani mashakani

Usalama wa mashabiki viwanjani mashakani

1056
0
SHARE

NA ASHA Muhaji,

PENGINE ile dhana ya kuwa Tanzania ni nchi ya amani ndiyo inayowapa kiburi wananchi wakiwemo mashabiki wa soka nchini kama haitakuja kutokea maafa katika biwanja vya soka.

Mchezo wa soka ni mchezo pekee wenye uwezo wa kukusanya mashabiki wengi pindi unapofanyika. Inakadiriwa kuingiza mashabiki kati ya 15,000 hadi 60,000 katika mechi zake nyingi kulingana na uwezo wa viwanja husika.

Kwa idadi hiyo ya mashabiki ni dhahiri suala la usalama ni kitu muhimu sana ndani ya viwanja vinakofanyika michezo hiyo. Lakini hali inayoonekana hivi sasa ni kama suala la usalama limekuwa likifanyika kimazoea tu.

Tukio la hivi karibuni la vurugu lililotokea katika pambano la watani wa jadi nchini Simba na Yanga, Uwanja wa Taifa kiasi cha mashabiki wa klabu inayodaiwa kuwa ni wa Simba kung’oa viti na kuvirusha katikati ya uwanja ikiwa ni ishara ya kutorishwa na maamuzi ya mwamuzi Martin Saanya kuwa haitendei haki timu yao, limeacha maswali kibao iwapo kweli hali ya usalama uwanjani hapo ilikuwa ya kiwango cha kuridhisha.

Katika tukio hilo ambalo iliwalazimu polisi kutupa mabomu ya machozi na kusababisha taharuki kubwa kwa mashabiki waliokuwepo uwanjani humo kuanza kukimbia hovyo kwa lengo la kujinusuru maisha yao, lilisababisha uharibifu wa viti vipatavyo 1700.

Mara moja Serikali ambayo ndiyo mmiliki wa Uwanja huo ilitangaza kuufungia kutumiwa na klabu hizo mbili sambamba na kuzuia mapato ya mchezo huo mpaka hapo ukarabati wa uharibu uliotokea kufanyika.

Ukilitazama tukio husika ni kweli polisi walikuepo uwanjani lakini swali la kujiuliza Je ni kweli wanafika hapo kusimamia majukumu kikamilifu? Kumbukumbu zinaonesha wazi kwa ujumla hali si salama kama inavyodhaniwa.

Inashangaza kuona idadi kubwa ya polisi waliofurika uwanjani siku ya pambano walishindwa kumkamata hata shabiki mmoja tu aliyeshiriki vurugu zile na badala yake kuziachia mzigo mkubwa klabu kulipa fidia.

Kwa mtazamo huo ni vigumu kukomesha vurugu ikiwa kila mara zinapotokea hakuna wahusika wanaotiwa nguvuni. Ajabu kubwa uwanja kama ule uliojengwa kwa mamilioni ya fedha eti hauna kamera za kubaini matukio mabaya uwanjani hapo.

‘Dalili ya mvua ni mawingu’, au ‘Panapofuka moshi pana moto’ hivyo ndivyo inavyoelekea kwa soka la Tanzania hivi sasa. Dhana ya usalama wa mashabiki katika viwanja vya soka inachukuliwa kama hoja nyepesi sana huenda siku yakitokea  maafa ndipo wakubwa watashtuka.

Wengi walidhani matukio ya fujo na vurugu yaliyowahi kutokea katika baadhi ya mechi katika miji mbalimbali hapa nchini kuwa kama angalizo la vyombo vyenye mamlaka ya usimamiaji na mchezo huo kuboresha usalama ndani ya viwanja vyote.

Ilikuwepo dhana kuwa mashabiki wa klabu kubwa za Simba na Yanga pekee ndiyo wenye kusababisha vurugu lakini uchunguzi unaonesha mashabiki wote wa soka kwa ujumla ni wenye hulka za jazba pindi wanapodhani mambo hayaendi sawa kwa timu zao.

Kawaida polisi wanaofika viwanjani hupenda kujazana ndani ya uwanja na mara nyingi wamekuwa ‘busy’ kufuatilia mchezo na sio kuangalia usalama. Haishangazi kuona baada ya tukio ndipo hushituka na kuanza kutekeleza majukumu yao.

Wengi tumekuwa tukishuhudia utendaji kazi wa polisi katika nchi za wenzetu ambapo hukaa hadi sehemu za kukaa mashabiki jukwaani huku pia wengine wakiwageukia mashabiki kwa juda wote wa mchezo na sio kuangalia mpira.

Laiti kama kungekuwa na utaratibu wa polisi kusimama katika baadhi ya majukwaa wanaokaa mashabiki ni wazi fujo au vurugu za ana hiyo zisingeweza kutokea.

Lakini pia kutochukuliwa hatua kali kwa mashabiki wa soka inaweza kuwa ndiyo njia ya kuwapa kiburi zaidi wakorofi wanaoharibu amani ndani ya viwanja vya soka.

Mtindo wa polisi kulipua mabomu kama njia ya kutisha mashabiki si sahihi wala salama kwani katika sheria za CAF na FIFA hali hiyo ikitokea ni wazi pambano linatakiwa kuvunjika.

Ulipuaji wa mabomu ni ishara kuwa hali si salama na iwapo inajitokeza katika mechi ya kimataifa ni dhahiri timu mgeni anaweza kupewa ushindi iwapo atalalamika na kuwasilisha vielelezo.

Tumeshuhudia maafa makubwa yakitokea katika baadhi ya nchi kutokana na fujo au vurugu zinazofanana na hizi zilizotokea hivi karibuni. Je tusubiri maafa ndipo tuzinduke? TFF Usipoziba ufa utajenga ukuta.

Misri wanaweza kuwa na kumbukumbu nzuri kufuatia kupoteza mashabiki zaidi ya 70 na kuwaacha wengine kwa mamia wakiwa majeruhi katika pambano baina ya Al Masri na Al Ahly. Chanzo cha vurugu hizo ni mashabiki wa Al Ahly kutoridhishwa na kipigo cha mabao 3-1.

Mwaka Jana dunia ilishuhudia maafa makubwa nchini Ghana ambapo mashabiki wa soka wanaokadiriwa kufikia…..walifariki katika tukio kama hilo.

Nchini Afrika Kusini katika pambano la watani wa jadi,kati ya Kaizer Chiefs na Orlando Pirates burugu zilizuka baada ya mashabiki wa Orlando kuwavamia wenzao wakiwa na visu nakusababisha tafrani kubwa iliyoacha mashabiki 42 wakipoteza maisha. Kama hiyo haitoshi tukio kama hilo likajirudia tena mwaka 2001 na kusababisha mashabiki 43 kupoteza maisha.

Ukiacha matukio ya hayo na mengine, vurugu kama hizo ziliwahi kutokea katika mechi kati ya Mbeya City na Yanga misimu mitatu iliyopita katika Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya na kusababisha uharibifu wa mali kadhaa sambamba na mchezo baina ya Mbeya City na Prisons katika msimu huo huo.

Lakini msimu uliopita tu tumeshuhudia pambano la Coastal Union na Yanga mjini Tanga likigubikwa na vurugu za aina hiyo ambazo nusura zilete madhara zaidi kwa mwamuzi kupigwa jiwe na mashabiki achilia mbali uharibifu wa mali kwa mashabiki kuvunja mageti na miundombinu ya uwanja.

Mashabiki wa Simba walisababisha vurugu na kusababisha mabomu ya machozi kulipuliwa uwanjani hapo wakati ikipambana na Kagera Sugar katika moja ya mechi za Ligi Kuu.

Yanga nayo imefanya matukioa ya aina hiyo mara kadhaa wakati ikishiriki michuano ya kimataifa dhidi ya TP Mazembe ambapo walivunja mageti. Lakini pia ikicheza dhidi ya …..mwaka mashabiki wake waling’oa viti kwa hasira wakichukizwa na kipigo cha mabao …..

Bila shaka baadhi ya matukio hayo yalitosha kabisa kutoa somo kwa malaka husika kuweka njia za kukabiliana na mashabiki wa aina hiyo ili kulinda usalama wa kweli ndani ya viwanja vya mpira.

TFF, chombo chenye dhamana ya kusimamia mchezo huo hapa nchini hakiwezi kukwepa lawama zozote zitakazotokea kutokana na kushindwa kuweka mikakati madhubuti ya kuwakabili mashabiki korofi. Bado hawajachelewa wanaweza kuanza sasa.