Home Latest News USHINDI WA TRUMP MAZINGAOMBWE

USHINDI WA TRUMP MAZINGAOMBWE

1115
0
SHARE
Donald Trump

WAHINGTON D.C.

Shirika la Ujasusi la Marekani (CIA) sasa linaamini pasi shaka kwamba Russia ilikuwa inamsaidia Donald Trump ashinde uchaguzi dhidi ya Hillary Clinton. Nchini Marekani, habari hii wiki iliyopita imeibua ushabiki wa kisiasa zaidi kuliko uzalendo.

Na ndiyo maana hivi karibuni viongozi wa chama cha Republican na kile cha Democratic wameonekana wakikwaruzana upya kuhusu kujiingiza kwa Russia katika mchakato wa uchaguzi wa Marekani mwezi uliopita.

Hata hivyo tuhuma kuu inayogonganisha vichwa ilikuwapo kwa miwezi kadha – kwamba mwaka 2015 na tena mwaka huu vikundi viwili vya udukuzi wa tovuti vyenye uhusiano wa kijasusi na Marekani waliungilia mfumo wa tovuti wa makao makuu ya Chama cha Democratic mjini Washington DC na pia katika mfumo wa barua peoe wa watu mashuhuri kama vile John Podesta, aliyekuwa mwenyekiti wa Kamati tya Kampeni ya Bi Hillary Clinton na baadaye kuzituma baadhi ya barua pepe za kusononesha kwenda mtandao wa Wikileaks na kuziweka hadharani.

Na kabla ya uchaguzi wa mwezi uliopita taarifa ya pamoja kwa umma iliyotolewa na Mkurugenzi wa Masuala ya Kiintellijensia na Waziri wa Usalama wa Ndani ilisema kwamba taasisi za kijasusi zilikuwa zina uhakika pasi shaka kwamba serikali ya Russia iliagiza kufanyika kwa udukuzi huo.

Hata hivyo taarifa hii haikuwastua wafuasi wa  Donald Trump ambao walikuwa wamemsikia mgombea wao akitilia shaka taarifa hizo za kiintellijensia, na badala yake walikuwa wanashabikia zaidi yale yaliyokuwemo katika barua pepe zile zilipochapishwa kwenye vyombo vya habari.

Kwa Trump, hili lilionekana ni ushahidi zaidi wa kuonyesha kwamba Hillary alikuwa ni ‘muovu’ pasi shaka na si kwamba serikali ya Russia ilihusika katika kumuangusha kwa niaba ya Trump

Lakini haya yote yalionekana kubadilika siku chache zilizopita – kutokana na habari zilizoandikwa kwenye magazeti ya New York Times na Washington Post – kwamba sasa inafahamika CIA iliwataarifu wajumbe waandamizi wa Bunge la Marekani (Congress) kabla na baada ya uchaguzi kwamba kwa ujumla dhamira ya Russia si tu ililenga kudhoofisha imani ya Wamarekani kuhusu demokrasia yao, bali pia ni kuhakikisha Hillary Clinton anashindwa uchaguzi.

Pengine haya mapya yaliyojiri hayatakuwa yamebadilisha mawazo ya Wamarekani. Wafuasi wa chama cha Republicans na viongozi wao ambao wanamchukia Hillary Clinton bado wanachekelea kwamba mama huyo alishindwa uchaguzi. Na wale wafuasi wa Clinton wnaomchukia na/au kumuogopa Trump wamepata sababu nyingine kubwa ya kufanya hivyo – kujiingiza kwa Russia katika masuala ya Marekani, kitu ambacho Trump atapata tabu kukipuuza.

Na uingiliaji huu wa Russia katika nchi nyingine kadha za Magharibi sasa umekuwa kama kirusi kinachosambaa na kinachoshambulia mfumo mzima wa demokrasia za nchi hizo.

Kwa hali ya kawaida Marekani imekuwa ikijilinda na uingiliwaji huu kutokana na ‘umoja’ mkubwa uliopo baina ya vyama viwili vikuu vya siasa dhidi ya uingiliaji wa aina yoyote kutoka nje.

Aidha Marekani siku zote imekuwa ikijigamba kumiliki mifumo ya kisasa kabisa ya kujilinda kiintellijensia na udukuzi wa tovuti, na kama makachero wa CIA wanawaambia viongozi wa Bunge lao, hasa wale wajumbe wa kamati za kiintellijensia kuhusu vitendo vya ki-uadui kutoka taifa la nje, kinachotarajiwa ni kuwepo kwa mshikamano wa kizalendo na wa kipamoja baina ya vyama vikuu. Mshikamano huo wa kizalendo sasa hivi haupo.

Lakini tatizo kuu si kwamba viongozi wote wa chama cha Republicans Bungeni wanazipuuza taarifa za Russia kuingilia uchaguzi wao. Wenyeviti wa kamati za Bunge hilo wameahidi vikao vya dharura kulijadili suala hilo

“Kamwe hatuwezi kuruhusu serikali za nje kuingilia demokrasia yetu,” alisema wiki iliyopita Mwakilishi (Representative) Michael McCaul wa kutoka Jimbo la Texas ambaye ni mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Masuala ya Usalama wa Ndani.

Naye Seneta John McCain wa Arizona, na Mwenyekiti wa Kamati ya Vyombo ya Ulinzi na ambaye hana uswahiba na Russia aliwaambia waandishi wa habari wiki iliyopita: “Kila mtu ninayemfahamu amesema Warusi wameuingilia uchaguzi huu. Pia waliuingilia uchaguzi wa 2008, je hii inamshangaza yeyote?”

Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Masuala ya Kiintellijensia, Mwakilishi Devin Nunes kutoka Jimbo la California naye amesema anaamini Russia ni mhusika moja kwa moja pasi shaka, lakini zaidi alizielekeza tuhuma zake kwa utawala wa Barack Obama, akisema azma ya rais huyo ya kutaka kuuweka upya uhusiano wa Marekani na Russia ilimfanya yeye na wakuu wa taasisi za kijasusi kushindwa kubaini njama za nchi hiyo ya Putin dhidi ya taifa la Marekani.

Nunes alilalamika kwamba utawala wa Obama ulizipuuza taarifa nyingi kutoka kwa wajumbe wa kamati za Bunge kuhusu njama zilizokuwa zikipangwa na Russia.

Hata hivyo wafuasi wa Republicans hawataki kukubali ukweli unaojitokeza na kwa ushahidi mkubwa: kwamba utawala wa kibabe ambao siku zote ni hasimu wa Marekani ulifanya kila liwezalo Trump ashinde uchaguzi.

Nunes, ambaye ni mfuasi mashuhuri wa Trump wakati wa uchaguzi alitoa kauli hiyo aliyosema ina ushahidi mwingi wa kimazingira na kiuhalisia pia.

Wafuasi wengine wa Republicans wamekuwa wakilipuuza suala hilo. “Sawa, ni suala zito, lakini tumekuwa tukilisikia kwa muda mrefu sasa,” alitamka Seneta John Cornyn wa jimbo la Texas, na kuongeza; “Hii si habari mpya.”

Ripoti ya Washington Post wiki iliyopita imewanukuu Wabunge wa Republicans wakitoa hoja kwamba haiwezekani kwa Russia kutaka Trump ashinde kwa sababu Trump alikuwa ameahidi kuliongezea nguvu jeshi la Marekani, kitu ambacho akina Putin wasingetaka kukiona kinafanyika.

Na kwa upande wao, Wabunge wa chama cha Demokratic ambao hawana uwingi katika Mabunge yote mawili wamejibu tuhuma hizi kwa kutoa changamoto kwa wenzao kuchukua msimamo wa kizalendo zaidi kuikabili Russia.

Na wamempongeza Rais Obama kwa kuagiza ufanyike uchunguzi wa kina kuhusu suala zima na mataokeo yake yatangazwe kwa umma kabla ya siku ya kuapishwa kwa Trump mwezi ujao.