Home Makala UTANDAWAZI KAMA NYENZO YA UCHUMI

UTANDAWAZI KAMA NYENZO YA UCHUMI

4025
0
SHARE

NA MARKUS MPANGALA


MWANAZUONI Ayub Rioba aliwahi kujadili suala la sera zenye maudhui ya uchumi kwa jina la “Ujepari”. Tafsiri yake ilikuwa juu ya kuunganisha nguvu za Ubepari na Ujamaa, akipanua mjadala uliowahi kuanzishwa na marehemu Profesa Leonard Shayo.

Kwamba ili mataifa yajiwekee kwenye kambi fulani ya kuendesha uchumi ni zinatakiwa kuchagua kuwa katikati, kati ya Ubepari na Ujamaa ambao ni Ujepari. Wanazuoni wote wawili wanakubaliana na dhana kuwa hakuna ubepari bila ujamaa, na hakuna ujamaa bila ubepari.

Mfano wao wa karibu ulikuwa ni taifa la China. Jambo la msingi ambalo walitufikirisha katika dhana zao ni kujiuliza hili; “mapinduzi ya kiuchumi ya China yalianzaje? Na vilevile China iliwezaje kudumu katikati ya dhoruba za Ubepari?

Suala la utandawazi lilianza miaka mingi iliyopita yaani karne nyingi zilizopita. Wachina wanaelewa kuwa ili kujikita katika utandawazi unatakiwa kufanya mambo makuu mawili; mapinduzi ya kiutamaduni; na pili; mapinduzi ya kisera ambapo yanajikita zaidi kwenye jamii, malengo, mpango, na mikakati.

Kama tunavyojua utandwazi upo kwenye mtaji wa pamoja katika jamii kulingana na sera husika ya nchi. Mtaji wa jamii ni namna serikali zetu zinavyoweza kutunga sera makini za kuhakikisha uchumi unasalia nchini.

Mathalani sheria za kulinda rasilimali, kulinda uchumi na kuhakikisha wananchi wananufaika na utajiri wa mataifa ni pamoja na kuhakikisha mitaji inayozalishwa ndani ya nchi inakuwa chachu ya kutanua wigo wa uzalishaji na kuboresha maisha ya wananchi.

Mwalimu Nyerere aliandika kwenye kitabu cha “Ujamaa ni Imani”, kwamba wawekezaji wanataka faida, wanataka kwenda nazo kwao, lakini sisi kama hatuna mipango au mikakati imara ya kudhibiti kiwango kikubwa cha fedha kwenda nje, basi tutakuwa tunashindwa kunufaika na uwekezaji.

Sasa huo mtaji wa pamoja wa jamii katika nchi hakuna tofauti zozote na itikadi ya ujamaa inayohimiza umilikaji wa mali kwa jamii.

Kwahiyo katika suala la utungwaji wa sera unaambatana na mambo mawili; uwekezaji wa nje kutoka ndani ya nchi, na jambo la pili ni; faida ya uwekezaji katika siasa za kimataifa.

Tuliwahi kueleza hapa kuwa, kampuni kutoka Marekani inapokuwa na wateja wengi Tanzania italazimika kuweka tawi lake hapa. Labda tucuhukue mfano wa karibuni kutoka benki moja ya Afrika kusini imeingia katika soko la Tanzania kufanya biashara ya kibenki.

Hatua hiyo ni utandawazi ambao ni nyenzo ya kukuza uchumi, huwezi kukwepa kusambaza huduma hadi mlangoni kwa mteja.  Je, tuna benki hapa nchi ambazo zimeweza kuanzisha matawi yao Ulaya, Amerika, au Asia?

Kwahiyo hakuna mahali ambapo ujamaa unakataa suala la uwekezaji katika biashara ya kimataifa na misingi ya sera. China walifanya mapinduzi ya kiutamaduni, wakajikita kwenye kilimo, wakaelimisha wananchi wao umuhimu wa kazi na manufaa yake.

China ya leo imeliteka soko la Afrika kwasababu wameamua kutumia utandawazi kama nyenzo ya kukuza uchumi wao hivyo kumsogelea mteja mlangoni kwake lazima usambaze huduma bora. Vivyo hivyo kwenye elimu, vipo vyuo vinaanzisha matawi yao hapa nchini, sababu kubwa ni utandawazi.

Wanajaribu kuwafikia wateja wao popote walipo duniani. Ikiwa watanzania wataamka na kutazama upande wa pili wa utandawazi kupitia elimu, teknolojia na kadhalika, hakuna shaka tutaona mabadiliko makubwa sana katika uchumi wan chi yetu na uchumi wa mtu mmoja mmoja.

Ninachotaka hapa ni kupindua utamaduni wa kubweteka, kupindua utamaduni wa kuamini hiki cha wazungu na hiki ni cha waafrika. Kwahiyo utandawazi tangu karne ya 4 na kuendelea ni nyenzo ya kukuza uchumi, kutangaza lugha na kadhalika.

Wakati huohuo serikali nayo inapaswa kuwa makini katika utungaji wa sera zenye manufaa kwa watanzania kwanza, sio kuwalegezea masharti wawekezaji.

Kama kuna jambo linalotuumiza nchini mwetu, basi sera ni moja ya tatizo kubwa sana. Tunasema wawekezaji, tunaimba wawekezaji lakini hatuzalishi wawekezaji wa ndani.

Hatuzalishi itikadi mpya ya uwekezaji, hatutoi fursa za kutosha kwa wawekezaji wa ndani, hatuwajengei mitaji bali tunataka ‘qualified’ hilo ndio tatizo kubwa.

Matokeo yake hatutengenezi ajira kwa wachonga vinyago, wahunzi na wengineo. Baadhi ya viongozi wetu wanadhani uwekezaji au suala la utandawazi linahitaji watu ‘qualified’ ambao wanaendesha Benz, au wenye ukwasi mwingi benki.

Sera zetu hazioneshi namna ya kuwadhibiti wadanganyifu au vitu vidogo vidogo kuwa vikubwa ndani ya utandawazi. Wakati wa michuano ya kombe la dunia watu walifurahi kuhusu Pweza Paulo. Lakini lile ni jambo dogo sana kwa Ujerumani ambalo likageuzwa kuwa mtaji wa kupata watalii, wanahistoria, watafiti na kadhalika.

Kwenye kilimo tunahitaji wakulima wa ndani wawekewe mazingira ya kurahisisha kazi zao. Habari za kwamba serikali haina fedha ni uzembe, ndio maana mabwana shamba wengi wanasota mijini na kula “cool time” wakati wakulima wanahangaika.

Sera ni usimamizi. Sera ni kukataa kuona nchi yetu inaruhusu Mkurugenzi wa Supermarket anatoka ulaya, Asia au Amerika. Hatuhitaji wawekezaji wa mafundi mchundo, hatuhitaji ofisa mtendaji mkuu kwenye gereji.

Hatuhitaji wawekezaji wa gereji na kadhalika. Kutunga sera za kuweka kipaumbele kwa wazawa sio dhambi, wala tusishikilie onyo hilo la Mwalimu Nyerere, halitusaidii chochote linaweka kikwazo cha kukua uchumi. Kwahiyo haku