Home Makala UVUVI HARAMU SAWA NA DAWA ZA KULEVYA

UVUVI HARAMU SAWA NA DAWA ZA KULEVYA

524
0
SHARE

NA OSCAR ASSENGA,TANGA

WAKATI Serikali ya awamu ya tano chini ya Dk. John Magufuli

ikipambana na dawa za kulevya nchini, lipo dude jingine linaloonekana kubeba sura sawa na mapambano ya dawa za kulevya.

Uvuvi haramu ndilo dude linaloonekana kukaribiana kwa mfanano na dawa za kulevya kutokana na kubeba madhara makubwa kwa viumbe vya baharini ambavyo vinaweza kutoweka.

Kwenye ukanda wa bahari ya hindi na maziwa makuu uvuvi haramu umeshika

kasi kutokana na dhana ambazo zimekuwa zikitumiwa ikiwemo zile za nyavu ndogo na virungu ambazo zinatajwa kuwa mwiba kwa ustawi wa viumbe vya baharini.

Kutokana na hali hiyo Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Uvuvi kutoka Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi Fatuma Sobo anasema suala hilo hivi sasa linaundiwa mikakati mizito ya kuhakikisha linatokomezwa kwa wizara tatu kushirikiana ili iweze kuwa na tija .

Fatuma  aliyasema hayo wakati wa kikao baina yao na madiwani wa halmashauri  Jiji la Tanga,Mkurugenzi na wakuu wa idara ikiwa ni mkakaati wa kuhakikisha rasilimali za bahari zinatunza na kulindwa.

Ambapo alisema waliamua kuweka mikakati hiyo ili kuwezesha urahisi wa kufanikisha jambo hilo kutokana na kuwa wizara hizo zinaweza kukabiliana nalo na kuweza kuleta mafanikio makubwa tofauti na ilivyokuwa huko nyuma.

Alizitaja wizara ambazo zitashirikiana kuwa ni za Maliasili na Utalii,Nishati na Madini,Sheria na Katiba na Ofisi ya Rais ambapo kupitia huko wanaweza kuona namna ya kulibeba hilo kwa uzito mkubwa ambao utasaidia kuondosha changamoto hizo.

“Kupitia mpango huo tunaweza kufanikiwa kukabiliana na vitendo vya uvuvi haramu ambavyo vimekuwa vikifanyika kwenye maeneo mbalimbali hapa nchini na kusababisha uharibifu wa mazalia ya samaki lakini pia kuleta madhara kwa viumbe “Alisema

Fatuma ambaye pia ni Mkurugenzi Msaidizi upande wa wa Idara ya Maendeleo ya Uvuvi kutoka Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi anayeshughulikia masuala ya uendelezaji wa rasilimali za uvuvi alisema rasilimali za bahari ni muhimu kwa ukuaji wa uchumi .

Aidha aliwataka madiwani hao kutumia elimu walioipata kuifikisha kwa wananchi hao juu ya athari za uvuvi haramu ili kusaidia kupunguza tatizo hilo hasa kwenye maeneo ya ukanda wa bahari ya hindi kwani wao ndio wanajua mabomu yanapigwa kwenye maeneo gani.

“Ninaamini kikao hiki kitakuwa mwanga mzuri kwenu nyingi kuona namna ya kusaidia harakati hizi za kupambana na suala la uvuvi haramu kwani limekuwa na athari kubwa lakini sisi kama wizara hivi sasa tunashirikiana na wizara nyengine kwa lengo la kuzibiti suala hilo “Alisema Fatuma.

“Tukiweza kuzuia uharibifu wa mazingira utatusaidia kuzibiti uvuvi haramu lakini pia tushikiane na wananchi hasa wale wanaoishi karibu na fukwe za bahari ya hindi kulinda rasilimali za bahari “Alisema

“Akizungumzia suala la wavuvi wanchi jirani kuingia kuvua hapa nchini alisema ni kosa la kisheria kwani sheria hairuhusu wao kuingia na kuacha kufanya shughuli za namna hiyo kwenye maeneo yetu hivyo wanapaswa kuacha kujihusisha na jambo hilo.

“Sheria haiwahurusu wavuvi kutoka nchi jirani kuvua kwenye nchi nyengine zilizopo jirani bila kuwa na idhini ya mamlaka husika hivyo niwatake wenye tabia za namna hiyo kuacha mara moja “Alisema.

Akizungumza kwa upande wake, Naibu Meya wa Jiji la Tanga (CUF) Mohamed Haniu alisema anaamini kupitia elimu hiyo itawasaidia kushirikiana na kamati za BMU kupambana na uvuvi haramu ambao umekuwa tishio kwenye maeneo yaliyopo pembezoni mwa bahari ya hindi.

“Nisema tunashukuru elimu hii ambayo ni muhimu kwa kutunza na kuvilinda viumbe vya baharini hivyo tutashirikiana na kamati za BMU kuona namna ya kukabiliana na suala hilo kwani rasilimali za bahari zinapasw kutunzwa kwa kushirikiana ili ziweze kuwa na tija kwa Taifa“Alisema Naibu Meya huyo.

Naye Mratibu wa Mradi wa Swiofish katika Halmashauri ya Jiji la Tanga Nkana Mwagala alitoa wito kwa jamii kutunza rasilimali za bahari kwa ajili ya manufaa ya kizazi cha sasa na baadae.

Alisema kupitia kikao hicho wanaamini madiwani watakaa na wananchi hao ili kuweza kuwaelimisha madhara ya kufanya uvuvi haramu ikiwemo kuachana na suala hilo .

“Kwa sababu madiwani wanakundi kubwa la wananchi kwenye maeneo yao hivyo kupitia kikao hiki wanaweza kusaidia kuipa jamii uelewa kuhusu athari za uvuvi haramu lakini pia waweze mabalozi wazuri kuzilinda rasilimali za bahari kwa manufaa ya sasa na kizazi kijacho “Alisema.